CMG sio rahisi kudorola kwa mfanyakazi mmoja tu kuondoka
Ni kweli kabisa kipindi Kama kipindi kinaweza ku shake kidogo na hii ni kwa muda mfupi sana
Tuangalie coverage Kwanza. Efm na Clouds ni redio gani ina coverage kubwa kuliko nyingine? Utagundua ni Clouds
Turudi kwenye XXL, huyo the Navigator hicho kipindi alikuwa peke yake? Jibu ni hapana. Kama ni hapana, ana nini cha ziada? Jibu ni ana kipaji, ameshajijenga hivyo ana ushawishi kwa jamii ya vijana na wanamuziki. Sawa, hapa unajiuliza je, ni rahisi kuhama na mashabiki wake wote? Hapa jibu ni hapana kwasababu hata XXL yenyewe watu wanapenda segment ya mwisho ambayo inakuwa mseto ikiongozwa na Mchumvo
Kwa hiyo utagundua huenda na yeye akakutwa na waliyokutana nayo kina Gardener walivyoondoka na baadae wakarudi
Clouds imeji establish sana kiasi kwamba mtangazaji mmoja sio rahisi kuua kipindi akiondoka. Nadhani aliyebuni utaratibu wa kuwaweka wengi aliona mbali
Kazi kubwa naiona kwake kuanza kuwashawishi shabiki zake wahamie alikohamia ikiwa ni pamoja na wadhamini wa kipindi maana hao huangalia coverage na audience
But all in all, wakati mwingine ni bora kutembea tembea kuliko kukaa sehemu moja. Huko akafanye cha tofauti zaidi ili watu wathibitishe talent yake