DOKEZO Hali ya Kawe ni mbaya, Serikali ichukue hatua dhidi ya Mwamposa na waumini wake

DOKEZO Hali ya Kawe ni mbaya, Serikali ichukue hatua dhidi ya Mwamposa na waumini wake

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
kitanda usichokilalia huwezijua kunguni wake. Kifupi ni kuwa watu wana shida nyingi sana na zimekosa utatuzi kabisa.

mtu yupo tayari kufanya chochote ili mradi apate nafuu. Kuna siku nilikuwa mwanza , mkutano wa Mwamposa alitarajiwa kesho yake saa 10 jioni, lakini watu ( wateja wa maji na mafuta) walishaanza kujikusanya na kulala eneo la tukio-viwanja vya furahisha.

Na mkutano ukiisha huyu jamaa anakuwa wa kwanza kuondoka eneo la tukio tena kwa escort na kuwaacha wateja wake wakilala hapo uwanjani.

it is not fair
Akumbuke Yesu alilisha wafuasi wake
Yeye anashindwa vipi kuwapa huduma bora waumini (wateja)wake
Uko sahihi kwa asilimia 100
 
Afrika na upumbavu haviwezi kutofautishwa.
image_downloader_1667297212984.jpg
image_downloader_1666966539825.jpg
JamiiForums1404360063.jpg
FB_IMG_16604753657782156.jpg
 
Hivi unaboreshaje sehemu ambayo sio kwako umepanga maana mwamposa pale amepanga suala la kupaboresha Ni la anayechukua Kodi yaani serikali
Mhhh basi uwanja ni sehemu ya ibada na sio sehemu ya kulala, sidhani kama kipindi alipokuwa anakodisha alisema waumini watakuwa wanalala. Still mwamposa kuna sehemu hayupo sawa!
 
Sema walioleta "hii" dini ya Ukristo na sio walioleta "hizi" dini, kwani hapo kwa Mwamposa (Mwam- PESA) kuna dini ngapi??.
Dhamira ilikuwa kufikisha fikra zangu ambazo nina yakini ni huru. Niliposema hizi dini nilimaanisha zote ambazo kwa mtazamo wangu bila kuzitaja naamini ni kajanja.

Kabla kusahihisha ilipaswa ujue chimbuko la maoni yangu.

Uwe na siku njema. Ramadhan Karim kama muislam na kwa resma njema kama ni mkristo✌️
 
Nawasalimu wote kwa jina la Upendo. Amani, baraka na neema za Mwenyezi Mungu ziwe pamoja nanyi.

Kwa wakristu, hongereni kwa kuingia nusu ya pili ya mfungo wenu. Pia, nawatakia ndugu zangu waislam mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, mwenyezi Mungu awakirimie Neema na azipokee sala na funga zenu.

Pasipo kuathiri imani na ibada yao kwa Mungu, nataka nitoe maoni yangu kuhusu uzembe uliopo Tanganyika Packers, kwa waumini wanaosali kwa Mtume Mwamposa.

Binafsi, sina shida yoyote na kusali kwao. Isipokuwa, kumekuwepo na tabia ya watu hawa kulala chini, kwenye uwanja wa wazi usiku kucha wakisubiri huduma hii.

Jumatatu moja Mwaka jana mwezi wa 7 wakati naanza kazi kwenye taasisi moja iliyo karibu na maeneo haya, nilishangaa kuona kusanyiko kubwa la watu waliolala chini ambao kwa hesabu ya haraka hawakuwa pungufu ya 500.

Katika kundi hilo, idadi kubwa ya watu walikuwepo ni wazee, wajawazito na wanawake wenye watoto wachanga sana. Hali hii haikuishia siku hiyo, imekuwepo hadi sasa.

View attachment 2562265
Sehemu ndogo ya makundi ya watu waliolala hapo usiku wa kuamkia leo Machi 23, 2023
Mtu yeyote mwenye akili timamu hahitaji elimu ya sayari ya 5 kuona kuwa mazingira haya ni hatari kwa afya ya wahusika.

Kwa kuwa mimi ni mtu mwenye elimu ya fani fulani ya afya, inayohusika na kushughulikia wagonjwa moja kwa moja, huwa nawaza sana kila ninapoona watu hawa asubuhi. Fikiria hali ya sasa ya mvua, kisha mtazame mzee, au mwanamke mjamzito, mama mwenye mtoto mchanga au mgonjwa wa kisukari, presha au kifafa anayelala hapo usiku kucha kwa siku kadhaa akisubiria huduma.

Kibaya zaidi, sehemu za kujisaidia na kupata huduma muhimu za kibinadamu hazitoshi. Mathalani, ukipita hapo asubuhi utakuta watu wanapiga mswaki hadharani na kutema uchafu barabarani, au hata sehemu ileile ambayo huitumia kulala wakati wa usiku.

Baridi kali na vumbi ni chanzo cha magonjwa mengi hasa kwa watoto na wazee. Badala ya kupata huduma za kiroho, watu hawa wanaweza kuondoka hapo wakiwa na mzigo wa magonjwa mengine makubwa zaidi.

Naomba Serikali itazame suala hili kwa umakini. Kama imeshindwa kabisa kuweka utaratibu mzuri wa kumbana Mwamposa kwa kuwa yeye ndiye kiongozi, basi miundombinu ya eneo hili iboreshwe.

Kuacha hali hii iendelee ikiwa hivi itasababisha maafa makubwa. Uponyaji wa kiroho unapaswa kwenda pamoja na uponyaji wa kimwili.

Naomba kutoa hoja!
Bubu wa roliyondo na kikombe cha uongo
 
Kwani hicho kiwanja anakimiliki yeye? Kiwanja cha ile hotel ya Mbeya anakimiliki
kwani hostel hazijengeki katika kiwanja kingine chochote tofauti na hapo wanapofanyia ibada? Kama aliweza kumiliki kiwanja cha mbeya nini kinamzuia kumiliki kiwanja Dar es salaam?
 
Dah, Mwamposa noma sana, ni mwendo wa kujipigia hela tu
Wakiristo wengi uwezo wa kutumia akili zao uwa ni mdogo sana hasa katika mambo ya imani mfano kwa babu roliyondo kwa zamaladi mwanza wapo baadhi wanao dhani anaenda mbinguni jushua alivunja rekodi Kakobe kibwetele wa uganda hacha waliwe si akili zao ndogo
 
Hiyo ndo inasemwa kuwa ".......kwa kukosa maarifa".

Hana sehemu rasmi ya kufanyia hiyo biashara yake ya kukusanya pesa za wenye matatizo. Anajijengea Hotel, kwamba anajiandaa kidunia zaidi na si kiimani sio?

Huyo aliyemruhusu aendelee kutumia TP pale naye achunguzwe.
Viongozi wa makanisa yote duniani hawako kiroho bali wako kibiashara zaidi
 
kwani hostel hazijengeki katika kiwanja kingine chochote tofauti na hapo wanapofanyia ibada? Kama aliweza kumiliki kiwanja cha mbeya nini kinamzuia kumiliki kiwanja Dar es salaam?
Unadhani kupata kiwanja cha kujenga hotel Kawe ni rahisi kama Mbalizi?
 
Wakiristo wengi uwezo wa kutumia akili zao uwa ni mdogo sana hasa katika mambo ya imani mfano kwa babu roliyondo kwa zamaladi mwanza wapo baadhi wanao dhani anaenda mbinguni jushua alivunja rekodi Kakobe kibwetele wa uganda hacha waliwe si akili zao ndogo
Acha limwamposa liendelee kujipigia pesa mpaka akili zitapowakaa sawa.
 
Back
Top Bottom