Hali ya Chid Benz Inasikitisha sana

Hali ya Chid Benz Inasikitisha sana

Chidi ni rapa mkali sana ila mfumo wa nchi kwenye mziki wa hip hop haujampa mafanikio kulinganisha na alichotoa(uwezo wake) imepelekea kupata msongo wa mawazo na kutumbukia kwenye uraibu wa madawa ya kulevya.

Mtu mwingine anayekuja kwa sifa ni Young dee soon kitaumana.
Mkuu, kwani Chid mfumo haukumpa chochote kitu.? Alikitumiaje kidogo alichokipata.? Ni yeye tu mkali ambae mfumo haukumpa stahiki yake.?

Kwa sasa kuficha madhahifu ya Chid kwenye mfumo ni kutafuta kisingizio cha kuhalalisha makosa yake. Nchofikiri ni Chid akubali kuwa alifanya makosa na apambane kuyakabili. Pia abadili wa washauri.

Ukweli tunaoogopa kumwambia Chid ni kuwa mziki haumtaki kwa sasa kutokana na mambo kadhaa yanayoendelea kwenye industry. Anapaswa kuukubali huo ukweli na kubadili namna zake za maisha.

Kwanza akubali hawezi tena kuwa Chid yule na kuishi maisha ya ndotoni, atafute michongo mipya kabisa ya maisha itakayompa kipato huku akifanya mziki kama burudani tu.

Tunaogopaga sana kuwaambia wasanii wa zamani kuwa mziki wa sasa hauwataki wala kuwafaa. Mashabiki wa sasa hawaelewi chochote kilichowahi kuimbwa na kaka/baba zao. Na sisi ambao ni mashabiki wa mziki wa zamani tumeshapunguza vurugu za maisha kwa ukubwa na wingi wa mashabiki vijana. Hivyo wasanii wetu pendwa hatuwezi kuwapambania kwenye soko la digitali au analojia.
 
Addiction yoyote haifai, sababu end product ya addiction ni Depression. Depression na addiction ni mtu na mwanae. Depression inaanza kuja pale unapotakiwa kuiface reality, wakati akili yako ina dunia yake na sio hii ambayo mwili upo., hence addiction inakuwa ni a spider web, kujitoa ni ngumu kuliko ngamia kupita katika tundu la sindano.


Kwa sisi wakristo Biblia inatuagiza kwa habari ya kiasi, kwenye maisha ukifanikiwa kuiaminisha akili yako juu ya kiasi utaepuka matatizo mengi sana.
You such a Genius Binti,,###UziUfungwe###
 
Chunga wanao na masela Mavi sio watu wazuri

Katika vifo vilivyoniuma zaidi ni KIFO cha Pancho Latino wale Jamaa eti anazama wanamuona wanamuacha tu wanaanza kulialia na clip Video wanachukua Ile iliniuma kishenzi

Weka wanao mbali sana na masela Mavi
Pancho kilichomchukua ni nini?!
 
Sasa hisia ile ile ni kwenye alosto ya Unga na inakuwa ni mara 50 au zaidi.
Kama unaikumbua series ya Narcos, kuna afisa wa CIA alitoa kauli hii:

" Cocaine hijacks the pleasure centers in the brain. A rat will choose cocaine over food and water. It would choose cocaine over sleep, over sex over life itself".

Usijaribu hii kitu coz kutoka ni ngumu mno kwani mbadala wake ni ngumu kupatikana! Kaulize madaktari wa ubongo watakuambia kwa nini ni ngumu kutoka.

Mfano huo hapo juu kuhusu panya na cocaine kwenye maabara! Aliwekewa cocaine na hivyo vingine lakini bado akachagua cocaine!

Unaacha chakula, maji, mapenzi,usingizi na hata maisha yenyewe kisha unachagua cocaine!
 
Chidi ni rapa mkali sana ila mfumo wa nchi kwenye mziki wa hip hop haujampa mafanikio kulinganisha na alichotoa(uwezo wake) imepelekea kupata msongo wa mawazo na kutumbukia kwenye uraibu wa madawa ya kulevya.

Mtu mwingine anayekuja kwa sifa ni Young dee soon kitaumana.
Lame excuse
 
Pancho kilichomchukua ni nini?!
Walienda beach hapo Koko nahisi km sijakosea Kunduchi wakala mitungi sasa Jamaa 'Pancho Latino' akiwa amelewa akawaambia wenzie anataka akaogelee wakamzuia Ila akakomaa basi wakabidi waende kwenye maji Jamaa akaingia vizuri tu kaanza maji ya ugoko akaendelee mbele maji kiunoni akaendelee mbele maji ya SHINGO

Kumbuka hapo amelewa tungi basi vuaaaa mara hawamuoni wakaanza kupagawa Pancho yupo wapi Pancho yupo wapi wakapigwa bumbuwazi Pancho kazama ikabidi wapige kelele ndio wale Beach boys waje kutoa msaada

Beach boys wakazamia huku na huku huku na huku mara Pancho huyu hapa wakamuibua kwenye Maji Pancho hakua amekufa alipoibuliwa alikua kwenye Koma Ila ilibidi apatiwe huduma ya kwanza ya haraka angepona maana Mwili ulikua bado unapapatika wakiwa wamembeba wale beach boys na mapovu yanamtoka mdomoni na puani wakamweka chini kumkamua maji

Steps za kumkamua maji wakakosea wao walikua wanaminya tumbo lake wakati inabidi uminye kifuani na sio tumboni

Kumbe wakati huo maji yashaingia kwenye Mapafu kingine hawakumpuliza Mdomo kumuongezea Hewa kwenye Mapafu ili maji yaweze kutoka mdomoni na puani wala kumminya Pua ili kusudi Hewa ikijaa ndani maji yanamtoka mdomoni na puani wala hawakumpasha Joto Mwili wake maana Mwili unahitaji nguvu alikua kashalegea

Na ilibidi kuminya kifua chake ila wakambeba huku wanalialia kwamba Pancho ameshakufa lakini laiti wangejua pale walipomtoa kwenye Maji hakua amekufa alikua kwenye Koma nahisi ni tungi ndio zilizowazuzua mpaka wanafika hospital too late taarifa inakuja Pancho Latino is dead

Nimekusimulia kwa mujibu wa Clip waliyoirusha wao wenye waliokua nae kipindi cha umauti unamfika kule baharini

RIP Pancho Latino
 
Hali ya Msanii wa Hiphop Rashidi Makwilo (Chidibenz) inasikitisha sana sana, Siku za hivi karibuni amekua akiishi Msasani (Maandazi road) maskani moja na mateja, Kinachonisikitisha zaidi jamaa anaonekana hayuko sawa kiafya miguu imevimba, anaonekana aliumia na hajapona vizuri,miguu ameifunga bandage na anatembelea ndala, Nimemuona leo asubuhi nikiwa naelekea kazini atembea kwa msaada wa watu wanampa support (Nahisi alikuwa amelewa sana) Uso wake ni kama hauna matumaini

Nitoe wito kwa wasanii wenzake na Familia yake wamfuate pale msasani coz anaishi maskani na hana mtu wa kumuangalia, Sina uhakika ila kuna uwezekano labda amerudi tena kwenye wimbi la madawa ya kulevya

Kwa inavyoonekana ni kama wasanii wenzake wamemsusa, hawana time naye tena Lakini naona sio sahihi coz ni Msanii mwenzao inabidi wakubali kubeba hili jukumu la kumlinda na kumtunza Chidibenz, Juzi kwenye show ya Serengeti pale K/nyama viwanja vya posta, Chidibenz alipanda kwenye show ya Rosa ree lakini hakuchukua mda akashushwa, na alikua amevaa ndala, Wakiendelea Kumtenga hivi depression inaweza ikam-maliza kabisa, Kwa upande wa Familia yake sijui wao wamejipangaje coz inaumiza sana kumuona Ndugu au mtu wako wa karibu akiwa anapitia kipindi kigumu

Vijana tujitahidini sana kuishi kwa nidhamu, Ujana una mambo mengi bila yakua na nidhamu ni rahisi kuanguka
Unadhani amefika hapo alipo kwa bahati mbaya?
Amefanya juhudi kubwa sana na maombi juu kufika hapo alipo.
 
Kama mwenyewe hajionei huruma Nani mwengine wa kumuonea huruma labda mama yakemzazi
 
Waja si wanasema kuwa uyu jamaa ni jiniazi japo ameshawehuka lakin bado watu wanamchukulia kichwa haitaji msaada wa kisaikolojia. Ila uyu mwamba ni jeuri na mjuaji sana hapaswi kusaidiwa
 
Hakuna wa kumsaidia zaidi yake mwenyewe, hakuna kitu kigumu kutoka kama drugs na haijalishi tajiri au maskini, akichomoka madawa atakuwa na bahati sana, madawa yanakumaliza live huku ukijiona sawa tuu na huna tatizo lolote
 
Daah Kuna Ngoma yake naangalia muda huu kaimba na P unit kutoka Kenya jamaa Yuko Bling bling hatar na ana afya njema tu nikisoma huu Uzi nasononeka sana
 
Back
Top Bottom