Sema mwendazake alipotaka kuigawa Dsm alitakakufeli sana yaani maamuzi yakijinga kabisa
Anyway temeke aiwezi kua jiji ndani ya jiji Maybe vigawanye kua mkoa nanikitu ambacho akina maana yeyote!.
You are completely wrong and out of point!
Jiji moja kuwa ndani ya Jiji lingine inawezekana kabisa. Sema wewe binafsi kama walivyo Watanzania wengi zaidi mmekosa exposure na uelewa (elimu) ya kutosha kuhusiana na masuala haya ya Taaluma ya Mipango-miji au taaluma ya maendeleo ya Miji duniani. Hili ndilo tatizo kubwa Sana kwa Waafrika wengi.
Rais Magufuli alipotaka kuigeuza Manispaa ya Ilala kuwa ndio Jiji la Dsm alikuwa sahihi kwa kiasi kikubwa, Mimi binafsi nilimuelewa vizuri kabisa katika lengo na idea yake hiyo. Sema TATIZO kubwa alilokuwa nalo Rais Magufuli kuhusiana na suala hili ni kwamba hakuwa na uelewa/elimu ya kutosha kwenye suala hili la Mipango-miji na maendeleo ya miji, hivyo alishindwa kubuni au kuanzisha njia na mchakato sahihi ili kufanikisha azma yake hiyo aliyokuwa nayo. Aidha, pia alikosa Wataalamu Wabobevu wa kumpatia Mwongozo na Ushauri wa namma ya kufanikisha mchakato mzima wa lengo na ndoto yake aliyokuwa nayo, hata Wasaidizi wake wote aliokuwa nao hawana uelewa/elimu sahihi juu ya masuala haya ya maendeleo ya miji, na tatizo hili la kukosa wataalamu wabobevu kwenye masuala ya maendeleo ya miji bado lipo hadi Sasa.
Lengo la Rais Magufuli lilikuwa ni kuifanya/kuigeuza Manispaa ya Ilala kuwa 'Dsm Metro City,' na sehemu nyingine iliyobaki ya Mkoa wa Dsm alitaka iwe majiji mengine ambayo yangetambulika kwa majina yake, e.g. Kinondoni City, Kigamboni City, Temeke City au Ubungo City.
Na ukiyakusanya na kuyajumuisha pamoja majiji hayo yote kabisa yaliyopo kwenye Mkoa huo wa Dsm Basi yangeunda Jiji Moja kubwa Sana ambalo lingetambulika kwa Jina moja la 'DAR ES SALAAM METROPOLITAN CITY.'
NB: Chukua tahadhari ya tofauti iliyopo kati ya neno 'Metro City' na 'Metropolitan City.'
Mifano hai kuhusu Majiji ya namna hii ipo nchini Uingereza katika Jiji la London Metropolitan City, ambako Jiji Hilo limeundwa na Jiji la Greater London na majiji mengineyo. Aidha, hata katikà nchi ya Afrika ya Kusini nako Kuna Jiji la Johannesburg Metropolitan City, ambalo limeundwa na Majiji ya Johannesburg Metro City (aka: Johannesburg Central), Soweto City na Ekuruleni City.
Kwa hiyo Rais Magufuli katika suala hili alikuwa yuko sahihi, alikuwa na idea sahihi na nzuri, isipokuwa alikosa miongozo, elimu na uelewa sahihi kwenye suala hili.