Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Mzee wang mohamed said..pole na hongera kwa mwezi huu mtukufu...ukipata picha ya mke wa mzee wetu yaan mke wa sykes ..miaka ya karibuni kabla ya umauti ..ilete tafadhali tuione
Escotter,
Wa kwanza kushoto ndiye Mama Daisy, mbele yake ni Bi. Titi Mohamed
na mbele ya Bi. Titi ni Bi Zainab aliyekuwa mke wa Tewa Said Tewa.

 
Aksante. Nimekisoma sana kitabu chako na pia majambo yalipitika nimeyaona ila yale matundu uliyoaacha ndio hayo sie twataka utujuze kwa undani.
 
Aksante. Nimekisoma sana kitabu chako na pia majambo yalipitika nimeyaona ila yale matundu uliyoaacha ndio hayo sie twataka utujuze kwa undani.

Kwezisho,
Kasome Sehemu ya Tatu ya Kitabu.
Maswali yako yote majibu yake yamo mle.
 
Mkuu unavitabu umeandika, ningependa kuvisoma.
 
Mkuu unavitabu umeandika, ningependa kuvisoma.
Menyidyo,
Soma kitabu ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...''
Kinapatikana Ibn Hazm Media Centre Bookshop Msikiti wa Manyemana Mtoro,
Kariakoo bei shs: 10,000.

Kipo pia Soma Bookshop Mikocheni na Novel Idea Slip Way Masaki hapa wana
nakala ya Kizungu, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes...''
 
Aksante. Nimekisoma sana kitabu chako na pia majambo yalipitika nimeyaona ila yale matundu uliyoaacha ndio hayo sie twataka utujuze kwa undani.
Kwezisho,
Nashukuru kuwa umesoma kitabu.
Hayo matundu usemayo mimi siyajui.

Nimejitahidi kutafiti na kuandika kadri ya uwezo wangu.

Mara nyingi hupata maswali ya sampuli yako na mimi
huwa najibu kuwa labda Nyerere angeliandika historia
yake na vipi alikutana na Abdul Sykes tungeweza kupata
mengi.

Lakini kwa bahati mbaya sana Nyerere hakuandika.

Kwa nini hakuandika historia hii muhimu katika maisha yake
hatutoweza kujua kwa uhakika ila tutafanya, ''speculation,'' tu.

Miaka michache iliyopita katika ukumbi huu huu palifumuka
vumbi kubwa niliposema kuwa hotuba ya Nyerere aliyosoma
UNO 1955 ilikuwa imetayarishwa 1950 na jopo la Abdul Sykes,
Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Amir, Stephen
Mhando, Dr.Vedasto, Kyaruzi
na timu nzima ya TAA Political
Subcommitee ambayo Abdul alikuwa katibu wake.

Waliofuatilia mnakasha ule watakumbuka.
Kwa wengi hii ilikuwa habari mpya.

Kuna baadhi walikuwa hawajasikia hata hilo jina la Abdul na
majina mengine niliyotaja kama Sheikh Hassan bin Amir na
Said Chaurembo.

Ilikuwa kama vile nimemtukana Mwalimu Nyerere.

Na kila nilipojaribu kueleza historia ya TANU kama niijuavyo
ndivyo nilivyozidisha ghadhabu za baadhi ya watu.

Sishangai kukuona unahangaika na kuwa katika hali ya kutotosheka
na niliyoandika.

Hauko peke yako katika hili.
Mwalimu wangu Prof. Haroub Othman yeye alikwenda mbali zaidi.

Prof. Haroub alimkabili Mwalimu Nyerere uso kwa macho kutaka
kusikia kutoka kinywani kwake ukweli katika yale niliyoandika.

Je ungependa kujua jibu la Mwalimu Nyerere?
 

Wewe ni mbobezi na mtaalamu wa tafiti za kihistoria, kwa uelewa wangu mdogo historia zote dunia ambazo zinavuma huwa zinataja key figures katika jambo linalosimuliwa. Haiwezekani na haitakaa itokee historia itaje watu wooote kwa uzito Sawa katika events moja. Ulivyosema baada ya kitabu chako cha Abdul Sykes kumeibuka disinterest kwa Nyerere, japo sijakisoma huenda hiyo imeletwa na mtazamo wa mwandishi juu ya hao wawili! Cha msingi historia haiwezi kuwabeba watu wote kwa usawa! hata katika familia watu wakishatutoka hatuwakumbuki kwa uzito unaofanana na hiyo itategemea nani alikuwa nani kabla ya hapo. Mfano mzuri ni Zanzibar, Mzee Karume anatajwa sana kana kwamba yale mapinduzi aliyaandaa peke yake. Lakini ishu sio hiyo, ni kwa sababu miaka yote historia hum-feva kinara wa mwisho (the last key figure not initiators). Wewe waweza kuwa shahidi Kati ya mtu anayetoa wazo la jambo fulani na mtu anayetimiliza hilo wazo, Kati ya hao wawili ni yupi atafahamika zaidi. Hata nyie waandishi waweza pewa wazo zuri la kuandika kitu fulani ambalo hukuwahi kulidhani kama lingekuwa zuri lakini utakapoliandika na likapokelewa vizuri na jamii mtu atakayefahamika zaidi ni wewe uliyaandika hicho kitabu na wala huenda Jamii isimfahamu huyo mtoa wazo. Inawezekana kabisa hiyo ndo sababu ya Nyerere kutajwa zaidi kuliko hao wengine
 

Ni kweli kabisa, hata mimi nilishangaa kusikia hivyo. Nikiri kwamba historia kamili ya wapigania uhuru wa Tanganyika nimekuja kuwafahamu nilipokuwa chuo kikuu chini ya mwl wangu wa HISTORY OF TANZANIA Dr Mkanachi. Waanzilishi wote wa chokochoko za ukombozi na kwamba Nyerere aliingia rasmi TAA 1953 baada ya kutoka masomoni Wingereza nilivijulia huko. Nachotaka kusema, ordinary historians si rahisi kufahamu initiators wa uhuru. Wanawafahamu zaidi key figure ambao walikuja kushika madaraka na hilo si kosa wala dhambi kwani ndo historia ya dunia ilivyo. Historia ya dunia ni tofauti na historia za dini ambazo Waanzilishi ndo waliozieneza kwa sababu mwenyezi Mungu alipanga iwe hivyo.
 
Naam, sheikh napenda sana kujua. Ila bado naufikirisha sana ubongo wangu. Je, yumkini Abdulwahid Sykes aliogopa kilichompata mtu aliyemtaka awe Rais wa TANU Bwana David Kidaha Makwaia? Zote ni speculation ila ni vyema kujua kwa kuwa hizi ni zama za kutaka kujua zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…