Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Iko na njemba pale imepeleka tezi dume ikabewe na mwamposa hahahhaDah, Mwamposa noma sana, ni mwendo wa kujipigia hela tu
Lile eneo ni la serikali,sidhani kama anashindwa kupafanyia marekebisho,nahisi amepanga...Mwamposa ni mfanyabiashara mzuri sana ila amekosa elimu ya kuboresha sehemu yake ya biashara
Kuna jamaa aliandika "Pastor akihitaji gari, anawaambia waumini wachange, waumini wakiugua hoi wanakosa fedha ya matibabu Pastor anawaambia pray"Ila Mwamposa anazingua. Kuliko kujenga hotel Mbeya kwanini asingeanza kujenga hostels kwa ajili ya waumini wake kwanza.
Dah noma sanaa.Iko na njemba pale imepeleka tezi dume ikabewe na mwamposa hahahha
Ni miaka kadhaa sasa huduma hii inaendelea hapo, sijapata kusikia hata magonjwa ya mlipuko, why?Nawasalimu wote kwa jina la Upendo. Amani, baraka na neema za Mwenyezi Mungu ziwe pamoja nanyi.
Kwa wakristu, hongereni kwa kuingia nusu ya pili ya mfungo wenu. Pia, nawatakia ndugu zangu waislam mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, mwenyezi Mungu awakirimie Neema na azipokee sala na funga zenu.
Pasipo kuathiri imani na ibada yao kwa Mungu, nataka nitoe maoni yangu kuhusu uzembe uliopo Tanganyika Packers, kwa waumini wanaosali kwa Mtume Mwamposa.
Binafsi, sina shida yoyote na kusali kwao. Isipokuwa, kumekuwepo na tabia ya watu hawa kulala chini, kwenye uwanja wa wazi usiku kucha wakisubiri huduma hii.
Jumatatu moja Mwaka jana mwezi wa 7 wakati naanza kazi kwenye taasisi moja iliyo karibu na maeneo haya, nilishangaa kuona kusanyiko kubwa la watu waliolala chini ambao kwa hesabu ya haraka hawakuwa pungufu ya 500.
Katika kundi hilo, idadi kubwa ya watu walikuwepo ni wazee, wajawazito na wanawake wenye watoto wachanga sana. Hali hii haikuishia siku hiyo, imekuwepo hadi sasa.
View attachment 2562265Mtu yeyote mwenye akili timamu hahitaji elimu ya sayari ya 5 kuona kuwa mazingira haya ni hatari kwa afya ya wahusika.
Sehemu ndogo ya makundi ya watu waliolala hapo usiku wa kuamkia leo Machi 23, 2023
Kwa kuwa mimi ni mtu mwenye elimu ya fani fulani ya afya, inayohusika na kushughulikia wagonjwa moja kwa moja, huwa nawaza sana kila ninapoona watu hawa asubuhi. Fikiria hali ya sasa ya mvua, kisha mtazame mzee, au mwanamke mjamzito, mama mwenye mtoto mchanga au mgonjwa wa kisukari, presha au kifafa anayelala hapo usiku kucha kwa siku kadhaa akisubiria huduma.
Kibaya zaidi, sehemu za kujisaidia na kupata huduma muhimu za kibinadamu hazitoshi. Mathalani, ukipita hapo asubuhi utakuta watu wanapiga mswaki hadharani na kutema uchafu barabarani, au hata sehemu ileile ambayo huitumia kulala wakati wa usiku.
Baridi kali na vumbi ni chanzo cha magonjwa mengi hasa kwa watoto na wazee. Badala ya kupata huduma za kiroho, watu hawa wanaweza kuondoka hapo wakiwa na mzigo wa magonjwa mengine makubwa zaidi.
Naomba Serikali itazame suala hili kwa umakini. Kama imeshindwa kabisa kuweka utaratibu mzuri wa kumbana Mwamposa kwa kuwa yeye ndiye kiongozi, basi miundombinu ya eneo hili iboreshwe.
Kuacha hali hii iendelee ikiwa hivi itasababisha maafa makubwa. Uponyaji wa kiroho unapaswa kwenda pamoja na uponyaji wa kimwili.
Naomba kutoa hoja!
umeongea ukweli mtupu.. makanisa mengi ya Tanzania haya ubora wa huduma sio kimwili sio kiroho, mambo ni vurugu varaga as long as wanaingiza sadaka kwao hawajali watu wanaowapa sadaka hizoNawasalimu wote kwa jina la Upendo. Amani, baraka na neema za Mwenyezi Mungu ziwe pamoja nanyi.
Kwa wakristu, hongereni kwa kuingia nusu ya pili ya mfungo wenu. Pia, nawatakia ndugu zangu waislam mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, mwenyezi Mungu awakirimie Neema na azipokee sala na funga zenu.
Pasipo kuathiri imani na ibada yao kwa Mungu, nataka nitoe maoni yangu kuhusu uzembe uliopo Tanganyika Packers, kwa waumini wanaosali kwa Mtume Mwamposa.
Binafsi, sina shida yoyote na kusali kwao. Isipokuwa, kumekuwepo na tabia ya watu hawa kulala chini, kwenye uwanja wa wazi usiku kucha wakisubiri huduma hii.
Jumatatu moja Mwaka jana mwezi wa 7 wakati naanza kazi kwenye taasisi moja iliyo karibu na maeneo haya, nilishangaa kuona kusanyiko kubwa la watu waliolala chini ambao kwa hesabu ya haraka hawakuwa pungufu ya 500.
Katika kundi hilo, idadi kubwa ya watu walikuwepo ni wazee, wajawazito na wanawake wenye watoto wachanga sana. Hali hii haikuishia siku hiyo, imekuwepo hadi sasa.
View attachment 2562265Mtu yeyote mwenye akili timamu hahitaji elimu ya sayari ya 5 kuona kuwa mazingira haya ni hatari kwa afya ya wahusika.
Sehemu ndogo ya makundi ya watu waliolala hapo usiku wa kuamkia leo Machi 23, 2023
Kwa kuwa mimi ni mtu mwenye elimu ya fani fulani ya afya, inayohusika na kushughulikia wagonjwa moja kwa moja, huwa nawaza sana kila ninapoona watu hawa asubuhi. Fikiria hali ya sasa ya mvua, kisha mtazame mzee, au mwanamke mjamzito, mama mwenye mtoto mchanga au mgonjwa wa kisukari, presha au kifafa anayelala hapo usiku kucha kwa siku kadhaa akisubiria huduma.
Kibaya zaidi, sehemu za kujisaidia na kupata huduma muhimu za kibinadamu hazitoshi. Mathalani, ukipita hapo asubuhi utakuta watu wanapiga mswaki hadharani na kutema uchafu barabarani, au hata sehemu ileile ambayo huitumia kulala wakati wa usiku.
Baridi kali na vumbi ni chanzo cha magonjwa mengi hasa kwa watoto na wazee. Badala ya kupata huduma za kiroho, watu hawa wanaweza kuondoka hapo wakiwa na mzigo wa magonjwa mengine makubwa zaidi.
Naomba Serikali itazame suala hili kwa umakini. Kama imeshindwa kabisa kuweka utaratibu mzuri wa kumbana Mwamposa kwa kuwa yeye ndiye kiongozi, basi miundombinu ya eneo hili iboreshwe.
Kuacha hali hii iendelee ikiwa hivi itasababisha maafa makubwa. Uponyaji wa kiroho unapaswa kwenda pamoja na uponyaji wa kimwili.
Naomba kutoa hoja!
Wengi wanaokwenda hapo kwa mwamposa kichwani hawako sawaNimecheka kaa fala [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
😆🤣😆🤣Inabidi ajifunze kuthamini malighafi yake (waumini) ili kuendelea kuvuna zaidi (sadaka).
Wanatafuta waumeNje ya Mada: Tuendelee kuwaombea Wanawake, ukiangalia hapo takwimu za haraka ni kuwa 3/4 ya hao waumini ni Akina Mama. Vivyo hivyo wanaoenda kwa Waganga 3/4 ni Wanawake pia.
Seems Wanawake wana shida nyingi kuliko Akina Baba au ikoje hii?
Hivi hii kitu ni kweli mkuuu au inakuwaga story tu za vijiweni 🤔
Nunua maji kwa mangi naja lipa"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa". Ni heri upungukiwe na pesa kuliko upungukiwe na akili.
Pesa zimeenda kujenga hotel mbeya. Acha waibiwe mi hata siwaonei huruma na watazidi kuwa masikiniKwan kuweka mahema kunahitaji pesa kias gan
Hata wakikojolea sisi hatujali maji yetu mwaposa wetu mbele kwa mbele nyuma mwikoActually wajukuu zetu wanakua imara kwasababu wazazi wao watateseka sana
Jamii yetu ya sasa itazaa wajukuu wenye hasira sana na sisi
Watatuchukia na kukojolea makaburi yetu