Ingekua wapo walio nyuma yake raia wasingeandamana na kufurika mitaani kumpinga Netanyahu.
Muswada tunaupima kwa asilimia.
Asilimia kubwa ya raia wa Israel wamechoshwa na hili ndio maana wakaingia road kuandamana.
Hivyo hiyo asilimia kubwa ndio inatizamwa.
Ni Raia wote wa israel? Sasa hao raia kusema hivyo ndo inamaanisha kwamba Netanyahu ndo peke yake ndo anataka vita iendelee? Je, kipindi Netanyahu anatangaza vita si alitangaza na malengo ya vita, je hao wananchi walisema hatuyataki hayo malengo ya vita? Hiyo vita inapiganwa na israel na hamas, mbona hamas wao hawapo tayari kuachia mateka vita iishe?
Hiyo vita si Netanyahu ni waisrael na imebeba msitakabali wa maisha yao kama ambavyo mnasema hamas imebeba mustakabali wa maisha ya wapelestina.
Kwa hiyo acha kuendelea kupotosha kwamba Netanyahu ndo anataka vita kwa mustakabali wa kisiasa. Shida munaimba nyimbo zinazoanzishwa na Al Jazeera ambao pia ni washiriki wa vita ndo maana hiyo Al Jazeera imepigwa marufuku karibu nchi kubwa zote za kiislamu kwa tabia yao ya kutetea makundi yenye msimamo mkali wa kidini ya brotherhood…
Nikisema bro hauna unalolijua ninakosea!?
Kipindi Yair Lapid akiwa kiongozi wa Israel Gaza na Israel walikua na uhusiano mzuri sana kiasi kuna wayahudi ama wazayuni waliwekeza Gaza.
Aliporudi Netanyahu alifadhili baadhi ya Israel settlers wakiwa na IDF wavunje nyumba na kupanua makazi ya walowezi wa kizayuni,media zilikaa kimya,wapo hadi waisrael waliopinga hili.
Oktoba 7 Hamas walianzisha vurugu kwa malengo makuu matatu na walishayasema;
1)Mipaka ya Gaza ama Palestina itoke nje ya occupation ya Israel.
2)Waachiwe huru wafungwa wote wa kiPalestina hususan watoto wa chini ya miaka 12 ambao wamefungwa jela za jeshi la IDF.
3)Israel kuondoa jeshi lake maeneo yote yanaowahusu Palestina.
Vita ilipoendelea Hamas alitoa wazo ili vita ikome na mateka warudishwe hayo mambo matatu hapo juu yanatakiwa yatimizwe.
Simple tu ondoeni majeshi yenu,vunjeni occupation,wachilieni wafungwa wa kiPalestina kesha MATEKA WA Israel wote wataachiwa na kurudi kwao.
Netanyahu alikataa akisema mateka atakomboa mwenyewe na lengo lake ni kuiteketeza HAMAS isitawale tena Gaza.
Wananchi walipoona ndugu zao watatu ambao moja ya mateka wakipigwa risasi pasi na kufuata rules of engagement na jeshi lao lenyewe la IDF waliandamana wakishika mabango vita ikomeshwe fanyeni PRISONAL SWAP vita haina mshindi ni maumivu.
ASILIMIA KUBWA YA WAISRAEL WALIANDAMANA,kama umesoma hisabati nadhani unajua maana ya percentage,kitu tunakipima kwa asilimia.
Asilimia kubwa ya raia hawakuitaka vita ndio maana wakaandamana,na hiyo asilimia kubwa ni sawa na Israel wote.
Raia walikua wanataka mabadilishano ya wafungwa yafanyike na vita ikome.
NARUDIA NETANYAHU AKAKATAA.
Ndani bunge liligawanyika makundi mawili,wapo waliokua wanapingana na Netanyahu na wapo waliokua wanakubaliana na Netanyahu tena wachache sana.
Netanyahu ni waziri ambaye madarakani toka zamani anakaa kinguvu,ila raia wengi hawampendi na sio mara ya kwanza kuandamana yeye atoke.
Upande wa watu 350 kati ya 500 na upande wa watu 150 kati ya 500 upi usikilizwe!!??
Mkiambiwa ukweli mnasema tunapotosha.
HUNA UNALOJUA MKUU.
Maana hujaleta uthibitisho wowote.
Nataka ushahidi wa ALJAZEERA kufungiwa mataifa ya kiislam.
Maana hakuna taifa la kiarabu lililofungia chombo cha Aljazeera zaidi ya ISRAEL peke yake.
Hiyo Aljazeera unayosemea ni chombo cha habari ambacho kimepokea tuzo nyingi za kimataifa za kutokurusha fake news na haikuwahi kushutumiwa ilhali hadi BBC imewahi kushutumiwa.
Nasubiri ushahidi hapa wa Aljazeera kufungiwa Saudi Arabia au hata Jordan.[/QUOTE][/QUOTE]