Hamna watu wanaotapelika kirahisi kama waumini wa dini hii

Hamna watu wanaotapelika kirahisi kama waumini wa dini hii

Kama mtu hutamiliki gari hapa duniani kaa ukijua akhera hamna magari wala simu yani hamna kitu chochote cha kujifurahisha bali kuna pombe na wanawake
Kuna starehe nyingi,siyo pombe na wanawake tu
 
Akili ya mtu hupelekea kufanya huo upumbavu unaouongelea sio kilevi. Hivi wewe unadhani ni wote ambao wanafanya huo upumbavu wakilewa?

Mfano mzuri ni Mama yangu mkubwa, huwa akilewa anaenda kujipumzikia ndani hiwezi kusikia anabwabwaja kuongea upumbavu.

Mwingine ni Baba yangu, yeye kwanza hanywi sana kwasababu ufahamu aliyopewa na MUNGU unamsaidia kutambua madhara ya excessive use of alcohol so huwa anatumia kiasi then anaenda kujipumzikia ndani.

Ugaigai wote unaofanywa na walevi ni matumizi mabaya ufahamu ambao ni zawadi kutoka kwa MUNGU.

Usilete ujinga wa kusema eti mbinguni watu wakilewa hawawezi kuleta maafa kwanza nani amekwambia watalewa? nani amekwambia mbinguni kuna bia? Nani amekwambia mbinguni kuna gongo,henessy na mapombe mengine?

Acheni kupotosha watu matapeli wa kifikra nyiee!!
Mathayo 26:29...Kama ana ufahamu hajalewa Ila kanywa pombe
 
Eti ungali hai unakatazwa usitumie pombe na usiwe mzinzi, lakini cha ajabu ukishakata umeme unaruhusiwa kutumia vyote, inabidi uzimie uzinduke kama mara trilioni hivi ndipo utaweza kuelewa huo mstari [emoji1787]
Bora Pepo hii aliyoihaidi ALLAH kuwa wale waliomuamini na wakatenda wema ataenda kuwapa starehe zisizo na ukomo. Hakuna kuabudu huko peponi kwa kuwa duniani ulishajipinda kufanya ibada, kwa wanaume wataensa kupewa wanawake special ambao jicho halijapata kuwaona wala nafsi kuwaza jinsi uzuri wao ulivyo, na kwa wanawake walioamini na wakatenda mema nao wataingia peponi na wataozeshwa kwa wanaume walioingia peponi na si hivyo tu ,ALLAH atawapa maumbo bora kuliko haya waliyokuwa nayo duniani na watakuwa ni wazuri zaidi ya Hur al ayn. Pia kutakuwa hakuna kuzeeka peponi na hakuna kwenda haja, haja zitatoka katika mfumo kama wa jasho ambalo linanukia harufu ya miski. Mtu atakula na kunywa kile nafsi yake inachokitamani.

Tofauti na pepo ya kikristo ambayo wanaambiwa wataenda kukaa na malaika kuabudu tu mwanzo mwisho. Hapa duniani ukiambiwa ukae asubuhi mpk jioni unafanya ibada mwenyewe ufaomba poo! Sembuse huko peponi.
 
Kuna kiongozi mmoja wa dini ya kiislam yupo huku zenji anaendesha kipindi kwenye radio cha kujibu maswali anaitwa musabaha alipoulizwa swali hilo eti akasema "hiyo ni Siri ya Mungu tuache kutaka kujua kila kitu"

Hili ni swali gumu sana kwa waislam
Kwa wanaume sio siri ila kwa wanawake ni siri. Mambo mengi muda mchache
 
Kuna mwamba huko nchini DRC anajiita Nabii, aisee mwamposa mwenyewe cha mtoto, jamaa anajaza uwanja wa taifa wa DRC pale kinshasa kila jpili, watu zaidi ya 80000 wanajaa kwenda kumshuhudia huyo nabii feki.

Biashara yake haina tofauti na ya mwamposa kwani yeye anawauzia dawa anawaaminisha kuwa inaponya magonjwa ya kila aina, anauza lita moja ya mchanganyiko wa Gasoline & limao kwa thamani ya euro 14 (takribani elfu 36 za kitanzania).Jamaa sasa hivi ni miongoni mwa multi-millionaire nchini DRC
 
Kuna kiongozi mmoja wa dini ya kiislam yupo huku zenji anaendesha kipindi kwenye radio cha kujibu maswali anaitwa musabaha alipoulizwa swali hilo eti akasema "hiyo ni Siri ya Mungu tuache kutaka kujua kila kitu"

Hili ni swali gumu sana kwa waislam
Ni kweli shahidi atapewa wanawake hur al ayni ...na si shahidi tu bali kila mwanaume atakaefuzu kuingia peponi atapewa hur al ayni ( ambao ni bikra, yaani hakuna mwanaume aliyewahi kuwagusa isipokuwa yule atakaetunukiwa na ALLAH).
 
Ungejikita kwenye hii mada ingekuwa jambo jema sana.

Ngoja nikusaidie. Allah aliyotufunulia na kutujuza ni machache sana kuliko ambayo hajatufunulia hasa katika malipo ya waja wema.

Kwahiyo malipo ya Wanawake wema anayajua Allah, ila wanawake wa peponi watakuwa bora zaidi ya hao mabikra tutakao pewa huko peponi. Mola wetu atujaalie pepo ya juu kabisa.

Kuna muda mnatakiwa muwe mnatumia akili zaidi ya mihemko. Someni,kisha mtafakari muujue ukweli.
Amin thuma amin
 
Kama mtu hutamiliki gari hapa duniani kaa ukijua akhera hamna magari wala simu yani hamna kitu chochote cha kujifurahisha bali kuna pombe na wanawake
Peponi kutakuwa na vipando pia na vinavyosafiri kwa kasi kuliko hivi vya duniani. Pepo itakuwa na madaraja kwa mujibu wa uchamungu wa Mtu. Kuna watakaokuwa pepo ya juu zaidi( Mitume, mashahidi,wachamungu n.k) na wengine watakuwa katk pepo za chini...umbali kati ya pepo moja na nyingine ni safari ya miaka 500
 
Mombasa, Kenya

Ndugu hawa walioamua kwenda upande wa pili wakati wamekulia upande mwingine. Wote yaani wanaonekana wameamua kubaki upande mpya wa pili mbali ya kujaribu kutikiswa imani yao mpya kuhusu upande wa pili. Waliojaribiwa mmoja ni wa jinsia ya kiume na mwingine ya kike, lakini wote wameamua kushikilia imani yao mpya kuhusu upande wa pili kama video ilivyorekodi :

Dawah kanisani kwa pastor Ezekiel | Waislamu wakatalia kanisani.

 
Naona watu wanastuka kuwa mwanaume wa kiislam akiingia peponi atapewa Hur al ayni( wanawake special walioumbwa kwa ajili ya peponi)...ni hivi Mtume Muhammad pbuh anasema kuwa mwanaume wa peponi atapewa nguvu za wanaume mia wa duniani ,yaani uwezo wa wanaume mia unapewa mtu mmoja hivyo kuwahudumia (kuwaridhisha) hao wanawake 72 sio ishu sana na pia ni hivi huko peponi hakuna kuzeeka. Watu wote watakàoingia peponi watakuwa katika umri wa ujana mfano wa miaka aliyokuwa nayo Mtume Issa mwana wa Mariam kabla hajapaishwa kwenda mbinguni (takribani miaka 33).

So nguvu za kujamiiana huko haziishi ni vile mtu tu atakavyojiskia. Mtu wa chini kabisa kwa peponi atapewa ufalme mara kumi zaidi ya ufalme waliopewa wafalme wa ulimwengu huu...Imagine hao ambao wako katika daraja za juu ufalme wao peponi ukoje.

Mito ya Asali, Maziwa, mvinyo n.k mtu atakuwa anajichotea tu . Hayo ni machache tu ambayo Allah amemfunulia Mtume wake . Ila kuna mengi huko ambayo nafsi haijapata hata kuwaza. Bilauri za Dhahabu na fedha, lofty mansions n.k

Mungu tujaalie waja wako tuwe miongoni mwa watakaoingia peponi bila ya hesabu ameen
 
Bongo utakuta mtu anaitwa Mohammed Juma Abdullah anakwambia hana jina la ukoo lenye asili ya kwao, lakini huko Afrika Magharibi waislam wana majina asili kabisa kama NGOLO KANYE, SADIO MANE etc, Bongo tunaona utamadani wa watu ndio ujanja

Mkristo/yahudi ama pagani kabla ya kusilimu alikuwa akitumia jina la James, mapunda cjui shoziniga. Sasa mtoto na baba wote wamesilimu wakaitwa majina mazuri ya kiisilamu Abdallah, Said, Suleiman n.k. na kuachana na majina ya kikafiri. Sasa hapo unataka akupe jina gani tena mzehe. Wakati majina mazuri ndiyo haya ya kiislamu.
 
Wakristo lazima muichukie hii pepo tuliyoahidiwa na Mola wetu maana kwenye vitabu vyenu mmeambiwa mnaenda kuabudu tu mwanzo mwisho hakuna kula ,hakuna wanawake, hakuna starehe yeyote.


Kwanza mnasema kuwa mnamfuata Yesu ila hakuna sehemu iliyoandikwa kuwa Yesu ameoa au kufundisha watu waoane. Je nyie huo ujasiri na mafundisho ya kuoa mmeyatoa wapi?

Wanawake tuachieni sisi waislam tuzidi kuwaoa maan kwetu tumeruhusiwa kuoa hadi wanawake wanne.
 
Pamoja na yote hayo bado Yesu ni Mwokozo, na hakutokea magharibi bali alitokea juu mbinguni. Ili akuokoe wewe unayeonekana kama ni msafi lakini kumbe mambo yako ya sirini yanatisha. Uokolewe leo!
 
Kunachofanywa na manabii fake kina mwamposa na wenzake ni utapeli ambao ulishafanywa na televangelists huko nchini marekani mwanzoni mwa miaka ya 2000 , wanahubiri kuhusu mafanikio na pesa tu. Yaani mzunguko wote wa mahubiri yao yanaangukia ktk kupata pesa kwa wajinga wengi wanaowafuata na kweli wamefanikiwa ktk hilo.

Chupa ya maji ya sh 300 ya kampuni ya canada wanawauzia watu kwa sh 2000.Chumvi ya jero mtu anauziwa 5000-10000.
 
Kuna ile video imetrend, wanawake wananyolewa mavuzi na wanaume huko lanisani nchini ghana. Mwenye video atupie hapa jinc wanawake wanapigwa wembe.
 
Islamic wengi ni waganga wa kienyeji,, hujiita wanatoa mashetani kwa njia ya kitabu cha dini yao huku uhalisia ukija kuwa ni matapeli na waganga wa kienyeji...

Wakristo ndio sina la kuongeza,, Wamekuwa wanapelekwa kama bendera..

Note: Dini tu yenyewe ni Mchongo.
Wapi sahihi au kipi sahihi tufuate?
 
Ni kweli watu wanapishana hawa wa imani hii wanaenda kwa waganga wengine wanaenda kwa manabii, yaani ni mchanganyiko wote kuna kitu wanatafuta nje ya imani zao

Waislamu wanaoenda kufanyiwa miujiza kanisani | Nini tatizo?​


Muislamu kwenda kanisani kufuata hiyo miujiza ni sawa tu na mtu wa dini kwenda kwa mganga kwa ajiri ya kutatua shida yake hali ya kuwa bado ana imani na dini yake.
 
Back
Top Bottom