Halmashauri ipi nchini inafaa kupandishwa hadhi kuwa Jiji la Saba?

Halmashauri ipi nchini inafaa kupandishwa hadhi kuwa Jiji la Saba?

Halmashauri inayofuata kuwa jiji la 7 Tanzania ni

  • Total voters
    118
  • Poll closed .
Hivi watu mnaichukulia Temeke poa....🤯
Tulikosea mfumo wa decentralisation tangu awali ndio sababu kubwa.

Mpaka leo foleni za magari asubuhi ni kuelekea kariakoo na Posta na jioni kuwatowa watu maeneo hayo kuwarudisha walipotoka.

Mbagala, gongo la mboto na Tegeta zilipaswa kuwa Center kubwa kwa watu wa wilaya hizo na kupunguza kundi kubwa la watu wote hao kuelekea kariakoo na Posta asubuhi.
 
Mbagala,Tandika,Gmboto na Tegeta zinaenda kuwa centre kubwa sana za kibiashara....ndani ya miaka 7 hii...
 
Mkoa Hauwi Jiji,ila Wilaya ndiyo huwa Jiji....
Wilaya ya Tanga ilikuja kuwa Jiji miaka ya 1970 by kipindi ilikuwa ina kubwa sana la fedha kutokana na mkonge na maelfu walikimbilia huko kutafuta ridhiki..
Mkoa mmoja unaweza kuwa na majiji mawili hata manne.
Naona hapo umechanganya.
Halmashauri (wilaya) ya Tanga mjini (sio mkoa wa Tanga wote) imekuwa jiji miaka ya katikati, sio miaka ya 1970. Zao la mkonge halilimwi Tanga mjini bali katika wilaya zingine za mkoa wa Tanga. Umaarufu wa kipesa wa Tanga mjini uliletwa na Bandari na viwanda vikubwa.
 
naom

nataka kuuliza kwani Jiji linawezq kua ndani ya jiji??

yaan kinondoni iwe jiji ndani ya jiji la dar es salaam
Kiufupi tu wewe fahamu, hakuna kitu kinaitwa jiji la Dar, ni mazoea tu kuita hivyo. Kiofisi na kisheria kwa Dar jiji ni Ilala. Mkoa hauwezi kuwa jiji bali manispaa ndani ya mkoa ndio inayoweza kupandishwa hadhi na kuwa jiji. Hivyo Kinondoni inaweza kupandishwa hadhi na kuwa jiji.
 
Naona hapo umechanganya.
Halmashauri (wilaya) ya Tanga mjini (sio mkoa wa Tanga wote) imekuwa jiji miaka ya katikati, sio miaka ya 1970. Zao la mkonge halilimwi Tanga mjini bali katika wilaya zingine za mkoa wa Tanga. Umaarufu wa kipesa wa Tanga mjini uliletwa na Bandari na viwanda vikubwa.
Inajulikana kama zao Mkonge lilikuwa likilimwa Wilaya nyingi huko Tanga,lakini Halmashauri ya Tanga ndipo
  • Malighafi yote ilipokuwa ikifika kwa kuchakatwa viwandani
  • Mzigo ukienda Bandari ya Tanga na kusafirishwa nje ya nchi
  • Uwekezaji wa Hoteli na makazi ya matajiri wa mkonge ulipofanyika.
Baada ya kupitwa kwa wakati kwa bidhaa za mkonge na soko lake kupungua,,,basi uchumi wa Jiji nao ukadolora na ndiyo mpaka leo hakuna cha ajabu kinachoendelea katika hilo Jiji.
Bandari imebaki jina tu.
 
Hata haya yaliyopo yaondolewe hadhi yawe mikoatu. Hali inakua tia maji tia maji uchafu, wizi ,vibaka,internet hamna yakueleweka, umeme sio wa uhakiki barabara hazipitiki wakati wa mvuaa
 
Ni kwamba kuna wazungu wameipenda wilaya ya Serengeti so mkurugenzi kaandaa propasal ya uwekezaji baada ya wadau kuikubali wakatoa go ahead, serekali kuu ilivyoona project ni kubwa wakataka wachukue hisa mwekezaji kawapa asilimia 21 za mradi,halmashauri nayo imechukua asilimia chache, asilimia kubwa anachukua mwekezaji,mpaka sasa mwekezaji kishatoa tirion 1.2 kuandaa master plan kiufupi huyu mwekezaji anabadilisha wilaya kuwa smart city kutakuwa na hotels za kisasa shule,miundombinu, apartments zilizopangiliwa reli na kiwanja kikubwa Cha ndege.
Kuandaa master plan trilioni moja?!!
 
Inajulikana kama zao Mkonge lilikuwa likilimwa Wilaya nyingi huko Tanga,lakini Halmashauri ya Tanga ndipo
  • Malighafi yote ilipokuwa ikifika kwa kuchakatwa viwandani
  • Mzigo ukienda Bandari ya Tanga na kusafirishwa nje ya nchi
  • Uwekezaji wa Hoteli na makazi ya matajiri wa mkonge ulipofanyika.
Baada ya kupitwa kwa wakati kwa bidhaa za mkonge na soko lake kupungua,,,basi uchumi wa Jiji nao ukadolora na ndiyo mpaka leo hakuna cha ajabu kinachoendelea katika hilo Jiji.
Bandari imebaki jina tu.
Umeshawahi kuishi Tanga?
Mimi nimekwambia kitu ambacho ninakifahamu.
Viwanda na mashamba ya mkonge yalikuwa mkoa Tanga lakini sio tanga mjini!

Viwanda vya kuchakata mkonge vilijengwa ndani ya mashamba ya mkonge na kisha ulisafirishwa na treni kutoka shambani kupelekwa popote. Na makazi makubwa ya wafanyakazi wa mkonge yalikuwa jirani kabisa na mashamba ya mkonge.

Tanga mjini kulikuwa na bandari, tena bandari busy, na kulikuwa na viwanda vingi vya mafuta, madawa, vyakula nk.

Mkoa wa Tanga umekuzwa na mkonge, lakini Tanga mjini palikuzwa na Bandari.
 
Kahama inaenda kwa kasi sana, labda na iringa japo sijawahi fika then morogoro

Moshi hapana kwakweli, ❌❌❌❌
Kama sio siasa Moshi ingekuwa mbali sana ila tangia uhuru Moshi ilionekana kama wapinga serikali hvo miundo mbinu na mambo ya muhimu ni juhudi binafsi za wanachi ila project nyingi kubwa zimekuwa zinapitishwa kushoto
 
Back
Top Bottom