KERO Halmashauri ya Mkuranga watumishi hawapewi stahiki zao kwa wakati

KERO Halmashauri ya Mkuranga watumishi hawapewi stahiki zao kwa wakati

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Halmashauri ya Mkuranga watumishi hawapewi stahiki zao kwa wakati, zikiwemo likizo, uhamisho na stahiki nyingine.

Fikiria unaomba likizo yenye malipo, lakini hulipwi hadi miaka inapita. Unashindwa kuelewa kinachoendelea, na wanapokulipa baada ya miaka kadhaa, fedha hizo hukatwa bila sababu ya msingi.

Pia, unatokea Mkuranga lakini unalipwa nauli kuanzia Magufuli Stand.
 
WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MKURANGA KUDHURUMIWA STAHIKI ZAO ZA UHAMISHO NA LIKIZO

Kuna taarifa za malalamiko ya watumishi wa halmashauri ya Mkuranga, kudhurumiwa stahiki au malipo yao ya likizo na hata uhamisho, hali hii hutokea kwa watumishi wa halmashauri ya Mkuranga mkoani Pwani, kudhurumiwa ama kupunjwa stahiki zao za uhamisho na likizo

Jinsi inavyofanyika:

1. Mtumishi akifuata taratibu zote za kimfumo na kupata ruhusa ya likizo, pamoja na stahiki zake za likizo husika, akiwa aproved kwenda likizo huenda likizo wakati mwingine bila kupata hela yake kabla ya kwenda, akirudi likizo na kufatilia malipo yake kwa upande wa maafisa utumishi, huanza kuzungushwa na inapoonekana anafatilia sana huwa wanampa kiasi, mfano anatakiwa kulipwa 2,000,000/ basi wao humpa 500,000/, akidai sana tena kipindi kingine humpatia kidogo na kabla haijakamilika hiyo stahiki yake huambiwa hela zake zimeisha.

2. Maombi hayo mtumishi huomba kwa kuwasilisha barua pamoja na mchanganuo wa madai yake ila Cha ajabu ofisi ya mkurugenzi chini ya kitengo Cha afisa rasilimali watu (HR) hawamjibu mtumishi barua hiyo badala yake mtumishi ataitwa na kupewa kiasi kidogo kidogo mwisho anaambiwa pesa yake imeisha wakati akiangalia alichoomba na alichopewa hakiendani.

3. utaratibu huo huwa unafanyika nje ya mfumo, na nje ya akaunti ya benki yaani hufanyika kwa njia ya cash, dirishani na kusaini kwenye karatasi. Hii inaleta ukakasi kwanini usilipwe stahiki kupitia benki akaunti jambo ambalo ni rahisi kifuatiliaji. Pesa inatolewa bank ili mtumishi apewe mkononi. Huu ni uhujumu uchumi Kuna Nini chini ya hili?

4. INAPOTOOKEA UHAMISHO : Stori haitofautiani sana kwenye malipo japo huko watumishia huambiwa kwamba uhamisho wako tunauchunguza kwanza kama umehama kweli? Mara Kuna waraka wa waziri mkuu unatakiwa kulipwa tuu pesa ya usumbufu. jambo ambalo kwa mujibu wa Sheria za utumishi wa umma sio sawa.

5. Pia Kuna afisa utumishi moja wakiume yeye anatumia mamlaka yake vibaya kwa kuhamisha watumishi hovyoo kwa tamaa zake za kimwili.

Kweli utumishi wa umma ni uzalendo ila Hawa wanaopata nafasi wanatumia vibaya mamlaka yao na kupaka matope serikali hii tukufu ya CCM.

TAFADHALI MKURANGA ICHUNGUZWE SIO TUU KWA MSTAKABALI WA WATUMISHI BALI KWA MAENDELEO YA JAMII KWA UJUMLA.
 
Back
Top Bottom