Poker
JF-Expert Member
- Oct 7, 2016
- 5,445
- 14,828
Hili jiji la arusha ambalo linasifika kwa utalii na ambalo lina historia nzuri ya kutoa wasanii, waigizaji na watangazaji maarufu, sifa zake kwa nje ni nyingi na nzuri sana. Ila kwa uhalisia ukifika ndani ya jiji hilo ni shida tupu.
Biashara ndani ya jiji hilo ni ngumu sana, watu wanafanya biashara kwa kujuana sana. Kiufupi mzunguko ni mdogo sana si soko la kilombero wala soko kuu.
Ukipita mitaa ya makao mapya utakuta nyumba self contained ya vyumba 3 shs 150,000/= na wanataka kodi ya hata mwezi. Ukienda huko ngarenaro mitaa ya shauri moyo unakuta wali wa kuku 1000.
Mbaya zaidi hili jiji mitaa mingi ni michafu sana kama sekei, sombetini, mbauda na huko mianzini. Biashara kubwa katika hili jiji ni biashara ya shule, biashara ya nyama aina zote na biashara ya bia.
Japo wanachuga hupenda kulitetea hili jiji, ila kiuhalia arusha ilipaswa kuwa mji kama miji mingine. Yaani saivi hata kahama kuna mzunguko wa hela kuliko arusha.
Hili ndio jiji ambalo matajiri wake wote hawapo top 100 ya matajiri Tanzania.
Hili pia ndio jiji linaloongoza kwa kuvaa mitumba wazee wa krokon na memorio.
Hili ndio jiji ambalo wakazi wake wengi ni lialia wakija kwenye biashara yako watataka uwapunguzie hata kitu cha mia.
Hili ndilo jiji ambalo ukikaa mwaka mmoja unaweza wafahamu wakazi wote wa hapo. Hapo utapata picha udogo wa jiji.
Imagine jiji uwanja wa ndege hauna taa za kuongozea ndege usiku.