Responded Halmashauri ya Mufindi tumeanza kulipwa fedha zetu za Kujikimu, japo tumelipa nusu

Responded Halmashauri ya Mufindi tumeanza kulipwa fedha zetu za Kujikimu, japo tumelipa nusu

A

Anonymous

Guest
Ningependa kutoa mrejesho kuhusu thread ya malalamiko niliyowasilisha hapo awali kuhusu kutolipwa fedha za kujikimu kwa watumishi wa Halmashauri ya Mufindi, Mkoa wa Iringa.

Soma: Mufindi: Watumishi wapya wa kada ya Tabibu Daraja la II na Maafisa Afya hatujalipwa fedha zetu za kujikimu

Nathibitisha kuwa tayari tumepokea malipo ya kiasi cha Shilingi 600,000/= kama ilivyoahidiwa na uongozi wa Halmashauri. Hata hivyo, kiasi hicho ni sehemu tu ya stahiki zetu, sawa na takribani nusu ya fedha zinazopaswa kulipwa.

Kwa mujibu wa hesabu za stahiki, jumla ya fedha za kujikimu zinazotakiwa kulipwa ni Shilingi 1,050,000/=, hivyo bado kuna salio ambalo halijalipwa.

Aidha, tumepokea taarifa kuwa kuna malalamiko kama hayo kutoka katika Halmashauri nyingine kuhusu kutokamilishwa kwa malipo ya fedha hizi za kujikimu kwa watumishi.

Tunaomba msaada zaidi katika kufuatilia na kusukuma suala hili ili malipo yaliyobaki yakamilishwe na watumishi wapate stahiki zao zote kwa wakati.

Tunashukuru kwa hatua iliyochukuliwa hadi sasa na tunaomba ufuatiliaji zaidi kuhakikisha suala hili linamalizika kikamilifu.
 
Back
Top Bottom