Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Hali isiyotarajiwa imetokea mapema jana baada ya makombora sita ya masafa marefu kurushwa kutoka Gaza kuelekekea jiji la Jeusalem ambako ndiko ziliko nyumba mbili za waziri mkuu wa Israe.
Benjamin Netanyahu. Kwa hofu ya vitu kama hivyo Netanyahu inajulikana alizihama nyumba zake hizo mwanzoni mwa vita na kuhamia nyumbani kwa raifiki yake Mmarekani ambako kuna handaki la nyuklia.
Tukirudi kwenye makombora hayo ,ving'ora vilihanikiza jiji lote na kusababisha watu kukimbilia kwenye mashimo ambayo kikawaida huwa hayako mbali na barabara kote jijini humo.
Kati ya makombora 6 nusu tu ndiyo yaliyodakwa na Iron dome na mawili kukosa shabaha yake japo yalitua kwenye majengon na kuleta madhara madogo. Moja kati ya hayo matatu lilichukua kasi zaidi na likipitiliza jijini hapo na kutua mashambani nje ya jiji.
Mwandishi wa shirika la habari la China,Xinhua alishuhudia kikosi cha uokoaji cha Magen David Adom kikimbia huku na huko kufuatilia miripuko ya makombora hayo ili kujaribu kuokoa watu kama kungetokea madhara zaidi.
Kumbuka makombora hayo yamerushwa kutoka ndani ya Gaza na huenda ni kaskazini yake ambako jeshi la Israel lipo huku na vifaru na askari kadhaa na ni katika mwezi wa tatu tangu vita hivyo vilipoanza ikitarajiwa Hamas wamedhoofika kutokana na nguvu kubwa iliyotumika kuwapiga.