Responded ‎Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma yatoa ufafanuzi kuhusu video ya uchakavu wa vyoo Shule ya Msingi Muhamani

Responded ‎Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma yatoa ufafanuzi kuhusu video ya uchakavu wa vyoo Shule ya Msingi Muhamani

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
‎‎Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma imetoa ufafanuzi rasmi kufuatia video inayosambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa Jamii Forums ikionyesha madai ya uchakavu wa vyoo katika Shule ya Msingi Muhamani iliyopo Kata ya Simbo.
‎
‎Akizungumza kuhusu suala hilo Kaimu Afisa Elimu Awali na Msingi Bw.Reinfrid Nyeshawu amewataka Wananchi kupuuza taarifa hizo zisizoakisi uhalisia wa mazingira ya shule hiyo, akisisitiza kuwa Shule ya Msingi Muhamani haina kabisa changamoto ya huduma ya choo na kueleza kuwa baadhi ya taarifa zinazorushwa mitandaoni hazijazingatia ukweli wa hali halisi na zina lengo la kurudisha nyuma Jitihada zinazofanywa na Serikali.

Pia soma ~ Vyoo vya Shule ya Muhamani - Kigoma Vijijini vimejaa, Wanafunzi hawana pa kujisaidia

‎‎Kwa upande wake,Diwani wa Kata ya Simbo Mhe.Neema Chikilanoza ameeleza kuwa Serikali imeshatoa fedha kiasi cha Shilingi Milioni 110 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya elimu katika Shule ya Msingi Muhamani, ikiwemo ujenzi wa vyoo vipya pamoja na madarasa manne, hatua inayolenga kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa Wanafunzi na Walimu.
_HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA YATOA UFAFANUZI KUHUSU VIDEO YA UCHAKAVU WA VYOO SHULE YA MS...webp

_HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA YATOA UFAFANUZI KUHUSU VIDEO YA UCHAKAVU WA VYOO SHULE YA MSIN.webp
‎
‎Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Muhamani Bi.Leticia Lweja amefafanua uhalisia wa hali ya vyoo shuleni hapo, akieleza kuwa choo kilichoonekana kwenye video kilishafungwa na hakitumiki kabisa, kutokana na kuwa cha zamani na kutokidhi viwango.

‎‎Ameongeza kuwa shule hiyo kwa sasa ina vyoo viwili, kimoja cha zamani na kingine kipya ambavyo vinatumika, huku mipango ya Serikali ikiendelea kuhakikisha miundombinu yote inaboreshwa kwa viwango vinavyokubalika ili kuwaondolea adha Wanafunzi.
‎
‎Aidha baadhi ya Wananchi licha ya kupongeza Jitihada zinazofanywa na Serikali wamesema ni wajibu wao kushiriki moja kwa moja kwenye shughuli za maendeleo kwa michango ya hali na mali ili kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto wao na kuharakisha maendeleo ya sekta ya elimu.
‎
‎Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma inasisitiza dhamira yake ya dhati ya kuboresha miundombinu ya elimu, ikiwemo vyoo, madarasa na huduma nyingine muhimu, na kuwataka Wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali pamoja na kupata taarifa sahihi kupitia vyanzo rasmi.
 
Back
Top Bottom