Doubleg Malafyale
JF-Expert Member
- Feb 17, 2017
- 3,243
- 4,502
Halmashauri ya Meru (Meru DC), Mkoani Arusha, inachelewesha malipo ya pesa za kujikimu kwa walimu walioajiriwa katika Mwaka wa Fedha 2025/2026.
Walimu tumekuwa tukifuatilia malipo tangu Januari hadi sasa, lakini tumekuwa tukizungushwa bila kupewa maelezo ya kueleweka. Tunaambiwa kuwa fedha hizo tayari zimepokelewa na Halmashauri, lakini hakuna maelezo yanayotolewa kuhusu sababu za kuchelewa kutufikia walengwa.
Hali hii imeibua maswali na wasiwasi kuhusu matumizi ya fedha hizo ndani ya Halmashauri. Kuna madai kwamba huenda kukawa na matumizi yasiyo sahihi au ucheleweshaji wa makusudi wa fedha hizo.
Pia fedha hizo huenda zikitumika kwa muda katika shughuli nyingine za kibiashara ili kuzalisha faida, kisha baadaye faida hiyo kugawanywa kabla ya fedha kuwalipa walengwa. Hata hivyo, madai haya yanahitaji uchunguzi wa mamlaka husika ili kubaini ukweli.
Naomba mamlaka zinazohusika zifuatilie suala hili kwa kina na kutoa ufafanuzi kuhusu fedha hizo zilipokelewa lini, ziko wapi kwa sasa na sababu za kuchelewa kutulipa walimu.
Ucheleweshaji huu unatuathiri walimu tulioajiriwa na unaweza kuharibu taswira ya Serikali, huku baadhi yetu tukiona kana kwamba Serikali haitujali, wakati huenda tatizo likawa katika utekelezaji ndani ya Halmashauri.
Naomba uchunguzi ufanyike ili kubaini ukweli na kuhakikisha fedha hizo zinatufikia walengwa kwa wakati.