Halima Mdee: Deni la Taifa limefika Tsh. 71 trillion, maana yake kila mtanzania anadaiwa Tsh. 1 million na ushee

Yule mungu wenu mbona alikuwa anajinasibu kuwa akopi,kuwa miradi anafanya kwa fedha za ndani
 
Basi kila mmoja apangiwe deni lake alipe..
Ole wako uje kwangu kunidai hiyo hela! Nakukata panga akyamungu! Tena panga butu,hapa nadaiwa na kikoba,nadaiwa na mama birigita yule wa dukani,nadaiwa na muhindi ninayefanya kibarua kwake,nadaiwa na jamaa mwingine alinipa hela yake nimwekee nikaitafuna,nadaiwa kodi ya banda(nyumba?) Ya miezi saba,nadaiwa hela kibao baba kevi wa pale kilabuni,nadaiwa na muuza maziwa na wengine weeeeeengi kabisa,niacheni,nisije kuua mtu akyamungu
 
Hizo pesa Trilioni 71 alipeleka kwenya akaunti zake binafsi za uswisi? very poor argument.Barabara zilizojengwa huzioni? umeme kila kijiji huuoni? Elimu bure huioni? Ndege huzioni? Vituo vya afya nchi nzima huvioni? nk wewe kipofu?
Nyau ww, mbona lile limungu lenu lilikuwa linasema kuwa miradi yote anafanya kwa fedha za ndani
 
Hao wamisionari si ndiyo tulifundishwa huko gavmenti kuwa walikuwa wasoma ramani wa wakoloni? Endeleeni kubishana
 
Dah....Uzuri deni la JPM asilimia kubwa "halikuliwa na wajanja"....miundo mbinu inaonekana...mabarabara...majengo ya hospitali..masoko...nk nk.... JK alitumiaje hiyo mikopo?[emoji2960][emoji87][emoji87]

Sent using Jamii Forums mobile app
Jiridhishe vizuri wewe sukuma gang. Kwa rekodi za Tanroads JK ndiye aliyejenga miundombinu mingi huyo Mwendazake hata 1/4 hajafikia na wala hakuchukua kodi za dhuluma na hakutesa watumishi na deni halikupaa kama sasa. Nyerere alikuwa na ndoto ya kujenga madaraja 5 makubwa. Mto Mara, Kilombero, Malagarasi, Kigamboni, na Rufiji. Nyerere alijenga moja la mto mara; Mkapa alijenga la mto Rufiji. JK kajenga Kigamboni, Kilombero na Malagarasi.
 
Halima we, Halima we, Halima we, alisikika mh Seif (marehem) pia akimuita polepole, tafadhali rejea kundini, na polepole ukatubu kwenye kaburi la marehem Seif alikuita Mara tatu kipindi Cha uhai wake so chukua hatua
 
Nyau ww, mbona lile limungu lenu lilikuwa linasema kuwa miradi yote anafanya kwa fedha za ndani
ujinga kukariri notisi badala ya kuelewa unachosoma kwani ukikopa unalipa kwa hela zako au za mkopeshaji? si unalipa kwa pesa zako ulizokusanya ndani ziwe dola nk wasomi wapumbavu nyie mkiendelea na uelewa mdogo hivi kuna siku mtapigwa mawe na darasa la saba

kufanya kwa nje iwe kwa pesa za msaada ndio useme tumefanya kwa hela za nje.Akili hamna nyie

Iko siku wasiosoma watavamia vyuo vikuu na kuwakimbiza maprofesa na marungu kuwa hawajielewi waondoke darasa la saba wawe wakuu wa vitivo hasa wa vitivo vya uchumi
 
Mbunge asiyefungamana na upande wowote...hahahaha..
Hii nchi ina upuuzi mwingi sana.
Alafu mwingine alipe kodi huku watu wanazitumbua tu.....huu ni upumbavu wa hali ya juu.
Hivi Wabunge hawalipi kodi.....!!?
 
Kwa wasiofahamu mlolongo wa deni la taifa kwa tawala zilizopita,

1)Nyerere alikopa 3trln
2)Mwinyi alikopa 15trln
3)Mkapa hakukopa bali alijikita kulipa deni la mwinyi
4)Jakaya alikopa 25trln

Jakaya aliiacha nchi na deni la 35trln,

Kama hizi taarifa za deni la taifa kufika 71 trln ni za kweli basi Msukuma kwa miaka mitano amekopa 36 trln.

Kwa mikopo hii miradi inayoendelea kila kona haina cha ajabu tena nafikiri ingepaswa kuwa zaidi.Tulikuwa tunadanganywa tunafanya kwa pesa za ndani huku deni la taifa linakuwa kwa kasi.

Huyu msukuma alichojaaliwa ni roho mbaya tu lakini kiuhalisia ameua sana uchumi wa nchi yetu.
 
Decision ya kwenda kukopa (amount, wapi, kwa riba ipi, ili zifanyie nini) nadhani inapaswa asiachiwe Rais na kakikundi kake kadogo. Hii inatoa mwanya mkubwa wa wizi na ufisadi wa kutisha maana wanajua wao wataondoka na kutuachia msala sisi

Bunge makini lenye Speaker anayejielewa haliwezi kukubali huu upuuzi
 
Ukizungumzia Deni LA Taifa, etc kuna wabunge mjengoni hawaelewi kabisa. Hii kitu
 
Na kila Marekani anadaiwa takribani milioni 143 za kiTanzania,,Hizi siasa za kutoa sound bites zinazotisha ,zinatusaidiaje?hivi developing country unataka usidaiwe,kama tunataka hivyo ,let's become a high tax state kama Britain
Hautaki kujua uzito wa deni la taifa kwa lugha rahisi?
 
Nina maswali hapa mtaalamu, namba za madeni zilizotajwa humu na hasa kuhusu deni aliloacha JK ni Dollar bilioni 31, trilioni 35, trilioni 41, trilioni 43. Deni linalosemwa leo aliloacha Magu ni trilioni 71.

Mkapa akiondoka madarakani, aliacha deni kiasi gani? Maana nakumbuka nchi kusamehewa deni lote mwaka 2000, kabla ya kusamehewa lilikuwa kiasi gani na kabla ya kukabidhi nchi kwa JK, deni lilikuaje?

Wakati Mkapa anasamehewa deni, tuliambiwa amesamehewa lile deni halisi ila riba ataendelea kulipa, riba ilikuwa kiasi gani?

Je, mikopo iliyofuata haikuwa na riba? Kama ilikuwa nayo, ni kiasi kati ya hayo madeni yaliyorithiwa kutoka utawala mmoja kwenda mwingine?

Kiukaguzi, pesa iliyokopwa, ililingana na matumizi halisi ya sababu ya kukopewa?

Kama wewe au mtaalamu yoyote atanisaidia nielewe kwenye hayo maswali, nitashukuru sana.
 
Hautaki kujua uzito wa deni la taifa kwa lugha rahisi?
Kweli mkuu Nataka,lakini hii nyimbo nimesikia mda mrefu Sana ,sijawahi kuelewa ina-accomplish nn;wanatuhabarisha, ni reminder au there's hidden message!
 
Hebu mwambieni kwamba tunajenga kwa pesa yetu. Hatutaki pesa za mabeberu sasa deni linaongezeka vipi. Huyu atakuwa ametumwa πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Tunajenga kwa pesa zetu za ndani bwana huyo mdee anatumika kumchafua hayati. Hatukopi pesa ya Mabeberu tunajenga kwa pesa yetu ya ndani.
Kuopata vichekesho vingine kama hivi piga *155#
Usisahau na kile cha gawio la ATCL ambacho kilikuwa na exclusive perfomance ya hali ya juu.
Hivi mkuu unaweza kuniambia kichekesho kingine tafadhali kutoka team yenu.
 
Kasheshe kwa waliokuwa na wtt wengi maana si inabidi kuwalipia!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…