Uchaguzi 2020 Hali ya maisha mtaani ni ngumu mno

Yaani ukikenua meno tu unapigwa mzinga. Kula mzigo ni juu yako lakini elfu walau 10 umpe. Taifa la kudanga.
 
Ccm yenyewe kwenye kampeni zake inadanga kwa serikali. Ni fedha za umma. Mtoaji mtoto wa Dada. La sivyo tungepeana shikamoo mitaani .
 
Kuna watu watatu walienda kukopa mahali, kila mtu kamaliza shida zake hawajapeleka rejesho hata moja mmojawapo ni ndugu wa karibu ananipigia simu nimpe pesa ana issue ya haraka kabla ya saa 9 jana hela iwe imepatikana, nikamwambia hata mimi sina amesononeka sana. Leo hapa nimeshatumiwa namba za simu nitume rambirambi ,. Nawaza mie shida zangu nipeleke wapi? bora kusingekuwa kunakucha.
 
maisha hayajawai kua rahisi, kama yamekaza ni kwako, kama ni magumu ni kwako pekee
 
Yani hapa tu nmetoka kuandika comment sim inaingia mtu ananiomba laki kweli??
 
Maraisi wa nchi huwa wanakuwa na "Tax exemption"
 

Kwa kweli umepiga ngumi ya uso, kama vile unanisema mimi hapa, nimeandamwa na watu kama 7 hivi kila mtu ananiliia hali mbaya, wakati na mimi nahangaika nitoke vipi.
 
Lini hali ya maisha iliwahi kuwa RAHISI ? Kwa mifumo na utamaduni wa waafrika kuuondoa umasikini kwa watu wengi itachukua muda sana.Iwezo wetu wa kufikiri unatia shaka.
Lissu anakuja kumfanya kila mtu tajiri na hakuna kulipa kodi wala sheria kumbana mtu unaishi utakavyo.
 
Wanaogopa kupewa kesi ya utakatishsji pesa Ila ukweli tar 28 oct..alaf kaa ukijua wanaojitambua utawakuta Twitter na jamiiforum tuu..huko insta na Facebook ni wasiojitambua ndio wapo
 
Tunaposema mtaani hali ngumu, CCM matawi ya juu huwa hawaelewi, maana wao wanajitumbulia tu watakavyo. Ukimwambia nenda kajiajiri wanaanza kulia lia kama yule mkuu wa Mkoa aliyetumbuliwa akasema hana pa kushika
 
Tunapaswa kuingia mtaani na kufanya chochote hadi haki ipatikane, tusitegemee tume ya uchaguzi hakuna kitu pale.
Tuoneshe mfano. Anza kwa kurekodi ka video tu ukihamasisha tuingie mtaani kufanya chochote.
 
Ili kumuongoza mjinga mfanye kuwa mjinga zaidi,jawabu lipo 28/10 mnalialia nini?fanyeni mabadiliko sasa
 
vip wewe bado huna uchumi wa katikati
 
Tuoneshe mfano. Anza kwa kurekodi ka video tu ukihamasisha tuingie mtaani kufanya chochote.
Usiwakatishe watu tamaa kwa woga wako, sio mara ya kwanza wala si jambo la ajabu kwa watanzania kuingia mtaani wakidai haki zao. Haki yetu ikiminywa tutaingia mtaani.
 
Njoo ununue vitunguu huku vimejaa hakuna wanunuzi. Wanunuzi walikuwa Wakenya, bwana yule kagombana na Uhuru Kenyatta biashara imeota mbawa. Vitunguu vinaozea shambani. Tunapokuambia hali ni ngumu ujue ni ngumu kwelikweli.
leta gunia nitanunua 90elf, soko liko na vinauzika, acha kufuata upepo, bambana kivyako kwa manufaa yako na familia yako,
waache hao wanao shida vijiweni wapoteze muda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…