Hamjagundua watangazaji vituo vya redio wameanza kung'olewa!?

Hamjagundua watangazaji vituo vya redio wameanza kung'olewa!?

Huu sasa nao utakuwa ujinga mwingine tena kuwala vichwa watangazaji wakubwa kama wale waliojizolea umaarufu kwenye tasnia hii. Nani asiyejua uwezo wa kitenge kwenye spoti leo pale radio one na zembwela na super mix pale east africa raddio? Hii bodi ingechora mstari tu kama kwenye ualimu. Kulikuwa kuna walimu wa upe, wakaja wa grade B na A, kisha wakaja walimu wa diploma na degree, hawa wa madaraja ya chini hawakuondolewa kazini mpaka wakastaafu na wengine walijiendeleza wapate viwango vya juu kiasi cha kubadilishiwa muundo wa utumishi wao na madaraja ya mshahara kulingana na ngazi ya elimu waliyonayo. Hii bodi ya ithibati kwa waandishi ingetambua tu kuanzia basic certificate na siyo waanzie diploma.
 
Hauwi Wakili mpaka upite Law School. Sheria ni suala nyeti. Hauwi kandarasi mpaka usajiliwe ERB, sababu uinjinia ni tasnia nyeti, hauwi mfamasia mpaka usajiliwe sababu dawa ni nyeti. Hauwi mganga wa kienyeji mpaka usajiliwe baraza la tiba asili Tanzania.

hivyohivyo habari ni suala nyeti. Hauwi mtangazaji au mwandishi habari mpaka usajiliwe bodi ya wanahabari.

Waende darasani hakuna namna!
Hakuna kuchambua magazeti kwa mihemko tena wala kupanda juu ya meza eti ubunifu!
 
6:33M

578

bodi ya ithibati

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

BODI YA ITHIBATI YA WAANDISHI WA HABARI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAANDISHI WA HABARI

KUONGEZA MUDA WA USAJILI WA WAANDISHI WA HABARI

Dar es Salaam tarehe 21 Juni, 2025

Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) inatoa taarifa ya kuongeza muda wa usajili kupitia Mfumo wa TAI-Habari hadi tarehe 28 Juni, 2025. Lengo ni kuwawezesha waandishi wa habari waliokamilisha usajili lakini bado hawajalipia ada ya Ithibati kufanya hivyo, pamoja na kuwapa fursa wale ambao wameanza usajili na hawajakamilisha kumalizia usajili kupitia kiunganishi cha TAI-Habari.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 17(1)(a), 17(2) ya Kanuni za Sheria ya Huduma za Habari, Tangazo la Serikali Na. 18 la mwaka 2017, wanaopaswa kujisajili ni pamoja na Waandishi wa Habari, Wahariri, Watangazaji, Wapiga Picha, Waandaaji wa Vipindi, Waandishi wa kujitegemea (Freelancers). Wanafunzi na Waandishi wa Kigeni waliokidhi vigezo vya kitaaluma katika kiwango cha elimu ya kuanzia ngazi ya Stashahada na kuendelea.

Bodi inawahimiza waandishi wote wa habari nchini kutumia ipasavyo muda huu wa nyongeza kujisajili na kupata Ithibati kupitia Mfumo wa TAl-Habari. Baada ya muda huo kuisha, waandishi wa habari watakaoshindwa kujisajili hawataruhusiwa kufanya kazi za kihabari, kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na masharti ya Kifungu cha 19 cha Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229.

Bodi inatoa onyo kali kwa mtu yeyote atakayewasilisha vyeti vya kughushi au taarifa za uongo katika mchakato wa usajili. Kitendo hicho ni kosa la jinai na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wahusika kwa mujibu wa sheria za nchi. Bodi itaendelea kuhakiki vyeti na kutoa vitambulisho kwa waandishi wa habari waliotimiza vigezo, kwa mujibu wa masharti ya Sheria hata baada ya muda wa usajili kumalizika. Usajili huu ni hatua muhimu katika mchakato wa kuanzishwa kwa Baraza Huru la Habari, kama inavyoelekezwa katika Kifungu cha 24 cha Sheria ya Huduma za Habari, Sura ya 229

Aidha, kwa kuzingatia uwepo wa Uchaguzi Mkuu mwaka huu, na kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 12(g) ya Kanuni za Utangazaji wa Uchaguzi kwa Vyama vya Siasa (Tangazo la Serikali Na. 775 la tarehe 18 Septemba, 2020), waandishi wa habari ambao ni wagombea wa nafasi za kisiasa wanapaswa kuzingatia kwamba hawajihusishi katika shughuli au majukumu yoyote ya kihabari katika vyombo vya habari walivyoajiriwa kwa muda wote wa mchakato wa uchaguzi.

Hatua hii inalenga kuzuia mgongano wa maslahi na kulinda uaminifu wa vyombo vya habari mbele ya umma, hususan katika kipindi cha uchaguzi. Aidha, kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni tajwa hapo juu, Waajiri wanawajibika kuhakikisha kuwa waandishi wa habari wanaogombea nafasi kisiasa wanasitisha utekelezaji wa majukumu yao ya kihabari kwa kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi.

Patrick Kipangula

Kaimu Mkurugenzi Mkuu

Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB)

matukiodaimatv

MUDA WA USAJILI WAANDISHI BODI YA ITHIB

Akifuatiwa na emmanuelchengula na wengine 10

Tuma

:

+
 
Huu sasa nao utakuwa ujinga mwingine tena kuwala vichwa watangazaji wakubwa kama wale waliojizolea umaarufu kwenye tasnia hii. Nani asiyejua uwezo wa kitenge kwenye spoti leo pale radio one na zembwela na super mix pale east africa raddio? Hii bodi ingechora mstari tu kama kwenye ualimu. Kulikuwa kuna walimu wa upe, wakaja wa grade B na A, kisha wakaja walimu wa diploma na degree, hawa wa madaraja ya chini hawakuondolewa kazini mpaka wakastaafu na wengine walijiendeleza wapate viwango vya juu kiasi cha kubadilishiwa muundo wa utumishi wao na madaraja ya mshahara kulingana na ngazi ya elimu waliyonayo. Hii bodi ya ithibati kwa waandishi ingetambua tu kuanzia basic certificate na siyo waanzie diploma.
Kuwaita watangazaji si sahihi. Utangazaji ni taaluma. Kama hawana vyeti stahiki sio watangazaji
 
Back
Top Bottom