Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM yawaita ili kuwahoji Kinana, Makamba na Membe

Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM yawaita ili kuwahoji Kinana, Makamba na Membe

Shallow analysis. hao wote ni kwa vile wako kwenye utumwa wa Jiwe na wanabembeleza kitumbua, wanaogopa kutekwa, kuuawa, kufilisiwa biashara zao, kuulizwa uraia etc, etc. Ngoja iondoke madarakani kama kuna amtu ataitwa akaenda! Think deep!
Nitajitahidi kukuletea in-depth analysis
 
Nchi ni uongozi thabiti na ni CCM pekee yenye uongozi thabiti hivyo bila uimara wa CCM nchi itayumba
Nchi ni katiba sio chama.
Ccm ni sawa na vyama vingine kama kufa na kuzikana,saccos,scauti,mpira nk.
Chama kinachobebwa na dola badala ya hoja utasema vipi ni thabiti.
Kitu thabiti ni kile kinachowezasimama chenyewe bila kubebwa.
 
Chama kikongwe barani Afrika kimefikia mahali mtu akionyesha nia ya kuchukua fomu ya kutaka apitishwe na chama kugombea urais wa JMT anageuzwa adui ili afukuzwe chama?
Kama aliyepo anajiamini kuwa chama kinampenda kwa nini asiache mkutano mkuu ndio ukaamuwa kumpiga chini Membe kwa aibu? Hayo maamuzi ni dhahiri sio ya CCM bali ya Magufuli na kikundi chake kidogo kinachoburuza wengine ndani ya chama.
Ni dhahiri fukuto la kukosa maelewano ndani ya CCM ni kubwa lakini linalindwa na tabia waliyo nayo KONDOO wa CCM ambao hawajui kuhoji hata wakipelekwa machinjioni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukipishana na mwenyekiti wa ccm labda lakini usipopishana naye hata ufanye nini utapongezwa tu"mfano bashite alipompiga warioba akapewa ukuu wa wilaya.
 
Subutu! CCM haiwezi kumuita au kumuazibu mtu kama Pinda aliye simama na kusemea anatamani katiba imruhusu Magufuli aongezewe muda.
Inaweza kumwita na kumuazibu mtu kama Kinana kwa vile kasema mwenyekiti ni mshamba, hata kama hajasema hadharani na maongezi yake hayo yamenaswa kwa jinai ambalo ni kosa kubwa kuliko kuita mtu mshamba.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naanza kuyasadiki maneno ya mjeda mmoja aliwahi kuyasema mwaka uliopita. Membe anatafutiwa zengwe afukuzwe chamani ili aondoe ushindani uliomo na akishatoka ataanzisha chama chake ambapo atagonga mwamba kutokana na madaraka alopewa msajili wa vyama vya siasa. Nasubir kuona huu utabiri ukitimia.
 
Back
Top Bottom