DOKEZO Hali ya Kawe ni mbaya, Serikali ichukue hatua dhidi ya Mwamposa na waumini wake

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Umepiga picha kwa kuchungulia kiwiziwii sana kupitia senyenge...ulikua unaogopa kumwagiwa chumvi wa upako machoni na kisim chako cha mchina
 
Kama majitu yamerogwa yanalala chini huku yakisubiria kukanyaga mawese wewe inakuuma nini? acha wajinga waangamie kwa kukosa maarifa lile jibwa lenyewe linajenga mahoteli tu, wale nin wakuonea huruma tu na kuwaaacha maana wameamua wenyewe kurogwa
 
Ila Mwamposa anazingua. Kuliko kujenga hotel Mbeya kwanini asingeanza kujenga hostels kwa ajili ya waumini wake kwanza.
Kuna jamaa aliandika "Pastor akihitaji gari, anawaambia waumini wachange, waumini wakiugua hoi wanakosa fedha ya matibabu Pastor anawaambia pray"
 
Ni miaka kadhaa sasa huduma hii inaendelea hapo, sijapata kusikia hata magonjwa ya mlipuko, why?

Ukiongelea upepo mkali na baridi kali kama chanzo cha magonjwa basi kwa Dar es Salaam utakuwa inasema uongo kwani hali kama hiyo no nadra sana. Huku sio Mbeya wala moshi, kumbuka hilo ili uandike uhalisia.

Nijuavyo mimi hakuna mtu anaruhusiwa kulala kwenye eneo la Kanisa ndio maana hicho kikundi unachokisema (nimepita mara nyingi tu hawafiki hata 200) kinaweka kambi karibu na kituo cha daladala mbali na eneo la Kanisa.

Ikumbukwe kwamba sio jukumu la makanisa kujenga hosteli za kufikia waumini labda kama kuna huduma zinazohitaji waumini waweke kambi. Mwamposa huendesha ibada zake kwa siku na Waumini kurejea makwao. Hivyo basi mimi wajibu wa kila muumini anayekuja kuhudhuria ibada (hasa wanaotoka mikoani) kuhakikisha kwamba wanazo sehemu za uhakika za kufikia ili kupata malazi katika kipindi chote watakachokuwapo mahali hapo.

Ikumbukwe kuwa mambo ya kiimani huhesabiwa kuwa ni UPUMBAVU kwa wenye elimu kama yako, maandiko yanasema hivyo. Sasa Mungu ameyachagua mambo hayo yanayodharauliwa ili kuwaaibisha wakubwa na wenye nguvu, wasomi, nk!!

1 Wakorintho 1 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁷ bali Mungu aliyachagua mambo mapumbavu ya dunia awaaibishe wenye hekima; tena Mungu alivichagua vitu dhaifu vya dunia ili aviaibishe vyenye nguvu;
²⁸ tena Mungu alivichagua vitu vinyonge vya dunia na vilivyodharauliwa, naam, vitu ambavyo haviko, ili avibatilishe vile vilivyoko;
²⁹ mwenye mwili awaye yote asije akajisifu mbele za Mungu.
 
"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa". Ni heri upungukiwe na pesa kuliko upungukiwe na akili.
 
umeongea ukweli mtupu.. makanisa mengi ya Tanzania haya ubora wa huduma sio kimwili sio kiroho, mambo ni vurugu varaga as long as wanaingiza sadaka kwao hawajali watu wanaowapa sadaka hizo
 
Acha kondoo waendelee kumnufaisha mchungaji..
 
Mbona kila siku wanatangaziwa kwamba hapo sio mahali pa kulaa,watu wamekuja na shida zao hawana ndugu na hawana mahali pa kufikia wameamua kulala hapo unafanyaje?
 
Actually wajukuu zetu wanakua imara kwasababu wazazi wao watateseka sana

Jamii yetu ya sasa itazaa wajukuu wenye hasira sana na sisi

Watatuchukia na kukojolea makaburi yetu
Hata wakikojolea sisi hatujali maji yetu mwaposa wetu mbele kwa mbele nyuma mwiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…