Halima Mdee na wenzake watinga Bungeni licha ya CHADEMA kutangaza kuwafukuza rasmi

Halima Mdee na wenzake watinga Bungeni licha ya CHADEMA kutangaza kuwafukuza rasmi

Tatizo ni serikali yetu na viongozi wa juu haiwezekani katiba inapelekwa sivyo wametulia tu, mi ata sina shida nao wabunge wa COVID-19 waacheni nao wapige mipesa maana ata wasipopiga hakuna kinachobadilika kila mtu atakula kwa urefu wa kamba , ata wakitolewa izo pesa hazitufikii wala hatuambulii chochote zaidi ya kuishia kwenye mikono ya mafisadi
 
Mi naona watu kama wanaharaka sana kuwaona hao mabinti hawaingii bungeni sasa kama mnyika kapeleka barua leo ijumaa naimani hajamkabidhi spika Moja kwa Moja lazima itakuwa inepokelewa ofisi ya spika na masekretary wakati huo kikao kinaendelea na wale hawawezikuacha kwenda bungeni maana bado hawajazuiwa na spika spika akirudi ofisini mchana ataikuta barua ataisoma then maamuzi anaweza kutoa mchana huu sasa mnapolazimisha spika kapata barua ambayo ni ya leo kweli? Tatizo mnaharaka kama mmewabeba kichwani halafu siasa ukiichukulia hivi unaumiza kichwa tu
 
Barua imeshifika na imepokelewa, tunasubili reply. Ila hata hao wasaliti wanasubiri hiyo hiyo reply ambayo hatujui inaweza kuwa ya mchongo au haki. Waache walambe posho zao kwa mara ya mwisho..!
View attachment 2222688
Kwa maelezo hayainaweza kuwa imepelekwa (lakini hakuna ushahidi), spika anasema hajapokea barua (hakuna ushahidi)...yajayo yanafurahisha...
 
Barua impelekwa, haijapelekwa, waone aibu tu watulie mahali! Shame on them!
Wao ni lazima waeende bungeni. Barua ikishapelekwa ni sharti aloandikiwa akiri kuipokea.
Na kama kawaida ya spika wa ccm ni lazima atawasiliana na Ikulu kumpa maamuzi.

Kifupi tu ni kuwa Covid-19 wanaichafua Royal Tour!
 
Sasa aliyekata rufaa unampaje muda aombe msamaha wakati shauri lake halijasikilizwa? Hapo akikuomba msamaha means shauri la rufaa halina maana ni kulitupa tu. Bora nafasi ya kuomba msamaha wangepewa baada ya maamzi ya baraza kuu. Ningekuwa kiongozi, wabadilifu wangejipanga sana wakt wa kunipa maelezo ya upotevu wa rasilimali 😁😁
Hauoni ingekuwa vyema na bora kwao na kwa chama kama wangeomba msamaha na shauri la rufaa kutupwa ili waanze upya?
 
Dodoma. Baadhi ya wabunge kati ya 19 waliofukuzwa uanachama na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakiingia bungeni tayari kuendelea na shughuli za Bunge jijini Dodoma, leo Ijumaa Mei 13, 2022.

Jumatano ya Mei 11, 2022 Baraza Kuu la Chadema lilitupilia mbali rufaa za wabunge hao 19 kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kuwafukuza uanachama kwa tuhuma za usaliti kwa kukubali kwenda kuapishwa kuwa wabunge kinyume na msimamo wa chama hicho kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Sawa kabisa, maana spika hajapata barua, na hatujui ataipata lini, na akiipata aite kamati zake za kumshauri, na yeye apate muda wa kufanya maamuzi, kama maamuzi yana makosa, anayakataa
 
kaua wengi ndugu tena wasio na hatia na ndiyo maana damu zao zinanena hapa - hakuwa kiongozi makini - aliongozwa na mihemko. Imagine unamtoa mfungwa gelezani usiku wa manane then kesho yake asubuhi anaapa ati kuwa ubunge - akili hiyo.
Hebu taja aliowaua
 
Kuna invisible hand hapo,kama walivyotinga bungeni mwanzoni.
Kwa maelezo ya Mbowe walikataa kata kata kuomba msamaha.
Labda wanataka kucheza na mahakama kama Zitto alivyofanya alipofukuzwa Chadema.
Lakini wakifanya hivyo,watayumbisha chama.
Its sends out very bad signals kwa utawala huu wa sita . Na haswa Ccm
Kwamba if youve got connections you can violate any rules and the big boys are going to be there to give you support for you proliferation behaviour .
Halima na wenzake wamefukuzwa uwanachama , na wanakosa mandate ya kuwepo bungeni, uwepo wao bungeni si halali kwa maana yoyote , na naamini spika anajua kuwa wapo kinyume na sheria za bunge hilo.
 
Hii sinema ya Chadema bado inaendelea.
Pascal Mayalla imhotep Yoda Matola
Kuna watu wapuuzi kweli kweli...Chadema wametimiza wajibu wao na wamemaliza kazi yao. COVID-19 wamefukuzwa uanachama na kuendelea kuwahusisha na Chadema ni uhuni, period. Hata kama wamekata rufaa mahakami, hiyo rufaa peke yake haifuti uamuzi wa Chadema kama chama kuwafuta uanachama.

Kama baada ya maamuzi ya Chadema bado COVID-19 wameweza kutinga bungeni, ni wazi hatuna bunge bali tunalo genge tu linalotafuna pesa za wananchi kwa kibali maalum kutoka kwa watawala. Haingii akilini kwamba mhuni yeyote anaweza kutinga bungeni, chombo kinachotunga sheria na kuisimamia serikali.
 
Sawa kabisa, maana spika hajapata barua, na hatujui ataipata lini, na akiipata aite kamati zake za kumshauri, na yeye apate muda wa kufanya maamuzi, kama maamuzi yana makosa, anayakataa
Maamuzi ya kufukuzwa uanachama hayamuhusu kabisa spika !
 
hii nchi mwendazake alitaka kuiharibu vibaya sana, sema mkono wa Bwana umetuokoa !! mambo kama haya ni aibu kubwa kimataifa, looks like we're not organized & uncivilized.
Kila kitu mwendazake huo ni upumbavu ww
 
kaua wengi ndugu tena wasio na hatia na ndiyo maana damu zao zinanena hapa - hakuwa kiongozi makini - aliongozwa na mihemko. Imagine unamtoa mfungwa gelezani usiku wa manane then kesho yake asubuhi anaapa ati kuwa ubunge - akili hiyo.
Kijana ukiitwa mahakamani unao ushahidi wakutosha juu ya vifo hivyo au ni maneno ya kwenye kahawa.
 
Sawa kabisa, maana spika hajapata barua, na hatujui ataipata lini, na akiipata aite kamati zake za kumshauri, na yeye apate muda wa kufanya maamuzi, kama maamuzi yana makosa, anayakataa
Utaratibu wa barua ni dispatch book,sio maneno tu,aliyepokea barua ni nani?na sahihi yake kuwa kapokea.
 
Kuna watu wapuuzi kweli kweli...Chadema wametimiza wajibu wao na wamemaliza kazi yao. COVID-19 wamefukuzwa uanachama na kuendelea kuwahusisha na Chadema ni uhuni, period. Hata kama wamekata rufaa mahakami, hiyo rufaa peke yake haifuti uamuzi wa Chadema kama chama kuwafuta uanachama.

Kama baada ya maamuzi ya Chadema bado COVID-19 wameweza kutinga bungeni, ni wazi hatuna bunge bali tunalo genge tu linalotafuna pesa za wananchi kwa kibali maalum kutoka kwa watawala. Haingii akilini kwamba mhuni yeyote anaweza kutinga bungeni, chombo kinachotunga sheria na kuisimamia serikali.
Je unajua taratibu za ajira?
Vipi hao chadema wamepeleka barua yao ya kuwafuta uwanachama hao Covid?
Usiongee kwa mihemko tu kuwa bunge ni kama genge tu pale kuna sheria zinazofuatwa na wale bado wanatambulika bungeni hadi taratibu zote zifuatwe. Hapo nilijua utawalaumu viongozi wa chadema kwa kuchelewa kupeleka barua bungeni ya kuwafuta uwanachama wewe unalaumu bunge hapo umeonesha ombwe kubwa kuwa kuna sheria huzifatilii Mkuu.
 
Back
Top Bottom