Hali ya mabasi ya Mwendokasi Mbezi Mwisho ni kero tupu kama kawaida leo Novemba 15, 2023

Hali ya mabasi ya Mwendokasi Mbezi Mwisho ni kero tupu kama kawaida leo Novemba 15, 2023

Mvua ipo.. Tabata inanyesha sahivi.

Alafu kwani ni lazima mpande mwendokasi? Zamani mlikuwa mnaendaje huko ktk mizunguko yenu?
Mbezi - posta/kariakoo hakuna usafiri zaidi ya mwendokasi, daladala ziliondolewa.
 
Ulivyoanza mradi wa mwendokasi, bus zote za kwenda mjini zikazuiliwa
Nyie mnavyosema mjini mnamaanisha Kkoo ndio mnaita mjini ? Makumbusho je..? Mwenge? Sio mjini ryt?

Ni hivi. Kama unaenda katikati ya mji kuna means zingine za usafiri ikiwemo Bajaji. Kama huwez ku afford 2k basi unganisha gari mpk Mwenge pale zipo za kwenda katikati ya mji. Au uende mpk Makumbusho zipo gari kule.

Sasa fikiria kuna mtu kaaa hapo kuanzia saa 12 et anasubiri Basi la Mwendokasi na mwingine na akili zake timamu anaona hiyo foleni bado anaenda kukata ticket.
 
Kituo cha Mabasi ya Mwendokasi Mbezi Mwisho hali ni mbaya, abiria tupo wengi lakini mabasi hakuna, kuna watu wako hapa tangu Saa 12:10 Asubuhi (leo Novemba 15, 2023) lakini hakuna msaada wowote.

Hivi viongozi wetu wanaishi wapi mpaka hawaoni hii kero? Kila siku ni kilio cha Mwendokasi tu.

Hapa watu wameshakata tiketi, wengine wana hela za ngama, basi linakuja moja kisha lingine linakuja baada ya dakika 40 au zaidi.

Hakuna mvua kama ilivyosemwa na watabiri, labda ingetumika kama kisingizio, mamlaka zinatakiwa kuwajibika na ikiwezekana viongozi wanaosimamia usafiri huu wawajibishwe au wawajibike wao wenyewe, hii ni zaidi ya kero na shughuli nyingi za uchumi zimesimama.
Request Uber
 
Nyie mnavyosema mjini mnamaanisha Kkoo ndio mnaita mjini ? Makumbusho je..? Mwenge? Sio mjini ryt?

Ni hivi. Kama unaenda katikati ya mji kuna means zingine za usafiri ikiwemo Bajaji. Kama huwez ku afford 2k basi unganisha gari mpk Mwenge pale zipo za kwenda katikati ya mji. Au uende mpk Makumbusho zipo gari kule.

Sasa fikiria kuna mtu kaaa hapo kuanzia saa 12 et anasubiri Basi la Mwendokasi na mwingine na akili zake timamu anaona hiyo foleni bado anaenda kukata ticket.
Kumbe Mwenge na Makumbusho ni mjini? Basi sawa
 
Mjini sio kila mtu ana hela ya ziada mkuu. Kuna watu wanaishi ukitoa 500 kwenye mzunguko tiyari umeharibu. Na ujue ile imani kwamba gari litakuja, utasubiri utaona uongeze dakika 10, utaongeza 10 nyingine, 10 nyingine na ukitoka na daladala tu gari la mwendokasi ndio linafika. Na hapo utaunganisha kwenye foleni.
Sasa hao watu hapo karibu 300 hawana sh 500 ya ziada?.

Mie naona ni kukosa Akili ya kujiongeza na mazoea. Mtu kashakariri lazima nipande Mwendokasi wengine kusamehe hiyo hela aliyokata ticket roho inamuuma yuko tyr apoteze 4hrs kwenye foleni hapo.
 
Update: mvua zimeanza sasa,

Nilishawahi sema humu msipande mwendokasi.
Yaani serikali yenyewe imeshindwa kuwawajibisha, wale jamaa. Ile inajiendea tu.

Kiko wapi kelele la domo chafu RC wetu chalamila, wiki mbili, kikoooo wapiiii
 
abiria tupo wengi lakini mabasi hakuna, kuna watu wako hapa tangu Saa 12:10 Asubuhi (leo Novemba 15, 2023) lakini hakuna msaada wowote.

Kwanini utumie huo usafiri?

Kuna daladala hapo nyingi sana, huo usafiri wa mwendo kasi achana nao ndugu.
 
Ulivyoanza mradi wa mwendokasi, bus zote za kwenda mjini zikazuiliwa
Ilikuwaje mkakubali hilo zuio?

Kwa nini hamkuandamana kupinga hilo zuio?

Na kwa nini msiandamane hata sasa kupinga hilo zuio la kiukandamizaji ?
 
KUNA SIKU NILIKUJA DAR MWENDOKASI ZILIKUA NYINGI SANA ,NIKAJISEMEA MOYONI DAR HAWANA ADHA YA USAFIRI KABISAAA
 
Back
Top Bottom