inamankusweke
JF-Expert Member
- Apr 24, 2014
- 20,344
- 21,967
Kuna starehe nyingi,siyo pombe na wanawake tuKama mtu hutamiliki gari hapa duniani kaa ukijua akhera hamna magari wala simu yani hamna kitu chochote cha kujifurahisha bali kuna pombe na wanawake
Mathayo 26:29...Kama ana ufahamu hajalewa Ila kanywa pombeAkili ya mtu hupelekea kufanya huo upumbavu unaouongelea sio kilevi. Hivi wewe unadhani ni wote ambao wanafanya huo upumbavu wakilewa?
Mfano mzuri ni Mama yangu mkubwa, huwa akilewa anaenda kujipumzikia ndani hiwezi kusikia anabwabwaja kuongea upumbavu.
Mwingine ni Baba yangu, yeye kwanza hanywi sana kwasababu ufahamu aliyopewa na MUNGU unamsaidia kutambua madhara ya excessive use of alcohol so huwa anatumia kiasi then anaenda kujipumzikia ndani.
Ugaigai wote unaofanywa na walevi ni matumizi mabaya ufahamu ambao ni zawadi kutoka kwa MUNGU.
Usilete ujinga wa kusema eti mbinguni watu wakilewa hawawezi kuleta maafa kwanza nani amekwambia watalewa? nani amekwambia mbinguni kuna bia? Nani amekwambia mbinguni kuna gongo,henessy na mapombe mengine?
Acheni kupotosha watu matapeli wa kifikra nyiee!!
Swali gumu umeona wewe...na hapakua na swalu
Bora Pepo hii aliyoihaidi ALLAH kuwa wale waliomuamini na wakatenda wema ataenda kuwapa starehe zisizo na ukomo. Hakuna kuabudu huko peponi kwa kuwa duniani ulishajipinda kufanya ibada, kwa wanaume wataensa kupewa wanawake special ambao jicho halijapata kuwaona wala nafsi kuwaza jinsi uzuri wao ulivyo, na kwa wanawake walioamini na wakatenda mema nao wataingia peponi na wataozeshwa kwa wanaume walioingia peponi na si hivyo tu ,ALLAH atawapa maumbo bora kuliko haya waliyokuwa nayo duniani na watakuwa ni wazuri zaidi ya Hur al ayn. Pia kutakuwa hakuna kuzeeka peponi na hakuna kwenda haja, haja zitatoka katika mfumo kama wa jasho ambalo linanukia harufu ya miski. Mtu atakula na kunywa kile nafsi yake inachokitamani.Eti ungali hai unakatazwa usitumie pombe na usiwe mzinzi, lakini cha ajabu ukishakata umeme unaruhusiwa kutumia vyote, inabidi uzimie uzinduke kama mara trilioni hivi ndipo utaweza kuelewa huo mstari [emoji1787]
Kwa wanaume sio siri ila kwa wanawake ni siri. Mambo mengi muda mchacheKuna kiongozi mmoja wa dini ya kiislam yupo huku zenji anaendesha kipindi kwenye radio cha kujibu maswali anaitwa musabaha alipoulizwa swali hilo eti akasema "hiyo ni Siri ya Mungu tuache kutaka kujua kila kitu"
Hili ni swali gumu sana kwa waislam
Ni kweli shahidi atapewa wanawake hur al ayni ...na si shahidi tu bali kila mwanaume atakaefuzu kuingia peponi atapewa hur al ayni ( ambao ni bikra, yaani hakuna mwanaume aliyewahi kuwagusa isipokuwa yule atakaetunukiwa na ALLAH).Kuna kiongozi mmoja wa dini ya kiislam yupo huku zenji anaendesha kipindi kwenye radio cha kujibu maswali anaitwa musabaha alipoulizwa swali hilo eti akasema "hiyo ni Siri ya Mungu tuache kutaka kujua kila kitu"
Hili ni swali gumu sana kwa waislam
Amin thuma aminUngejikita kwenye hii mada ingekuwa jambo jema sana.
Ngoja nikusaidie. Allah aliyotufunulia na kutujuza ni machache sana kuliko ambayo hajatufunulia hasa katika malipo ya waja wema.
Kwahiyo malipo ya Wanawake wema anayajua Allah, ila wanawake wa peponi watakuwa bora zaidi ya hao mabikra tutakao pewa huko peponi. Mola wetu atujaalie pepo ya juu kabisa.
Kuna muda mnatakiwa muwe mnatumia akili zaidi ya mihemko. Someni,kisha mtafakari muujue ukweli.
Peponi kutakuwa na vipando pia na vinavyosafiri kwa kasi kuliko hivi vya duniani. Pepo itakuwa na madaraja kwa mujibu wa uchamungu wa Mtu. Kuna watakaokuwa pepo ya juu zaidi( Mitume, mashahidi,wachamungu n.k) na wengine watakuwa katk pepo za chini...umbali kati ya pepo moja na nyingine ni safari ya miaka 500Kama mtu hutamiliki gari hapa duniani kaa ukijua akhera hamna magari wala simu yani hamna kitu chochote cha kujifurahisha bali kuna pombe na wanawake
Bongo utakuta mtu anaitwa Mohammed Juma Abdullah anakwambia hana jina la ukoo lenye asili ya kwao, lakini huko Afrika Magharibi waislam wana majina asili kabisa kama NGOLO KANYE, SADIO MANE etc, Bongo tunaona utamadani wa watu ndio ujanja
Wapi sahihi au kipi sahihi tufuate?Islamic wengi ni waganga wa kienyeji,, hujiita wanatoa mashetani kwa njia ya kitabu cha dini yao huku uhalisia ukija kuwa ni matapeli na waganga wa kienyeji...
Wakristo ndio sina la kuongeza,, Wamekuwa wanapelekwa kama bendera..
Note: Dini tu yenyewe ni Mchongo.
Muislamu kwenda kanisani kufuata hiyo miujiza ni sawa tu na mtu wa dini kwenda kwa mganga kwa ajiri ya kutatua shida yake hali ya kuwa bado ana imani na dini yake.Ni kweli watu wanapishana hawa wa imani hii wanaenda kwa waganga wengine wanaenda kwa manabii, yaani ni mchanganyiko wote kuna kitu wanatafuta nje ya imani zao
Waislamu wanaoenda kufanyiwa miujiza kanisani | Nini tatizo?