Hali tete kwa Vladmir Putin, sasa ni dunia inataka kumtandika

Jipe moyo
 
Ulaya na UN iliyomuua Patrice Lumumba bila hatia ndio leo unasema inatafuta haki Ukraine?

Ulaya iliyoua ndugu zetu kwenye vita vya maji maji bila hatia,ulimewahi kudai hata waombwe radhi Acha fidia?,vipi mauaji ya halaiki ya Nama na Herero wa Namibia haikuumi,ila Ukraine inakuuma?
 

Mkuu,tatizo ni uelewa au tuseme elimu ndogo - lakini hao ndio wanaongoza katika nyanja za ubishi na matusi juu.

Mfano unafikiri ni Watanzania wangapi wanajua historia ya mauuaji ya halaiki ya makabila ya Herero na Nama huko Namibia,je,tuliwahi kusikia Serikali/Taifa la Kijerumani likiburuzwa kwenye Mahakama ya kimataifa kujibu mashataka ya kukihuka haki za binadamu au Ujerumani kulipa fidia kwa Serikali ya Namibia,hakuna!!

Je, Serikali ya Ubelijiji iliwahi hata siku moja kuwajibishwa kwa mauuaji ya Wakongomani wakati wa ukoloni au kulipa fidia Congo DRC kwa uporaji wa mali asili za taifa la Congo, hata huko Ulaya USA iliwahi kuvamia na kuua raia chungu mzima nchini Yugoslavia, kuharibu infrastructures karibu zote, kumkamata Rais na kumuua kwenye mazingira ya kutatanisha - sijawahi kusukia Merikani ukiwajibishwa kutokana na vitendo vyao vya war crime huko Yugoslavia sijawahi kusikia Bill Clinton wala Madelin Albright akiwajibishwa kwenye war crimes za huko Yugoslavia - badala yake Dunia inashinikizwa na akina Biden na genge lake kuitishia Urusi hasa Putin kwamba ashitakiwe for war Crimes conveniently avoiding to mention US past war crimes, cha ajabu kuna baadhi ya viongozi Duniani na raia wengine wanao unga mkono double standards za Wamerikani na wapambe wake,Wana ishupalia Urusi hasa Putin kutokana na msimamo wake thabiti dhidi ya siasa za kubeberu za kutaka kuitawala Dunia kinguvu.
 
Nashukuru umefanya kwa kirefu mkuu,mtu anae ilaani Urusi Hana akili hata kidogo,Na kwa wasiojua,leo Urusi ukishindwa hii vita,dunia ijiandae kwa kutawaliwa kimabavu,hata hawa wanaoitetea humu watalia
 
Putin ni mwehu kamili confirmed! Huwezi kuvamia nchi ya watu, kupora ardhi yao, wanapojitetea unapiga makombora ovyo ovyo makazi ya raia . Atakufa kifo cha aibu sana.
Mzee Putin alikurupuka tu, alidhani alichokifanya Crimea mwaka 2014 basi angeichukua Ukraine nzima kirahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…