Halima Mdee bado una nafasi ya kutubu, Heshima na tamaa havikai pamoja

Msimtisha bhana, leo mnasahau huyu dada alivunjwa mkono akikipigania chama, leo mnamuona hafai. Mwisho wa chadema kesho kama misimamo yenu ndiyo hii
Hao Covid hawawezi kukiua chama,wafukuzwe mara moja!
 
Kukacha BUNGE ni kusababisha CHADEMA iwaombe WAFANYAKAZI wake nchi nzima WAJITOLEE....sasa kimekuwa chama Cha HARAKATI ama cha SIASA?!!!!

Yaani WAFANYAKAZI wote waishi kwa kujitolea?!!!
Kutakuwaje na TIJA?!

SIASA INAHITAJI FEDHA....
CHADEMA wameamua kusema kuwa "fedha si mtaji wa maendeleo".

RUZUKU Ni muhimu...
RUZUKU Ni muhimu....
 
Yaani kweli mnawaonea wivu wanawake kwenda bungeni kuwatetea wanawake wenzao? ungekuwa wewe kweli ungekataa? Acha wivu aisee.
 
Chadema WAACHE mfumo dume....
Chadema WAACHE kuwaminya WANAWAKE....

KUWAFUKUZA akina MDEE ni kukiua CHADEMA na kusaliti AKINA MAMA WANADEMOKRASIA....
 

Acha kupotosha watu chama kinategemea michango ya wanachama wake hayo mambo ya ruzuku hayo ni ya vyama dola kama CCM.

Kama kuna jambo litakalokiangamiza chama cha Siasa ni pale kitakapoacha wasaliti waendelee kubakia katika chama. Jibu ni moja tu hao wote ni kuwafukuza wameshindwa kuthamini michango yao katika chama kama ni pesa za kuimarisha chama mbona mabeberu wako tayari kutoa wakati wowote kwanini awe na njaa ya hivo kiongozi mkubwa kama huyo.

Binafsi nimemtetea sana katika jimbo la kawe hasa kwenye kata yetu na alipata kura nyingi sana. Ametukosea kiasi kikubwa sana tuliokiwa tunamuamini lakini sasa kwenye Siasa huwa hauhitajiki ushahidi wa mahakamani kwamba mtu anahatia kule kujulikana kuwa amekwenda kuapa bila kufuata utaratibu wa chama na yeye akiwa ni kiongozi amepoteza Sifa ya kuwa mwanachama.
 
Eti halima katunukiwa na CCM, kila mtu akivuruga CHADEMA Basi kanunuliwa na CCM, ila akivuruga wa CCM amejitambua hajanunuliwa na upinzani, so sad
Kamati kuu ya chama haijawapitisha,spika anajua na Mahera anajua!Nini kimetokea mpaka wakaapishwa?Kwanini Mahera na Spika wamekuwa tayari kuvunja katiba na sheria kwa kupitisha watu ambao hawajateuliwa na chama?Kwanini wameshiriki dhambi hii?
Hawa akina Mama wamesahau jinsi Lipumba alivyotumika kuiharibu CUF?Leo ametupwa kama mpira wa kondomu!
CDM wawafukuze upesi,hawa wanataka kukibomoa chama!
 
Loooh....

Kwa hiyo mnazisubiri FEDHA ZA MABEBERU?!!!

Zitapitia wapi kwa mfano?!!!
 
Future ipo chadema? Ulisikia wapi?
Mdee ana uhakika wa ajira ya miaka mitano, mshahara mono na uhakika wa kuinua mgongo!
Alafu hivi ni viti ni nafasi ya wanawake, mbona mma gubu nyinyi

Hivi katika watanzania milion zaidi ya 50 ni wangapi wametajiriwa rasmi hadi useme ati ana uhakika miaka mitano nani hana uhakika na maisha yake. Kila mtu alipo anauhakika na maisha anayoishi hivi Nyerere angekuwa na njaa ya hivo tungepata uhuru kweli. Mambo mengine ni ya aibu sana
 
A good and wise appeal. I'm not sure whether it will land on a live ear.
 
Yaani kweli mnawaonea wivu wanawake kwenda bungeni kuwatetea wanawake wenzao? ungekuwa wewe kweli ungekataa? Acha wivu aisee.
sina wivu nao mkuu. mimi ni mtu mdogo sana labda nionee wivu wadogo wenzangu. Bungeni waende hata miaka 100 lakini kuna utaratibu. Why walazimishe na kuleta taharuki?
 
Kumfukuza Hallima Mdee ni kuwaumiza vijana ambao wanafanya kazi NYUMA YA HAO WABUNGE 19......
 
Kumfukuza Hallima Mdee ni KUZIACHA FEDHA ZA RUZUKU....
 
Mabibi na mabwana na hasa wale walio wazalendo. Ni ukweli ulio wazi kuwa maji yakishamwagika huwa hayazoleki. Hata hivyo tunaweza kuganga yajayo.

Ni ukweli usiopingika kuwa, Bi. Halima ni mmoja kati ya makamanda shupavu kabisa walioipigania CDM kwa uaminifu mkubwa, licha ya kupitia katika changamoto nyingi.

Wandugu, kujikwaa si kuanguka na kosa moja halifukuzishi mke!

Siyo siri kuwa, tukio hili lililopelekea mtafaruku huu, limetusikitisha na kutusononesha mno. Kwa hakika itakuwa vyema sana kama tutashirikiana sote kulimaliza suala hili kistaarabu kwa mustakabala mwema wa chama chetu.

Ni furaha iliyo je mbinguni, mwenye dhambi mmoja akitubu?

Msingi wa hoja kama chama ni kutokutambua haramu ya uchaguzi 2020 na yote yatokanayo nao. Huu haupingiki aliye na hoja tofauti na atushawishi kwa hoja. Hiyo ndiyo demokrasia.

"Hapa pana namna ambayo suala hili Bi. Halima, litakwisha na adui yetu akatepeta na kulegea vilivyo:

1.Ombeni radhi kwa dhati kabisa mkijutia yote yaliyotokea.
2. Wekeni wazi bila kuficha kama ni Hadaa, ghiliba, ahadi, vitisho, nk na mkiwaweka wazi wote waliohusika na sarakasi hii. Koleo na likaitwe kwa jina lake.
3. Tuunganeni sote kumshambulia na kumwaibisha mbaya wetu.
4. Mengine kama yatakavyo shauriwa na waungwana wengine."

Sote tu wakosaji, shuruti tuwe tayari kusamehe 7x70.

Hayupo aliyepanga kukufukuzeni. Chonde chonde uamuzi wa kutofika huko mnao pia mikononi mwenu.

Ashindwe mbaya wetu na washirika wake wote.

Washindwe na walegee!
 
Mimi najiuliza,ataweza kuhoji kwa vurugu kama alivyokuwa mwanzo....sawa tuseme amejitutumua akafanya hivyo so nduu'gai ataamuru askari bunge wamtoe nje?vichekesho hivi!!!

Vitu vingine ni vya kijinga sana,na hapa ndo utakapojua na kuamini kwamba siku zote mwanasiasa zaidi ya kuangalia tumbo lake hana kingine anachojua hata ndugu zake hawajali coz wao ndo wanaojitungia sheria ila huwa wanatunga sheria za hovyo kiasi wanasahau kwamba zitawarudi hata ndugu zao.
 
Hata akitubu hawezi kuaminika tena milele.

Karma is real.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…