DOKEZO Hali ya Kawe ni mbaya, Serikali ichukue hatua dhidi ya Mwamposa na waumini wake

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Hajaamua tu. Kwa alipofika sasa hata akienda mmbade watu watamfuata. Kwa sasa keshavuka kiwango cha kulenga eneo. Sasa hivi linauza jina lake.

Unless masharti ya uhubiri wake ni kuwa lazima iwe maeneo hayo.
 
Ushauri mzuri sana na wenye kujali afya ya jamii. Kama utaweza peleka ujumbe wako serikali za mitaa kuanzia Manispaa ya Kinondoni, Kata na hadi serikali ya mtaa inapofanyika ibada.

Mwamposa naye aelewe kuwa afya njema pia hupatikana katika mazingira safi ambayo ni kinga ya magonjwa mengi.
 
Mwamposa analipa Kodi kubwa saaaaana . Pia ana finance mafuta ya viongozi. So Kwa sasa aachwe Kwanza amalize kuchukua pesa za hao wanaolala nje ilihali Wana makwao
 
Hao ni homeless hata ulaya wapo na kuna baridi kinyama
 
Mwamposa anatreat waumini wake kama ng’ombe wasio na banda ni kuwakamua maziwa yaishe yote hadi chuchu zitoke damu.

Makanisa kama haya ndiyo yanatakiwa yafungiwe mpaka muhusika aweke mazingira bora ya kuwapuna hao wateja wake.
 
Duuh..mbona hatari hii..
 
Baridi kali na vumbi ni chanzo cha magonjwa mengi hasa kwa watoto na wazee. Badala ya kupata huduma za kiroho, watu hawa wanaweza kuondoka hapo wakiwa na mzigo wa magonjwa mengine makubwa zaidi
si wataponywa? You are contradicting yourself! hawawezi kupatwa na magonjwa kwa vile wako eneo la uponyaji
 
Hivi karibuni nilikuwa mkoa mmojawapo wa kusini, nikaambiwa Muislam flani anaendaga kusali kwenye kanisa la Mwamposa nilipinga sana hadi niliposhuhudia kwa macho yangu.

Huyo Muislam yuko radhi mpigane lakini si kumponda Mwamposa, ndipo nilipojua kumbe Mwamposa ana wateja mpaka Waislamu.

Imani ni Mtu binafsi na matendo mema wala si dini wala dhehebu lolote.
 
Nje ya Mada: Tuendelee kuwaombea Wanawake, ukiangalia hapo takwimu za haraka ni kuwa 3/4 ya hao waumini ni Akina Mama. Vivyo hivyo wanaoenda kwa Waganga 3/4 ni Wanawake pia.

Seems Wanawake wana shida nyingi kuliko Akina Baba au ikoje hii?
 
Changamoto; hizi nguvu huwa ni za msimu ndio maana hawawekezi kwenye ujenzi wa makanisa, na hatimaye kukimbilia kuwekeza sehemu nyingine itakayompatia ulaji pale nguvu zitakapo potea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…