Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Kupotosha imekuwa ada ya OMO na anafanya hivyo kutokana na chuki iliyomjaa dhidi ya WatanganyikaKweli yule anapenda sana kupotosha. Nimemshangaa anavyojaribu kupotosha hata issue ya electoral votes za Marekani. State ndogo ni ndogo tu, hata kama electoral college system ikitumika. State yenye 3 electoral votes, kwa mfano, inakuwa na sauti kubwa pale tu candidates wanapokuwa wanachuana vikali kiasi kwamba atakayeshinda hiyo state ndiye atakuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais. Otherwise, candidate anaweza kushindwa uchaguzi small states kibao, yet akashinda uchaguzi kama amezivuna electoral votes za majority ya zile states kubwa zaidi.
Naendelea kumweka wazi kwa kutumia maneno yake, tafadhali rejea clip hii
Clip: OMO anasema mambo ya muungano ni ya pamoja, upande mmoja umeyachukua na Zanzibar haishirikishwi katika kutunga sera ''policy'' yeye akiita sheria
Hoja: Miswada ya serikali inapitia baraza la Mawaziri la JMT.
VP ni mjumbe wa Baraza na Rais wa Zanzibar ni mjumbe tena kwa kuapishwa na Jaji mkuu wa Tanzania.
Mfano, SSH alikuwa VP na Shein Rais wa Zanzibar
Pili, Zanzibar ina Wabunge wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa ambao ni kutoa CCM na ACT
Wabunge wa Zanzibar wanachaguliwa na watu 2,500 kama yule wa ACT Wazalendo kutoka jimbo la ''Donge''
Wakiwa Dodoma wanakura sawa na Mbunge yoyote wa Bunge. Vipi OMO anasema Zanzibar haina uwakilishi?
Tatu, kuna Wabunge 5 kutoka Baraza la Wawakilishi wanaoingia Bunge la JMT, wanalipwa na kodi za Watanganyika kuiwakilisha Zanzibar
Nne, Wabunge wa Zanzibar wanaochaguliwa na watu 2,500 hadi 6,000 wana kura za mambo ya Tanganyika. Wabunge hao wapo katika kamati za Bunge za mambo yasiyo ya muungano . Kwanini OMO haoni ukweli huu? Nani anadhulumika hapo!
Tano, kama sheria zinatungwa JMT na kubambikiziwa Zanzibar, OMO asome kifungu hiki cha katiba ya Zanzibar ya 2010 na aeleza ni kwavipi sheria na sera za JMT zinaweza kutumika Zanzibar bila idhini hii hapa chini
132.(1) Hakuna Sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumika Zanzibar mpaka Sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya Muungano tu na ipitishwe kulingana na maelekezo yaliyo chini ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.
(2) Sheria kama hiyo lazima ipelekwe mbele ya Baraza la Wawakilishi na Waziri anayehusika.
Rejea Clip Dakika 7.29
OMO anasema Zanzibar haiendelei kiuchumia kwasababu haina nyenzo za kuisaidia akizitaja kama
1. Kodi
2. Fedha
3. Mambo ya nje
Hoja: OMO ni makamu wa Rais na kiongozi wa ACT na aliwahi kuwa AG . Katiba ya Zanzibar 2010 inasema ;
133.(1) Hakuna kodi ya aina yoyote itakayotozwa isipokuwa kwa mujibu wa Sheria iliyotugwa na Baraza la Wawakilishi au kwa utaratibu uliowekwa kisheria na uliotiliwa nguvu na Sheria iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.
(2) Masharti yaliyomo katika kijifungu cha (1) cha kifungu hiki hayatalizuia Bunge kutumia mamlaka yake ya kutoza kodi ya aina yoyote inayohusiana na mambo ya Muungano kwa mujibu wa madaraka ya Bunge hilo kwa kujua kwamba mashauriano baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano yamefanywa na kukubalika sehemu zote mbili kabla kupitishwa Sheria.
Suala la kodi llimejibika, tuangalie mengine
Hoja: Suala la fedha halieleweki OMO analizungumzia kwa maana ipi, kwamba, Zanzibar haina pesa au kwamba Zanzibar haina fedha yake! hili ni tata hata hivyo tutafafanua kwa kadri
Bajeti ya Zanzibar 2022/23 inaonyesha mamlaka ya mapato Zbar (ZRB) itakusanya Takribani bilioni 500 na TRA Takribani milioni 400. Pesa hizo zinabaki Zanzibar .
Zanzibar inapata 4.5% ya pato la Tanganyika , kiasi hicho ni kikubwa kuliko makusanyo ya kodi za ZRB na TRA. Kuna mikopo na Misaada na wakati huo huo Bajeti haionyeshi
Matumizi ya wizara ya ulinzi na Usalama
Mambo ya nje
Mambo ya ndani
Taasisi zote za muungano JMT
OMO anapolalamika Zanzibar haina pesa yeye angetaka ipate nini zaidi?
Kama OMO anataka Zanzibar iwe na sarafu yake basi aseme wazi '' vunja muungano''
Hoja: Wizara ya mambo ya nje ni ya muungano. Hatuwezi kuwa na muungano tukiwa na uwakilishi mara mbili.
Laiti ingalikuwa hivyo tungalikuwa na viti viwili katika UN. Ni wapi Zanzibar inanyimwa fursa?
Kuhusu kukopa, OMO afahamu Tanzania kuwa mdhamini wa Zanzibar ni baraka si ugonjwa kama anavyotusi
China wanajua akiwa AG, OMO aliongoza Zanzibar kukataa kulipa deni la Tanesco la Bilioni 50+ takribani dola milioni 16. Wachina wanajua Dollar milioni 200 ambazo ni takribani na bilioni 700-800 kwa leo ni karibu 1/3 ya Bajeti ya Trilioni 2.5, wanachelea kutoa mkopo bila udhamini wa JMT au Tanganyika
OMO aelewe wakopeshaji hawatoi zawadi wanaangalia pesa zao pia .
Nadhani Zitto na ACT wamshauri, kama ni kuongea awe na ''facts'' si leo anaongele moja la BoT kesho jingine.
Pia wamshauri aache chuki dhidi ya Watanganyika bali aelekeze malalamiko yake kwa Wazanzibar Wabunge JMT, wale kutoka BLW wanaokuja Dodoma na Wawakilishi katika baraza la mawaziri ambao leo wapo na CCM