Hamdu Shaka, hivi kazi yako haswa ni nini, kumsifia Rais Samia au kuelezea Itikadi ya CCM?

Tatizo liko wapi kama anasifia mambo mazuri anayo yafanya Rais wetu.
hata mimi na wewe tunao wajibu wa kumsifia Rais wetu kwa mazuri anayo wafanyia watanzania.
Watanzsnia tuwe na akili, ukiajiriwa kutimiza wajibu fulani kama huwezi basi wapewe wanaoweza.
Shaka hakuajiriwa kuwa na kazi ya kumsifu Mama Samia.
Soma katiba ya chama.
 
Kati ya kazi nzuri sliyoifanya Magufuli ni kumfukuza Hamdu Shaka, kazi na Sijui Samia alikwenda kumtoa wapi?​

Akili yake anailinganisha na watu wa wa Sehemu gani Tanzania.​

Si Shaka pekeyake wengi wanasifia hata ambavyo hawajui.
 
Si Shaka pekeyake wengi wanasifia hata ambavyo hawajui.
Tatizo huyu kijana inaelekea hajapita chuo chochote kinacho fundisha itikadi , yaani development studies.
Angekuwa amepitia Kivukoni angekuwa muelewa.
Mama Samia inabidi awe careful na watu wa aina hii katika uongozi wake.
 
haiepukiki Mkuu. washangazi wa Mjomba nafikir umenielewa
 
Kuna namna ukiwa CCM lazima uwehuke...
 
Kuna namna ukiwa CCM lazima uwehuke...
Eti mtu na akili zake timamu anamshabikia kijana kama huyo mzururaji. Tunapigwa tozo ili aendelee kuzurura hovyo na wapo wananomshangilia! Adui nambari one wa taifa hili hakika ni CCM na hadi tuing'oe na kuitupa kule, hatuvuki!
 
CCM haing'oki kwa namana unayoitaka maana siye ndani ya CCM kuna kukosoana kistaarabu.
Ujumbe ukifika huwa unafanyiwa kazi, siyo hivyo vyama vyenu mnapinduana kila uchao.
 
Mkuu hakuna CCM, bali kuna rais ambaye ni mwenyekiti wa CCM. Rais ndio roho ya CCM, huyo ndio mwenye kuweza kuilinda CCM kupitia madaraka yake. Shaka anajua CCM imeshachokwa ila madaraka ya urais ndio yanayoipa uhai. Hivyo hana namna zaidi ya kumsifia rais ambaye ndiyo roho ya CCM.
 
Nakuelewa mkuu, sifa huwa zinapofusha.
Kina Polepole na Bashiru Ally walianza hivi hivi.

Hizi sifa za kumsifia rais ni Magufuli effect. Hii tabia ya kumsujudia rais iliasisiwa na Nyerere enzi za mfumo wa chama kimoja watu wakiwa wamelala. Ila ikaja kuibuka kwa nguvu ya kutisha kipindi cha Magufuli. Na sasa mama naye anatembelea humo humo. Na itachukua muda tabia hii kuisha, iwapo tutaendelea kuwa na katiba hiihii inayomruhusu rais kumteua yoyote kwenye nafasi yoyote kwa utashi wake.
 
CCM haing'oki kwa namana unayoitaka maana siye ndani ya CCM kuna kukosoana kistaarabu.
Ujumbe ukifika huwa unafanyiwa kazi, siyo hivyo vyama vyenu mnapinduana kila uchao.

Mnaamini mnakosoana kistaarabu, ukweli ni kuwa hamkosoani kistaarabu bali mnaishi kwa woga wa kukosa madaraka. Hivyo mtu akipewa ukweli wake anatii kwa shingo upande ili asitolewe kwenye ulaji. Siku CCM inatoka madarakani ndio utajua CCM haikuwa na uimara wowote zaidi ya kufaidi nguvu za dola. Itazikwa kaburi moja na KANU ya Kenya ikipoteza madaraka.
 
nafikiri hajui kazi zake, na waliomtuma pia hawamstui kuhusu kazi zake!
Kinachouma ccm wanafanya mikutano kila uchwao lakini vyama vingine vimefungwa pingu za miguu, mikono na bandage mdomoni!
 
Msimsakame kwa maneno atasusa arudi kwa mumewe kule Mombasa.
 
nafikiri hajui kazi zake, na waliomtuma pia hawamstui kuhusu kazi zake!
Kinachouma ccm wanafanya mikutano kila uchwao lakini vyama vingine vimefungwa pingu za miguu, mikono na bandage mdomoni!
Mzee Kinana inabidi amgutue huyu kijana.
Ama sivyo tunarudi kwenye modus operandi ya Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…