Halima Mdee: Walichofanya wajumbe wa Baraza Kuu CHADEMA ni Uhuni! Mimi ni CHADEMA, nitaendelea kuwa CHADEMA

. Aliyekuwa mwanachama wa Chadema, Halima Mdee amesema hakukuwa na uhuru kwa wajumbe wa Baraza Kuu la chama hicho katika upigaji wa kura na kwamba, kilichofanyika ndani ya Baraza hilo ni uhuni.
Hakuna uhuni zaidi ya kuwa msaliti wa chama ulichokivujia jasho na damu.

Kusaliti watu waliokuamini na kukuheshimu; hata ambao hawakuwa wanachama wa chama chako.
 
Kwani chadema hawawezi kwenda mahakamani kuzuia hao wabunge wasihudhurie bungeni?

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
 
Hivi unajua wale sio Wanachama, mahakama itwasikilizaje watu ambao siyo wanachama wa chadema?.
Ndo maana nimemueleza wangekua wajanja wangeenda kuzuiwa kujadiliwa na kufukuzwa, sasa syo wanachama kwa mujibu wa katiba ya chama.
Wataenda mahakamani kama nani?

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
 
Kina Halima watafanya delaying techniques, wataenda Mahakamani.

So bado wana nafasi za kula hela ya nchi kidogo.

Unless otherwise iwe ni makubaliano kati ya Mbowe na Samia kua watimue na bungeni tuwatimue mlete wengine.
Hapo ni Mahakamani tu. Kesi inakuwa delayed mpaka 2024 ili watafune mishahara kidogo, basi tena ndo mambo ya ulaji wa kisiasa
 
Ni Bora Sasa wapeleke wawakilishi kule bungeni wa kuwasemea wananchi. Ni kweli waligomea matokeo, lkn Sasa hivi SERIKALI iliyopo madarakani inayafanyis kazi malalamiko ya vyama vya upinzani. Wakiendelea kugoma hawatawatendea haki wananchi
 
Shida ni kwamba kuna vitu kama nchi itapoteza. Je nchi ipoteze karibu 2 T kwa CHADEMA kuendelea na msimamo?
 
Yaani watu wote 423 ni wajumbe wahuni? / halima pengeni uliwapa mlungula wakakutolea nje au kulikoni?
 
Unaeleweka vizuri sana.
Lakini ni kama hayo yamekwishapitwa na wakati, kutokana na mahusiano mapya na utawala uliopo sasa. Ni kama vile Mbowe amekwishatambua uhalali wa serikali iliyopo madarakani. Kusema hawaitambui kwa vile uchaguzi haukuwa wa haki kutazua maswali yaliyo wazi: Mbowe anajihusisha vipi na uongozi usiotambulika na chama chake?

Mbaya zaidi, haiwezekani tena wakati huu kudai uchaguzi urudiwe tena!
 
Ni Bora Sasa wapeleke wawakilishi kule bungeni wa kuwasemea wananchi. Ni kweli waligomea matokeo, lkn Sasa hivi SERIKALI iliyopo madarakani inayafanyis kazi malalamiko ya vyama vya upinzani. Wakiendelea kugoma hawatawatendea haki wananchi
Viti maalum wanawakilisha wananchi gani?

Kama mnataka wananchi wapate wawakilishi CCM na serikali yake warudie uchaguzi mkuu, hii kwangu ndio better option ili kufuta ule ujinga wa 2020, lakini sio kuwaliwaza CCM kwa ujinga wao waliofanya makusudi.
 
Shida ni kwamba kuna vitu kama nchi itapoteza. Je nchi ipoteze karibu 2 T kwa CHADEMA kuendelea na msimamo?
Kama nchi ikipoteza vitu, hilo sio kosa la Chadema, ni kosa la wale wajinga waliochezea uchaguzi wakidhani wanawakomoa Chadema.

Kwangu haiwezekani kosa lifanywe na wengine, halafu masahihisho yake yaje kufanywa na wengine, muhimu waliofanya kosa ndio walisahihishe kwa kurudia uchaguzi mkuu, kama wakigoma lile bunge liendelee kubaki la CCM mpaka 2025.
 
Hapa patamu sana.

Ok, tukisema tumewasamehe CCM kwa zile rafu walizofanya makusudi kwenye uchaguzi mkuu uliopita, rafu ambazo zimesababisha leo hii wakina Mdee wamefukuzwa chamani tukiwaita wasaliti, kwanini basi na wakina Mdee wasisamehewe?

Kwangu, uamuzi wowote utakaosema yaliyopita si ndwele tugange yajayo, basi lazima uende moja kwa moja na kusamehe na kutibu yale majeraha yote yaliyosababishwa na kosa la msingi [rafu za uchaguzi 2020].

Je, utakuwa tayari kuwasamehe kina Mdee ili tuanze wote kwa pamoja? if No, kwanini uwagomee kina Mdee lakini uwasamehe CCM kwa zile rafu zao za makusudi?

Yes, ni CCM coz wakati ule wakitufanyia uhuni, Samia alikuwa mgombea mwenza, kama alikuwa hataki yale maovu angejiondoa kugombea, lakini nae akasikika akisema; "hata kama wasipotupigia kura bado tutangazwa washindi"

Hayo maswali unayoyaogopa kwangu ni suala dogo, nimeona next time wamesema Chadema watakutana na CCM na serikali yake kwa pamoja, hapa lazima CCM wakubali makosa yao na wafanye jambo kuyafuta, sijui kwanini unawatetea wasirudie uchaguzi? why unawahurumia?

Ujinga walioufanya wakati ule una gharama kubwa, na gharama hizo ndio wakati wao kuzilipa, na pesa za uchaguzi sio zao, ni za walipa kodi wa nchi hii.
 
Last kicks of a dying horse after butcher's sword has passed through the wind pipe
 
Lakini wanaendelea kuwa wabunge hadi kesi iamuliwe ina maana Chadema hawatakuwa na uwezo wa kuteua wabunge wengine

Wataendeleaje na Ubunge wakati sio wanachama?. Halafu walipata viti kwa njia isiyo halali.
 
Hivi hawatapewa mafao?

Unajua Kuna kesi ya forgery, hivyo ni mihimu kulijua Hilo. Maana walipata ubunge kwa njia ya udanganyifu na wakaapishwa sehemu isiyo rasmi nje ya bunge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…