Halikua lengo la Mungu binadamu tujisitiri tupu zetu. Pongezi kwa shetani

Ila kwer apa ukitaka kula kiboga unachomoka kama kuku jogoo shwaa unapiga unasepa😂😂tuanze tu
 
Uko sahihi na pia hauko sahihi. Haukuwa mpango kamili wa Mungu watu kuvaa nguo ili kujisitiri lakini pia halikua lengo la Mungu watu kuwa uchi.

Adam kabla ya kula tunda alitembea na utukufu wa Mungu uliomfunika kiasi kwamba hakuhitaji nguo. Utukufu wa Mungu ulimfanya Adam kung'aa hata kama ungeweza kumwangalia usingeona uchi wake.

Sasa kwa sababu utukufu ambao ndo vazi original kutoka kwa Mungu umeondoka, ilibidi kutafuta namna nyingine ya kujisitiri.

Mfano kidogo wa utukufu huu ni kama aliokuwa nao Musa wakati alipotoka kuongea na Mungu kwa siku 40, tukumbuke na Adam alikuwa na kawaida ya kuongea na Mungu kila siku kabla ya anguko ni vile hatujui ilichukua muda gani kabla ya kula tunda.

Kutoka 34:29
Hata ikawa, Musa aliposhuka katika mlima Sinai, na zile mbao mbili za ushuhuda zilikuwa mkononi mwa Musa, hapo aliposhuka katika mlima, Musa hakujua ya kuwa ngozi ya uso wake iling'aa kwa sababu amesema naye.
 
We unafikiri ni kwanini? walikuwa hawaoni dosari kuwa tupu, ila baada tu ya kula tunda wakajiona wako uchi na wakaaza kuona aibu.

Kwanini!!!?
 
We unafikiri ni kwanini? walikuwa hawaoni dosari kuwa tupu, ila baada tu ya kula tunda wakajiona wako uchi na wakaaza kuona aibu.

Kwanini!!!?
 
Binadamu hakujua mema wala mabaya. Bado natafuta mtu asiyejua mema wala mabaya anafananaje.
Nenda Rohoni Tena, utakavyoviona ni viwili tu, amani na utulivu,haya mengine ni ya nafsi ,,,,,zaidi tafuta watu wanaofanya tahajudi watakufafanulia zaidi kuhusu roho
 
Namaanisha,
Kama kweli binadamu tumedhamilia kumkataa shetani na Kila kitu CHAKE. Basi tuanze rasmi kuishi na kutembea uchi (Nudism) Kama viumbe wengine duniani maana Tangu mwanzo halikua lengo la Mwenyezi
Maada Yako umeiandika sana katika hisia za kimwili zaidi kuliko kiroho, unahitaji kujifunza zaidi utagundua kitu kikubwa sana hapo kwenye kitabu Cha mwanzo
 
Nenda Rohoni Tena, utakavyoviona ni viwili tu, amani na utulivu,haya mengine ni ya nafsi ,,,,,zaidi tafuta watu wanaofanya tahajudi watakufafanulia zaidi kuhusu roho
Rohoni sio kichaka cha kujifichia tunaposhindwa kueleza jambo? Binadamu alikula tunda katika mazingira ya kiroho au ya kinafsi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…