Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM yawaita ili kuwahoji Kinana, Makamba na Membe

huu ni mtego kwa Kinana..... ndiye anayetafutwa ili abambikiwe kesi zisizokuwa na dhamana.

comrade Kinana nakushauri ubaki huko huko uliko kama kweli unajipenda!
 
Hii taarifa ipo hapa Jf muda mrefu sana bwashee!
 
Hapo mi namtafuta atayemung'amua kati kumuoji mzee makamba kinana na mzee membe,naomba nisubri kuona haya nais yanafurahisha yajayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
huu ni mtego kwa Kinana..... ndiye anayetafutwa ili abambikiwe kesi zisizokuwa na dhamana.

comrade Kinana nakushauri ubaki huko huko uliko kama kweli unajipenda!
Kinana juzi tulikuwa naye kwenye msiba wa Mafuruki!
 
Kipindi cha pili sasa.. ngoja niongeze popcorn huku nafatilia mtanange huu [emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi kuna mwanaccm atakuja kuiona mbingu kweli?tunapotunga sheria kwa kutumia pesa za wale tunaowaita wanyonge harafu hatuzitekelezi huwa ina mnufaisha nani?Nalaum umri wangu other wise ningehama Tanzania
 
Anatafutwa Bernard Membe. Mzee Makamba na Kinana hawana cha kupoteza hata wakifukuzwa CCM.

Inatafutwa njia kumzuia Membe asigombee urais kupitia CCM ili kumchallenge Jiwe. Hakuna kitu Jiwe anaogopa kama ushindani.

Jana Mzee Pinda kaongea uharo sana. Kubadili katiba ili Jiwe aendelee kuua Watanzania kwa kisingizio cha ndege, SGR na upuuzi mwingine.
 
Binafsi napata kigugumizi kuzungumzia mazingira ambayo mwanachama anakuwa na nguvu kuliko chama. Mazingira hayo yanaogopesha na kutisha sana, kwamba mtu kwa mamlaka yake na cheo chake ndani ya chama anakuwa ana sauti kuliko chama, yeye ndio sheria, utaratibu na katiba ya chama. Utaasisi ndani ya vyama unaanza pale hakuna mwanachama aliyejuu ya chama, hii inakipa chama mamlaka na uwezo wa kumuadhibu mtu si kinadharia bali kivitendo.

Daima naamini mwanachama sharti awe chini ya mamlaka na uwezo wa chama, kufanya hivi kunaongeza ufanisi na uwajibikaji wa wanachama kwa chama. Kuna baadhi ya vyama vya siasa hapa Tanzania wanachama wana nguvu kuliko vyama, mwenyekiti wa chama ana mamlaka makubwa ya kusimama kama chama yeye ndio anakuwa sheria na katiba, naomba nisitaje vyama hivyo ila vipo na badala yake tutafuta muda wa kuvizungumzia kwa mapana, leo tuizungumzie CCM.

Miaka zaidi ya 40, CCM inazungumziwa kama chama cha mfano Afrika na duniani kwa ujumla, hii ni kwa sababu ya utaasisi ndani yake unayoifanya kiwe na nguvu kuliko wanataasisi( wanachama). kila mwenye kuifikria Tanzania ya kesho huifikiria CCM na asilimia kubwa ya watanzania wanaamini taasisi imara huandaa viongozi imara.

Kama si utaasisi wa CCM, naamini CCM ingekuwa imebaki stori kama KANU ya Kenya au inapata upinzani mgumu kama ANC ya Afrika kusini. Bila ya kuwepo kwa matukio ya kuitikisa CCM kama kuhamia kwa wanaCCM upinzani kama ilivyokuwa kwa Mrema 1995( alihamia NCCR-mageuzi) na Lowassa 2015( alihamia CHADEMA) nakiri kusema upinzani si tishio kwa CCM. WanaCCM hao wanaohamia CCM wanapata nguvu kutokana na kujifunza mbinu za kuwa viongozi bora wanatumia mbinu hizo lakini kwa CCM ni mfumo imara hawakuweza kuwa zaidi ya CCM.

Uwezo wa CCM kumwajibisha, kumuhoji na kumuadhibu( kufukuzwa uanachama, onyo au karipio kali) mwanachama wake yeyote bila kujali umaarufu wake, imekiwezesha chama kujenga nidhamu kwa wanachama, kuaminika, kupendwa na kuheshimika kwa wanachama na watanzania kwa ujumla. Chama ni watu na nidhamu ya chama ni wanachama waadilifu na wenye sifa za kushika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama na serikali.

Waasisi wa CCM walituachia msingi huu kwa kuamini kwamba CCM itaendelea kuchaguliwa na wananchi na ni CCM pekee yenye jukumu la kuhahakisha uongozi na viongozi bora vipo muda wote. Nidhamu ya wanachama ni njia mojawapo la kudumisha msingi huu.

Tanzania ni yetu sote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…