denooJ
JF-Expert Member
- Mar 31, 2020
- 18,509
- 68,228
Hapana, barua rasmi ndio kila kitu, kwasababu imeshaonekana hawa jamaa wanalindwa na Spika wa CCM na serikali yao, hivyo lazima ipelekwe barua [Mnyika ameshakiri kuipeleka], sasa kilichobaki ni Spika kukiri kuipokea na kuifanyia kazi.Acheni usanii....... Barua rasmi ni formality tu mbona Sofia Simba na wabunge 8 wa Lipumba hawakusubiri barua?? Press statement tu ilitosha kwa spika kuandika NEC kuwa viti vipo wazi!!!
Ni sawa na mtu ameshinda ubunge eti hatambuliki mpaka apate kile cheti Cha NEC!! Formalities zinaweza chukua hata wiki lakini hazizuii hukumu kutekelezwa. Mtu Hana uanachama toka juzi usiku then unasubiri barua kwanza?
Kangi Lugora alitimuliwa uwaziri stejini sasa angegoma kuachia ofisi eti kisa barua rasmi ya ikulu haijamfikia ofisini kwake??
Tuache usanii kesho mtadai minutes za kikao zimekosewa.... Kesho kutwa mtasema font haisomeki!!! Mnaharibu taswira ya nchi kama watunga Sheria hawafuati katiba.
On top of everything, ofisi zote hufanya kazi kwa maandishi, sio maneno ya mitandaoni. au magazetini.
Hii hoja unayoileta hapa, ndio ilitumiwa na Ndugai wakati ule kuwakingia kifua hao wahuni. Mpaka mdau mmoja huku nikamsoma akasema Mnyika akipeleka hiyo barua safari hii apigwe na picha kabisa, au arekodi na video.
Hii ifanyike ili kuondoa ile dhana iliyojitokeza mwanzo ofisi ya Spika kusema haikupokea barua, wakati Mnyika na Chadema walisema walipeleka.