Hamdu Shaka, hivi kazi yako haswa ni nini, kumsifia Rais Samia au kuelezea Itikadi ya CCM?

Tusije jisahau kuwa chama chetu cha CCM ni chama cha wananchi, zamani tukiita Wakulima na Wafanyakazi.

Yametokea mabadiliko mengi katika misimamo ya chama kiasi ambacho watendaji ndani ya chama ni kama wanakengeuka katika misimamo yao kiutendaji.

Alipoingia mzee Abdulrahman Kinana ingalau tulianza kusikia misimamo ile ya kichama kulingana na matakwa ya wananchi , hasa wana CCM

Lakini kwa ndugu yetu huyu Shaka Hamdu mimi simwelewi, hatetei Itikadi wala kudadavua sera za chama.
Yeye kutwa kuchwa ni sifa kwa Mama Samia.
Si kwamba sitaki Mama Smia asifiwe, lakini tusisahau kuwa Mama Samia anawatumikia wananchi na ndio kazi yake.

Inabidi kwa kweli Shaka aingie tuition ya mzee Kinana ili aanze kuelewa hasa kazi yake ni nini.
Zote ni Kazi zake..

Tatizo hapo ni wivu Rais akisifiwa Wala hakuna jingine.
 
Labda linamtaka maana yule mama kwa kuzimiwa na vijana hajambo
 
Zote ni Kazi zake..

Tatizo hapo ni wivu Rais akisifiwa Wala hakuna jingine.
Mkuu kwa umahiri wako hapa JF I expected a better line of thought.

Siasa si mapenzi.
Siasa ni matarajio ya wananchi mimaendeleo kisiasa, kiuchumi na kijamii.

CCM inabeba matarajio hayo.
Mkuu wa Itikadi na uenezi kazi yake ni kuainisha, kuhamasisha na generally kuwaamsha wananchi katika matarajio hayo.

Kama hujaisoma katiba ya chama nikukumbushe:

Idara ya Itikadi na Uenezi
-Kushughulikia masuala ya msingi ya Itikadi na Sera za Chama Cha Mapinduzi.

-Kueneza na kufafanua Itikadi na Sera za CCM.
-Kupanga na kusimamia Mafunzo na Maandalizi ya Makada na Wanachama.
-Kusimamia Vyombo vya Habari vya Chama, Mawasiliano na Uhamasishaji wa Umma kwa Jumla.
-Kuongoza na kusimamia maandalizi ya Sera, Programu na Ilani za Uchaguzi za CCM.
-Kusimamia Utafiti, Maktaba na Nyaraka za Chama

Rejea sasa katiba ya chama, hakuna mapenzi wala wivu hapo.
Tunataka kazi iendelee.
 
Tusije jisahau kuwa chama chetu cha CCM ni chama cha wananchi, zamani tukiita Wakulima na Wafanyakazi.

Yametokea mabadiliko mengi katika misimamo ya chama kiasi ambacho watendaji ndani ya chama ni kama wanakengeuka katika misimamo yao kiutendaji.

Alipoingia mzee Abdulrahman Kinana ingalau tulianza kusikia misimamo ile ya kichama kulingana na matakwa ya wananchi , hasa wana CCM

Lakini kwa ndugu yetu huyu Shaka Hamdu mimi simwelewi, hatetei Itikadi wala kudadavua sera za chama.
Yeye kutwa kuchwa ni sifa kwa Mama Samia.
Si kwamba sitaki Mama Smia asifiwe, lakini tusisahau kuwa Mama Samia anawatumikia wananchi na ndio kazi yake.

Inabidi kwa kweli Shaka aingie tuition ya mzee Kinana ili aanze kuelewa hasa kazi yake ni nini.
Tulionya huko nyuma, sasa udhaifu umeshughulikiwa.
 
Back
Top Bottom