Hali ya hewa ya Dodoma imenishinda

Hali ya hewa ya Dodoma imenishinda

Naona Dodoma inabadilika kwa kasi sana baada ya serikali kuhamia hapo, kigezo cha hali ya hewa kuwa mbaya sijui unaisemaje hali ya hewa ya Dar! Mimi joto la Dar sijawahi kulizoea licha ya kuishi huko miaka kadhaa. Nafikiri uamuzi wa kuhamia Dodoma ilikuwa ni kurahisisha nchi nzima kuzifikia huduma za serikali kwa ukaribu zaidi kwa maana ya kwamba Dodoma ni karibu karibia kwa kila mkoa uliopo Tz.
Kama uliliweza joto la Dar basi vumbi la Dom utalizoea tu pia.
 
Hiyo hali ya kupauka ngozi kunasababishwa na low humidity, hewa haina unyevu kama ilivyo kwa Dar. Inabidi watumie cream au lotion zinazoweka unyevu kwenye ngozi (moisturizing lotion/cream), na kutokana na hali ya baridi kuoga maji ya moto kwa muda mrefu (hot shower) hupelekea ngozi kupoteza maji, kwa hiyo kama unaoga maji ya moto jitahidi usijimwagie zaidi ya dk 5.....
Unavuta hewa kama unavuta misumari au viwembe puani
 
Nilishasema humu, hali ya hewa ya Singida ipo mild, wafanye extension ya kujenga makao makuu Singida.......lakini wademkaji wapo bize kupiga kampeni makao makuu kurudi Dar, kwa minajili ya kukuza miji yetu mtu mwenye akili timamu huwezi kushadadia makao makuu kurudi Dar....
Hakika mkuu na hata ikibaki hapo hapo ni sawa tu seikali iwekezepo tu mambo yatakaa sawa .mbona israel na uarabuni ni majangwa lakini wameweza kupatengeneza pakapendeza

Na mimi siungi mkono makao makuu kurudi dar.
 
Watu Wanatoka Tongotongo Kwenye Macho Mpaka Huruma YaaniHapa Bado!!🙄🙄😶😶😑😐😏😣
Samahani mkuu, hivi nini hasa husababisha tongotongo? chukulia macho ya Muhusika hayana shida yoyote.
 
Back
Top Bottom