Hamis Chaurembo: Dereva mjinga aliyeuwa abiria kwa mwendokasi Kigoma

Nimewahi kupanda gari lake huyu jamaa. Nilijitahidi sana kumcontrol kuhusu mwendo. Abiria wenzangu waliishia kunidhihaki tu ati naogopa kufa wakati hukukwepeki. Lakini ilisaidia kwani alipunguza mwendo baada ya kuwa mkali sana.
Uoga nao pia ni akili!
 
Inawezekana lkni nenda kokote kwenye mamlaka zinazihusiana na barabara uliza mwendo wa eneo hilo ukipanda public service
Hiyo inawezekana tu kwenye magari ya kusafirisha mirungi kutoka meru county to NAIROBI.
 
TITANIC ICON 😊
 
Mkuu asante kwa hii post japo ni ya kusikitisha sana. Na jamii nayo ina makosa. Walikuwa wanampamba na majina badala ya kuchukuwa hatua ikiwemo kususia gari lake.
Kama ambavyo wanazipamba Sauli, katarama na Newforce huku vyombo vya dola vipo jamaa wanapokea tu bukubuku alafu siku ikitokea ya kutokea wanaanza kujiliza. Mapumbavu kabisa haya matanzania. Mi hata nikiwa naumwa sipandi hizo gari.
 
Wacha blah blah na hizo subconscious na uongo mwingine. Maneno na Roho "Yohana 6:63" kwani pia Mungu aliumba kwa Neno hivyo unatakiwa uwe makini na nini unazungumza.😅😆😁😄😃
 
Mamlaka husika za mkoa wa kigoma ziangalie pia zile Toyota wish za kasulu kutokea mwembe togwa. Kuna siku tutaongea mengine kwenye jukwaa hilihili, polisi wetu wasipagawe sana na zile buku tatu tatu za madereva wa wish na probox.

Alafu unakuta probox inabeba abiria 15, yaani mbele kwa dereva mnakaa wanne [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] hatari sana.
 
Wee chonza kumbe alishafariki? Yule alikuwa anaishi block Q? Baba khalid?
 
Hua inabeba mpaka 15 chief nimeshuhudia kwa macho yangu, kwenye buti kule ndio inakula nyomi ya kufa mtu.
Pale mbele was dereva wa4, kati wa4 Mpaka wa5 inategemea na unene wa abiria kule nyuma wanakaa 6-8 ... .noma sana nilipandaga Moja kutoka kyabaari kwenda Butiama aseee... Vifo vingine Mungu anasingiziwa.
 
Tatizo sio mwendo kasi bali mwendo kasi kwenye nchi gani na barabara gani.Nchi zetu miundombinu bado ni changamoto,unakuta barabara ni highway ila ina viraka na mashimo kama chandarua uku watumiaji wengine wa barabara nao wamejiachia bila kujali chochote.
 
Umesema sahihi Mkuu, barabara zote zingekuwa walau kama hicho kipande cha Kimara mwisho hadi Kibaha ingekuwa nzuri zaidi, maana unakuwa unaendesha bila kuwa na wasiwasi wa ubovu wa barabara.

Kama Nchi tuna safari ndefu sana kwenye upande wa miundombinu.

Kwa kweli JPM atazidi kukumbukwa kwenye hili eneo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…