2013 nilikuwa na carry ya Engineering Mathematics. Nilipoenda kufanya hiyo carry nikakuta IMEKAZA BALAA. Nikakusanya nikafanya maswali mawili(2) nikakusanya hata dakika 30 hazikuisha. Nikatoka hapo nikanyooka kwa lecturer nikamwambia haya ni maisha yangu mzee muajiri anasubiri cheti nipeleke. Kabla sijamaliza kuongea naye kumbe wezangu nao waliona moto kama niliouna, ghafla watu kama 30 wako nje ya ofisi ya lecturer hapo. Wote woga hakuna anayetaka kuingia kukazia hoja lecturer akaanza kuniambia njie hamsomi paper yenyewe rahisi hivo. Nikamwambia mzee naona sahizi una mambo mengi ngoja baadae jioni ntakuja nyumbani kwako nikuelezee vizuri, angalia matokeo yangu ya semester zingine nina A za Mathematics mfululizo.
Hapo hapo akasema kwa sauti kubwa ila siyo kali, "NINI UJE KWANGU, UNIARIBIA WANANGU". Akanyanyuka akaangalia huku na huku, akatoa karatasi ya A4 kwenye inkjet printer yake akanipa akaniambia andika jina lako na namba yako ya usajili na uwapatie wenzako. Nikamshukuru akabaki akicheka.
Nilipotoka hapo nikawa nawaza tuu, asipofanya mambo yule mzee hapo nikurudia mwaka mzima.
Yule mzee alikuwa ni msabato safi. Matokeo yalipotoka wote tulioandika majina yetu tulikuwa tumepita kwa neema.
Ndo maisha jamani, PAMBANENI.