DOKEZO Hali ya Kawe ni mbaya, Serikali ichukue hatua dhidi ya Mwamposa na waumini wake

DOKEZO Hali ya Kawe ni mbaya, Serikali ichukue hatua dhidi ya Mwamposa na waumini wake

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
N ngumu sana kwa serikali inayoongozwa na chama cha siasa kuwachukulia hatua watu kama hawa walio shikilia imani za watu zaid ya milioni , kwenye uchanguzi ni hatari sna kukosa kura zaid ya milion moja , kisa tu maamuzi yasiyo athiri nafasi yako kwenye serikali.
 
Huu ujumbe umfikie Mwamposa asifurahie tu kuchukua pesa zao aangalie pia jinsi ya kuwawekea watu wake mazingira mazuri Ili kuboresha huduma zake, awajengee mahema ya kufikia watokao mbali aweke huduma za afya vyoo vya kutosha hata vile mobile washroom vikijaa vinatolewa. Awahakikishie jukumu la usalama, afya, huduma ya maji, nk.
Kama anayo pesa ya kujenga hoteli na viwanda hawezi shindwa boresha mazingira ya wafuasi wake.
 
kitanda usichokilalia huwezijua kunguni wake. Kifupi ni kuwa watu wana shida nyingi sana na zimekosa utatuzi kabisa.

Mtu yupo tayari kufanya chochote ili mradi apate nafuu. Kuna siku nilikuwa mwanza , mkutano wa Mwamposa alitarajiwa kesho yake saa 10 jioni, lakini watu ( wateja wa maji na mafuta) walishaanza kujikusanya na kulala eneo la tukio-viwanja vya furahisha.

Na mkutano ukiisha huyu jamaa anakuwa wa kwanza kuondoka eneo la tukio tena kwa escort na kuwaacha wateja wake wakilala hapo uwanjani.

It is not fair.
Akumbuke Yesu alilisha wafuasi wake.
Yeye anashindwa vipi kuwapa huduma bora waumini (wateja)wake.
Shida na matatizo mengi ya watu ni matokeo ya wengi kukaa mbali na maarifa, maarifa yanapatikana kupitia kujifunza mafundisho, au masomo mbalimbali ambayo kwa ulimwengu wa SAsa internet imekuletea elimu nyumbani.

Unapokosa maarifa ni lazima utawatajirisha waganga, mitume na manabii, wanasaikolojia nk. Ukipata maarifa unakuwa huru dhidi ya magonjwa yote ya kiroho na kimwili.

Kama wajinga wakitoweka duniani waganga, mitume na manabii, wanasaikolojia, wanasiasa, watakosa kazi ya kufanya watakufa njaa na maisha ni kutegemeana.
 
Unadhani kupata kiwanja cha kujenga hotel Kawe ni rahisi kama Mbalizi?
HOSTEL sio HOTEL.

Kwani bila ya kuhubiri Kawe mahubiri yake hayafanyiki? Hata akienda Chanika wanaomuamini watamfuata tu, ikiwa watu wanatoka Kigoma kuja hapo Kawe.

Jamaa yangu hebu acha ubishi kwa hoja nyepesi basi ili mradi tu uonekane unabisha.
 
HOSTEL sio HOTEL.

Kwani bila ya kuhubiri Kawe mahubiri yake hayafanyiki? Hata akienda Chanika wanaomuamini watamfuata tu, ikiwa watu wanatoka Kigoma kuja hapo Kawe.

Jamaa yangu hebu acha ubishi kwa hoja nyepesi basi ili mradi tu uonekane unabisha.
Na mimi nazungumzia kiwanja, bila kujali itajengwa Hotel au Hostel. Kupata kiwanja Kawe cha ukubwa ule si rahisi kama kupata kiwanja cha hivyo Mbalizi
 
Mimi nitakua nahesabu sadaka na kufanya sorting. Nimewahi tayari. Mchungaji ni Bujibuji Simba Nyamaume
Tukiacha utani, makanisa yamekuwa mradi mkubwa sana. Kuna jamaa namjua kabisa kuwa ni muislamu pure na familia yake yote waislam.

Baada ya kumaliza chuo alihangaika kupata kazi akaishia kufanya volunteering kwenye NGO ya wa missionary. Kupitia huko alipata connection na wahubiri wakubwa akaishia kufungua kanisa dogo tu maeneo ya Tabata (sitolitaja jina nisije kumuharibia).

Kupitia ujanja ujanja wa kuweza kupiga makelele ya kuongea na kukariri mistari michache ya biblia pamoja na kualika wahubiri wakizungu aliokutana nao alipokuwa volunteer, leo hii kanisa ni kubwa mno na jamaa ana pesa ya kutosha.

Point hapa sio ukubwa wa kanisa na pesa yake bali imani ya jamaa. Mpaka leo anaswali kama muislam akiwa mwenyewe na kwa watu wake wa karibu anajulikana ni muislam lakini kanisani kwake ni mtumishi wa Mungu na pesa ya kutosha ya sadaka anakula.

Kwa kifupi hizi imani zimekuwa miradi kwa sasa.
 
Na mimi nazungumzia kiwanja, bila kujali itajengwa Hotel au Hostel. Kupata kiwanja Kawe cha ukubwa ule si rahisi kama kupata kiwanja cha hivyo Mbalizi
We kiumbe kwani hawezi kuhubiri kwingine sharti iwe Kawe?
 
Ngoja ni mtag mwanangu GENTAMYCINE
Ila kwa kujazia tu hapo,hapo kwake kuna mental case nyingi sana

Ova

Yaani watu wanamatumaini mwamposa atatatua shida na dhiki zao kabisa, nimeona na waislamu wana wajinga wao wanaotegemea daawa na visomo kutatua shida zao kama magonjwa na eti yuko nairobi anatuma hela kwa sheikh wa tandika, afanye kisomo tandika halafu kikafanye kazi kenya ninaangalia tu nakucheka
 
we kiumbe kwani hawezi kuhubiri kwingine sharti iwe Kawe?
Hivi unadhani kwa nini pamoja na kukumbwa na mafuriko, watu waliopo kando ya bonde pale Jangwani hawataki kuhama? Sababu ni hiyo hiyo. Mwamposa atacheza Kawe, Mwenge, Makumbusho na maeneo ya karibu na hapo. Kuna suala la wateja na wateja muhimu. Chanika hatapata wateja muhimu
 
Waumini wake wengi hawewezi kulipia hotel, labda gesti za elfu saba.
Ila Mwamposa anazingua. Kuliko kujenga hotel Mbeya kwanini asingeanza kujenga hostels kwa ajili ya waumini wake kwanza.

Naamini angefanya hivyo angevuna pesa zaidi za kuweza kujenga mahoteli mengi zaidi.

Inabidi ajifunze kuthamini malighafi yake (waumini) ili kuendelea kuvuna zaidi (sadaka).

 
Sasa ndio nimejua chimbuko la maoni yako kwamba; "Samaki mmoja akioza pezi basi wote watakuwa wameoza".
Kwani kwenye uislamu hakuna huu ushaitwani!!? Kuna watu wanaua wenzao eti kisa uende peponi kurithi mabikira 72,ni moja ya ujinga wa hizi dini!!
 
Back
Top Bottom