Hali ya Chid Benz Inasikitisha sana

Kama amerudi kwenye unga, bas this time Gari limewaka kweli kweli
 
mguu kuendelea kuwa na vidonda means bado ni nyoka(mla unga).
Mguu kua na kidonda sio lazima ule unga, hata wewe hauli unga Ila unaweza ukachezewa tu nywele zako ziote km Mchicha mafungu mafungu hapa zinaota pale hazioti alafu watu waanze kukusema au ghafla unaanza kuota kiualaza cha Ben M watu wanaanza kujiuliza lile Afro lako imekuaje umepatwa na nini au ghafla tu unaanza kuota majipu sehemu nyeti majipu hayaishi na ukitumia hata Dawa gani majipu km unayaongeza tu kasi yaan hayaishi na hayasikii Dawa cha kufanya ni nini mrudie Mola wako piga Goti chini mengine ni majaribu ya Dunia tu na yanapita, wapi Fanani wa Hard Blasters kuna mtu anaemuongelea tofauti? Na alikua mraibu Chid hamfikii Ila sasa hivi nini kimetokea

Chid aachane na wale masela Mavi vidonda vyote atapona atapona ndani atapona nje Ila akikomaa nao soon watamtanguliza walianza na Mguu wakamtoboa sasa hivi anahangaika nao sasa akiendelea kukomaa nao wale masela Mavi anaowaona km masela wake wa utotoni na anawajua kabisa hawa ni masela Mavi soon watamuingiza SHIMONI masela Mavi hawafai si unaona wametoboa Mguu anahangaika nao Mguu chanzo ni masela Mavi
 
Chidi benzi ni sikio la kufa. Mnalaumu tu wasanii wenzake, Jamaa kwa hali aliyofikia hata apewe million 100 itaisha ndani ya mwezi kisha atarudia hali yake.
Now ni zaidi ya gunia la misumari hakuna anaeweza kulibeba
 
Si mlikua mnamsifia kwamba ni giniazi,tulitegemea giniaz ajue jinsi ya kujihandle na kujicontrol mmemjaza ujinga na kumpoteza kwenye ramani tena.
 
Dah!.... maisha yana mengi...ila huyu jamaa kama vile aliacha kabisa madawa hapo awali au karudia tena?
 

Addiction yoyote haifai, sababu end product ya addiction ni Depression. Depression na addiction ni mtu na mwanae. Depression inaanza kuja pale unapotakiwa kuiface reality, wakati akili yako ina dunia yake na sio hii ambayo mwili upo., hence addiction inakuwa ni a spider web, kujitoa ni ngumu kuliko ngamia kupita katika tundu la sindano.


Kwa sisi wakristo Biblia inatuagiza kwa habari ya kiasi, kwenye maisha ukifanikiwa kuiaminisha akili yako juu ya kiasi utaepuka matatizo mengi sana.
 
Tatizo la huyo kijana hana shukrani.

Watu kadhaa walishajitokeza kumsaidia ila mwisho wa siku anaishia kuwananga.

Diamond ,Babutale , walishajitokeza kumsaidia walichoambulia kusemwa vibaya

Haji Manara alishajitokeza kumsaidia alichoambulia kushushuliwa

Muacheni apambane na hali yake .
 
Hana shukrani huyo.

Manara ,Diamond hawana hamu naye.
 
Hasaidiki huyo na hana shukrani.
 
Aina ya maisha aliyochagua imempa hayo matokeo, na si hip-hop. Umaarufu umekuwa mzigo kwake, angalia life ya wasanii kama Nash Mc, Nikki Mbishi, wako simple na albums watoa kila mwaka.
Hao wamekubaliana na matokeo na hawategemei mziki kama chanzo chao kikuu cha kupata mkate.

Vingenevyo tungeongea stori nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…