Nimesikitika kwamba, sijaona mahali popote ambapo wanavijiji ambao wametinza misitu hiyo kwa miaka dahari, wameshirikishwa na hivyo kuelezwa wao watanufaika vipi.
Haki ya kutafuta kuni, dawa na kulisha mifugo imezingatiwa vipi katika mkataba huo? Katika hicho kiasi kiduchu, wanakijiji watapata nini?
Kingine , naona halmashauri inafanya kama serikali kuu, kuna watu wanaojiita wataalam lakini? Sijui ni rushwa. Inakuwaje wanakubali vitu kama hivi?
Walishindwa nini wao kama halmashauri kufajya hiyo biashara badala ya kuwapa waarabu hao? Eti Mkurugenzi mtendaji, hata kama alikuwa hajasikia alishindwa nini kujipa muda na kujiuliza hawa watu watanufaika na nini?
Tanzania yangu, nakulilia hawa ndio wanaojiita wazalendo kwa kutoa bure raslimali za umma kwa bei ya bure!