Mzee wang mohamed said..pole na hongera kwa mwezi huu mtukufu...ukipata picha ya mke wa mzee wetu yaan mke wa sykes ..miaka ya karibuni kabla ya umauti ..ilete tafadhali tuioneEscotter,
Allahuma Amin.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzee wang mohamed said..pole na hongera kwa mwezi huu mtukufu...ukipata picha ya mke wa mzee wetu yaan mke wa sykes ..miaka ya karibuni kabla ya umauti ..ilete tafadhali tuioneEscotter,
Allahuma Amin.
Escotter,Mzee wang mohamed said..pole na hongera kwa mwezi huu mtukufu...ukipata picha ya mke wa mzee wetu yaan mke wa sykes ..miaka ya karibuni kabla ya umauti ..ilete tafadhali tuione
Aksante. Nimekisoma sana kitabu chako na pia majambo yalipitika nimeyaona ila yale matundu uliyoaacha ndio hayo sie twataka utujuze kwa undani.Kwezisho,
Abdul Sykes hakupata kumsusa Nyerere hata siku moja.
Ikiwa umesoma kitabu changu utakuwa umesahau baadhi
ya vitu na hii ndiyo sababu unahangaishwa na hii ''kususa,''
au ungependa kuwa Abdul awe kasusa.
Mimi tabu mtu kunichokonoa.
Huwa siingii kwenye tundu nabaki mlangoni.
Rejea kwenye kitabu cha Abdul Sykes na soma Sehemu
ya Tatu ya Kitabu.
Uhuru ushapatikana 1961.
Palipitika majambo.
Soma kisha rejea katika mjadala.
Usiandikie mate na wino upo.
Aksante. Nimekisoma sana kitabu chako na pia majambo yalipitika nimeyaona ila yale matundu uliyoaacha ndio hayo sie twataka utujuze kwa undani.
Mkuu unavitabu umeandika, ningependa kuvisoma.![]()
Chief Michael Lukumbuzya wa Ukerewe
Nilikuwa naitafuta picha ya hayati Chief Michael Lukumbuzya kwa miaka mingi bila mafanikio. Sababu ya kuitafuta picha ya Chief Lukumbuzya ni kisa alichonihadithia Bi. Mwamvua biti Masha mke wa marehemu Abdulwahid Sykes maarufu akijuikana kwa jina la mwanae wa kwanza Daisy hivyo tukimuita Mama Daisy.
Nilikuwa kila nikipata fursa ya kuwa na mama yangu Bi. Mwamvua, yaani Mama Daisy nikipenda kumdodosa mambo yalivyokuwa wakati wa ukoloni walipokuwa wanapambana na Muingereza, kwanza kichinichini katika miaka ya mwanzo ya 1950 wakati wa TAA kisha wakipambana na mkoloni dhahiri baada ya kuunda TANU mwaka wa 1954.
Bi. Mwamvua alikuwa wakati mwingine bila kutegemea akiniangushia habari muhimu kupita kiasi. Mfano siku aliponiambia kuwa nafasi ya president wa TANU nafasi ile ilikuwa ya Chief Kidaha Makwaia lakini alikataa ndipo bahati ikamuangukia Julius Nyerere.
![]()
Chief David Kidaha Makwaia
Iko siku akanieleza taharuki iliyotokea nyumbani kwa Abdul Sykes baada ya Nyerere kula chakuka kilichomfanya tumbo limkate na ikadhaniwa kuwa amelishwa sumu.
Mkasa huu ulitokea wakati mama yake Nyerere, Bi. Mugaya Nyangombe yuko na Mama Maria Nyerere vilevile wamekaa uani na akina mama wengine na Abdul Sykes, Nyerere na viongozi wengine wako nyumba kubwa wanapanga mipango ya kupeleka harakati mbele.
Mama yake Nyerere alianza kulia akiamini kabisa kuwa mwanae katiliwa sumu katika chakula. Mama Daisy alikuwa na habari nyingi sana za nyakati zile. Historia ya TANU kama zilivyo nyaraka na picha zake nyingi zimo mikononi mwa watu.
Mfano mwingine ni wa mkutano wa kwanza wa Wanawake wa TANU uliokuwa ukifanyika Arnautoglo Hall na yeye alikuwa yuko nyumbani anafanya shughuli zake. Anasema, ‘’Aliporudi nyumbani Bwana Abdul kanikuta nimekaa, akaniuliza wewe hukwenda mkutanoni? Wenzako wote wako Arnautoglo…’’ Bi. Mwamvua anasema hapo hapo akachukua baibui lake na kuelekea mkutanoni.
Wasemaji wakuu walikuwa Bi. Titi Mohamed na Bi. Tatu biti Mzee. Huu ndiyo mkutano wa kwanza wa wanawake wa TANU.
![]()
Kushoto Mama Daisy na mbele yake ni Bi. Titi Mohamed
na Bi. Zainab mke wa Tewa Said Tewa
Katika mazungumzo kama haya ndipo siku moja akanihadithia habari za Chief Luumbuzya. Anasema walitoka Dar es Salaam yeye mumewe kwenda Nansio, Ukerewe kumtembelea Hamza Mwapachu.
Anasema walipanda meli Mwanza pamoja na Chief Lukumbuzya kuelekea Nansio. Lukumbuzya alikuwa anatokea Makerere Uganda alipokuwa anasoma anarudi nyumbani likizo. Abdul Sykes na Michael Lukumbuzya hawakuwa wanajuana.
Hamza Mwapachu alikuwa amekusanya wananchi na kikundi cha ngoma kuja kumpokea bandarini Nansio President wa TAA Abdulwahid Sykes. Lukumbuzya alishangazwa kukuta sherehe bandarini akifanyiwa mtu ambae yeye hakuwa anamjua na akiuliza anaambiwa ni mgeni kutoka Dar es Salaam.
Lukumbuzya alipigwa na butwaa kuona mapokezi ya watu wake wa Ukerewe wakiwa katika nderemo wakati yeye chief hakuna hata mtu alikuwa anajua kuwa yumo katika meli ile ile. Baadae Hamza Mwapachu alimfahamisha yule mgeni waliokuja kumpokea pale alikuwa nani katika siasa za Tanganyika.
![]()
Hamza Kibwana Mwapachu
Simulizi kama hizi zilinifikirisha sana katika kutaka kuwajua wazalendo wa wakati ule. Hamza Mwapachu alikuwa anafanya haya ya kukusanya wananchi kumpokea kiongozi wa Waafrika chini ya pua za Waingereza bila kujali nini kitampata licha ya kuwa yeye kupewa uhamisho kupelekwa kisiwani Ukerewe peke yake ilikuwa ni adhabu, kwa hakika ni kifungo khasa cha kumtia kuzuizini asiweze kuenedeleza mipango yake ya kuunda chama cha siasa.
Uhuru ulipopatikana Chief Michael Lukumbuzya alipelekwa nje ambako alikuwa balozi na mwisho akawa balozi Canada ambako huko ndiko umauti ulikomfika.
![]()
Abdulwahid Sykes
Menyidyo,Mkuu unavitabu umeandika, ningependa kuvisoma.
Ahsante sanaEscotter,
Wa kwanza kushoto ndiye Mama Daisy, mbele yake ni Bi. Titi Mohamed
na mbele ya Bi. Titi ni Bi Zainab aliyekuwa mke wa Tewa Said Tewa.
![]()
Kwezisho,Aksante. Nimekisoma sana kitabu chako na pia majambo yalipitika nimeyaona ila yale matundu uliyoaacha ndio hayo sie twataka utujuze kwa undani.
Kwezisho,
Nasikitika kukufahamisha kuwa baada ya mimi kuandika
kitabu cha Abdul Sykes kumeingia ''disinterest'' kwa hii
historia ya Nyerere kwetu sote.
Nyerere amekuwa sasa si muhimu tena baada ya ukweli
kujulikana katika historia ya AA, TAA na TANU.
Na nadhani baada ya Abdul na Ally Sykes kupewa nishani
katika kumbukumbu ya miaka 50 wa uhuru wa Tanganyika
kutambua mchango wao katika kupambana wa ukoloni sasa
hakuna tena jipya.
Imekuwa kama vile katika ''show,'' pazia limeshushwa.
Na yule mzee nani yule wa pale Gerezani, naye yupo?Onyx,
Baada ya uhuru Nyerere alimtia Chief Kidaha kizuizini Tunduru
chini ya Dentition Act of 1962.
Tupe jibu la mwalimu Nyerere
Kwezisho,
Nashukuru kuwa umesoma kitabu.
Hayo matundu usemayo mimi siyajui.
Nimejitahidi kutafiti na kuandika kadri ya uwezo wangu.
Mara nyingi hupata maswali ya sampuli yako na mimi
huwa najibu kuwa labda Nyerere angeliandika historia
yake na vipi alikutana na Abdul Sykes tungeweza kupata
mengi.
Lakini kwa bahati mbaya sana Nyerere hakuandika.
Kwa nini hakuandika historia hii muhimu katika maisha yake
hatutoweza kujua kwa uhakika ila tutafanya, ''speculation,'' tu.
Miaka michache iliyopita katika ukumbi huu huu palifumuka
vumbi kubwa niliposema kuwa hotuba ya Nyerere aliyosoma
UNO 1955 ilikuwa imetayarishwa 1950 na jopo la Abdul Sykes,
Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Amir, Stephen
Mhando, Dr.Vedasto, Kyaruzi na timu nzima ya TAA Political
Subcommitee ambayo Abdul alikuwa katibu wake.
Waliofuatilia mnakasha ule watakumbuka.
Kwa wengi hii ilikuwa habari mpya.
Kuna baadhi walikuwa hawajasikia hata hilo jina la Abdul na
majina mengine niliyotaja kama Sheikh Hassan bin Amir na
Said Chaurembo.
Ilikuwa kama vile nimemtukana Mwalimu Nyerere.
Na kila nilipojaribu kueleza historia ya TANU kama niijuavyo
ndivyo nilivyozidisha ghadhabu za baadhi ya watu.
Sishangai kukuona unahangaika na kuwa katika hali ya kutotosheka
na niliyoandika.
Hauko peke yako katika hili.
Mwalimu wangu Prof. Haroub Othman yeye alikwenda mbali zaidi.
Prof. Haroub alimkabili Mwalimu Nyerere uso kwa macho kutaka
kusikia kutoka kinywani kwake ukweli katika yale niliyoandika.
Je ungependa kujua jibu la Mwalimu Nyerere?
Naam, sheikh napenda sana kujua. Ila bado naufikirisha sana ubongo wangu. Je, yumkini Abdulwahid Sykes aliogopa kilichompata mtu aliyemtaka awe Rais wa TANU Bwana David Kidaha Makwaia? Zote ni speculation ila ni vyema kujua kwa kuwa hizi ni zama za kutaka kujua zaidi.Kwezisho,