Hali ya Chid Benz Inasikitisha sana


Hili neno naona umejifunza leo basi ndo limekuwa chorus.
 
Nataka kukumbusha tu kua wabongo wengi wanapitia hali ngumu hatujui kwasababu wao sio maarufu kama huyo Chid Benz. Street life ni gumu halafu kila mtu yuko busy na maisha yake na familia yake nobody cares about anybody else. Sasa hivi hata ukipoteza channel ya maisha familia, ndugu zako na watu wako wa karibu wanakuangalia tu hadi uugue ufe ili wakulilie na kukuzika fasta uwape gap la kusonga na maisha yao. Everybody is frustrated aseeh. Zamani familia hasa wazazi walikua karibu sana na watoto wao kiasi ambacho ni rahisi kupata msaada wa hali na mali, ushauri na counseling lakini sasa hivi watoto/ vijana wanalelewa na marafiki, wazazi wako busy kutafuta pesa ama unakuta hata hiyo familia haipo kabsa maana mtoto/ kijana analelewa na mzazi mmoja tu familia ishasambaratika (talaka). Inamana dogo akikutana na marafiki wazuri huko mtaani ni bora yake ila akikutana na marafiki wabaya anapotea mazima maana kumbuka hao ndo anashinda nao muda wote huko magetoni kwao so hata akipata changamoto yoyote itategemea watamshauri nini, wakimshauri upuuzi ndo hayo tunayoyaona kutopea kwenye uraibu wa madawa ya kulevya, ulevi na umalaya. Kwakifupi vijana siku hizi wanajilea wenyewe tu, nafasi ya wazazi na familia imekua ndogo sana na tunakoelekea ndo hatari zaidi maana ile bond kati ya mzazi na mtoto inazidi kupungua sana, I mean wazazi wanawakatia tamaa watoto wao mapema sana kwenye issue ya malezi. Nini kifanyike?! Kila mmoja akiwa mzazi ama mzazi mtarajiwa atafakari kwa kina nafasi yake kwa familia yake. Tuwemo!!
 
Amepona vipi na unaambia anakaa maskani na mateja..
 
Ndio usitoke kwenye mstari ukaungana na kampani za kishamba utarudishwa shamba ukiwa hujitambui
 
Ucjal mkuu mamb yatakaa sawa tu.
 
Pole yake.mama ajitathimini uongozi wake.kwa Nini kipindi hiki tu chake kumekuwa na wimbi kubwa la waathirika wa madawa ya kulevya ikiwemo chidibenz?mama thibiti madawa ya kulevya unatuharibia wasanii wetu
 
Huyu bwana ni example of poor life choices wakati wa mafanikio
 
Ukifanya tathimini utagundua madawa ya kulevya wayamewadhuru wasanii wengi sana.

Ngwair, langa, chiddy Benz, Ray C, O-ten,Mr.blue,Banza stone, majina mengine sijayakumbuka hapa ila ni wengi mno.
 
Kama kweli ni mteja, mtu pekee anayeweza kumsaidia Chidi Benz ni Chidi Benz.
 
Ukifanya tathimini utagundua madawa ya kulevya wayamewadhuru wasanii wengi sana.

Ngwair, langa, chiddy Benz, Ray C, O-ten,Mr.blue,Banza stone, majina mengine sijayakumbuka hapa ila ni wengi mno.
Sana mkuu wengi sana. Sijui huwa wanaingia kwa kujua au kuna watu huwa wanawategeshea then wanajikuta tayari washaingia maana wana mifano mingi ya wenzao waliopotezwa na hiki kitu.
 
Tumchangie pesa ya matibabu aende India. Mazombi rusheni pesa ya matibabu kwenye namba Ile Ile.
Linachomsumbua chiddy kwasasa ni depression sio uteja kama awali. Vita ya uteja ameshaishinda kwa kiwango kikubwa, kwa sasa anachohangaika nacho ni kukubaliana na hali kuwa yeye sie tena yule chiddy Benz aliyekuwa kwenye Peak level za kimataifa, kwasasa amechafua image yake jamii inamtazama kama teja au muathirika wa madawa.

Hiyo sio vita ndogo. Imagine kuwa katika hiyo aina ya depression halafu uwe hauna pesa na unaona wasanii kama akina diamond ambao juzi kati uliwaona wakiwa wanatembea kwa miguu kwenda studio hawana hata mia mfukoni leo wana mafanikio makubwa kukushinda na wamekupiga bonge la gepu.

Hiyo lazima imletee msongo wa mawazo na ndicho kinachomfanya awe busy na unywaji pombe usio na ratiba.
 
Wasanii wanaishi kisanii,wanasubiri wasikie kazima utaona watakavyomiminika msibani,wengine wakilia kwa uchungu utafikiri walikua hawajui aliyokua anapitia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…