Unaeleweka vizuri sana.
Lakini ni kama hayo yamekwishapitwa na wakati, kutokana na mahusiano mapya na utawala uliopo sasa. Ni kama vile Mbowe amekwishatambua uhalali wa serikali iliyopo madarakani. Kusema hawaitambui kwa vile uchaguzi haukuwa wa haki kutazua maswali yaliyo wazi: Mbowe anajihusisha vipi na uongozi usiotambulika na chama chake?
Mbaya zaidi, haiwezekani tena wakati huu kudai uchaguzi urudiwe tena!
Hapa patamu sana.
Ok, tukisema tumewasamehe CCM kwa zile rafu walizofanya makusudi kwenye uchaguzi mkuu uliopita, rafu ambazo zimesababisha leo hii wakina Mdee wamefukuzwa chamani tukiwaita wasaliti, kwanini basi na wakina Mdee wasisamehewe?
Kwangu, uamuzi wowote utakaosema yaliyopita si ndwele tugange yajayo, basi lazima uende moja kwa moja na kusamehe na kutibu yale majeraha yote yaliyosababishwa na kosa la msingi [rafu za uchaguzi 2020].
Je, utakuwa tayari kuwasamehe kina Mdee ili tuanze wote kwa pamoja? if No, kwanini uwagomee kina Mdee lakini uwasamehe CCM kwa zile rafu zao za makusudi?
Yes, ni CCM coz wakati ule wakitufanyia uhuni, Samia alikuwa mgombea mwenza, kama alikuwa hataki yale maovu angejiondoa kugombea, lakini nae akasikika akisema; "hata kama wasipotupigia kura bado tutangazwa washindi"
Hayo maswali unayoyaogopa kwangu ni suala dogo, nimeona next time wamesema Chadema watakutana na CCM na serikali yake kwa pamoja, hapa lazima CCM wakubali makosa yao na wafanye jambo kuyafuta, sijui kwanini unawatetea wasirudie uchaguzi? why unawahurumia?
Ujinga walioufanya wakati ule una gharama kubwa, na gharama hizo ndio wakati wao kuzilipa, na pesa za uchaguzi sio zao, ni za walipa kodi wa nchi hii.