Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

UncleE="Uncle Jei Jei, post: 16461586, member: 34691"]Wewe ni mbobezi na mtaalamu wa tafiti za kihistoria, kwa uelewa wangu mdogo historia zote dunia ambazo zinavuma huwa zinataja key figures katika jambo linalosimuliwa. Haiwezekani na haitakaa itokee historia itaje watu wooote kwa uzito Sawa katika events moja. Ulivyosema baada ya kitabu chako cha Abdul Sykes kumeibuka disinterest kwa Nyerere, japo sijakisoma huenda hiyo imeletwa na mtazamo wa mwandishi juu ya hao wawili! Cha msingi historia haiwezi kuwabeba watu wote kwa usawa! hata katika familia watu wakishatutoka hatuwakumbuki kwa uzito unaofanana na hiyo itategemea nani alikuwa nani kabla ya hapo. Mfano mzuri ni Zanzibar, Mzee Karume anatajwa sana kana kwamba yale mapinduzi aliyaandaa peke yake. Lakini ishu sio hiyo, ni kwa sababu miaka yote historia hum-feva kinara wa mwisho (the last key figure not initiators). Wewe waweza kuwa shahidi Kati ya mtu anayetoa wazo la jambo fulani na mtu anayetimiliza hilo wazo, Kati ya hao wawili ni yupi atafahamika zaidi. Hata nyie waandishi waweza pewa wazo zuri la kuandika kitu fulani ambalo hukuwahi kulidhani kama lingekuwa zuri lakini utakapoliandika na likapokelewa vizuri na jamii mtu atakayefahamika zaidi ni wewe uliyaandika hicho kitabu na wala huenda Jamii isimfahamu huyo mtoa wazo. Inawezekana kabisa hiyo ndo sababu ya Nyerere kutajwa zaidi kuliko hao wengine[/QUOTE]
Uncle,
Nakushauri usome kitabu kwanza kabla hujatoa uamuzi katika historia hii.

Ningeweza kusema mengi lakini sipendi kuathir fikra yako nataka uwe huru
uje utueleze ulichoona.
 
Kwezisho,
Shida inayokupata wewe nadhani ni kuwa hii historia ni ngeni kwako.

Abdul
hakuwa mtu wa kutishwa na Nyerere si wakati wa kudai uhuru
wala wakati uhuru ushapatikana.

Ukweli wa historia ya TANU ushajulikana na ndiyo maana nikakueleza
kuwa kwetu sisi hii historia ishafika mwisho.

Tatizo lilikuwa pale ambapo tulikuwa kimya.

Lakini baada ya kuieleza dunia historia ya kweli ya TANU kisa hiki sasa
kimefika mwisho.
 
hilo baibui alilovaa bi mwamvua(mama daisy) liko wapi hapo pichani?

"anasema hapo hapo akachukua baibui lake na kuelekea mkutanoni"
Mtanganyika...
Unachanganya matokeo mawili tofauti.

Suala la baibui ni 1955 wakati wa kuunda Umoja wa Wanawake wa TANU.
Siku hizo hata Bi. Titi alikuwa anapanda kuhutubia kavaa baibui.

Baadae mabaibui yaliwekwa pembeni.
Hiyo picha nilolweka hapo ni maandamano ya TANU baada ya uhuru.
 
Sheikh Mohamed, mimi sio mgeni wa historia na ni mfuatiliaji mzuri wa mabandiko yako pamoja na vipindi vya TV ila kinachonitatiza ni ushiriki wa familia ya Abdulwahid Sykes baada ya kuikomboa Tanganyika. Na hapo juu umegusia kwamba Abdul hakuwa mtu wa kutishwa na Nyerere si wakati wa kudai Uhuru au baada.
Ila kwa ufahamu wangu mdogo hili suala kama ulivyoelekeza ni suala linaloonesha bado kuna jambo au mambo hayapo wazi ingawa kwenye kitabu chako umegusia kuna mambo yalipitika, tunahitaji kujiuliza na kujua kwa nini ushiriki wa hii familia baada ya ukombozi.
Hebu tuwaombe wenye ufahamu kama Mzee wetu Mohamed Said watujuze.
 
Kwezisho,
Uamuzi ni wako.

Elimu haina mwisho ikiwa wako watakaojazia pale nilipoacha mie hiyo
ni kheri.
 
Tupe jibu la mwalimu Nyerere
Onyx,
Mwaka wa 1974 Ali Muhsin Barwani alifunguliwa kutoka jela za Bara ambako
Nyerere alimfunga kwa miaka 10 baada ya serikali ya Zanzibar kupinduliwa
mwaka wa 1964.

Hakupita muda Ali Muhsin alitoroka kwa kuvuka mpaka wa Horohoro kwa njia za
panya kwa miguu usiku wa manane akisaidiwa na wasamaria wema na hivyo
kuweza kufika Mombasa kisha Nairobi na kupata msaada wa UNHCR waliomsaidia
kufika Cairo kuungana na familia yake.

Ali Muhsin alitoroka Tanzania mwezi Mtukufu wa Ramadhani kama huu.
Mwaka wa 1997 aliandika kitabu, ''Conflicts and Harmony in Zanzibar.''

Unaweza kumjua Ali Muhsin kwa kuingia hapo chini:
Mohamed Said: KUTOKA JF: KUMBUKUMBU ZA ALI MUHSIN BARWANI: ''CONFLICTS AND HARMONY IN ZANZIBAR''
Mohamed Said: TUJIKUMBUSHE: SHEIKH ALI MUHSIN BARWANI MMOJA WA WAPIGANIA UHURU WA ZANZIBAR
Mohamed Said: MAISHA YA SIASA YA SHEIKH ALI MUHSIN BARWANI (1919 - 2006) - KUMBUKUMBU YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR


Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa U Thant akisalimiana na
Waziri Mkuu wa Zanzibar Mohamed Shamte na Waziri wa
Mambo ya Nchi za Nje Ali Muhsin Barwani mwaka wa 1963
New York


Katika kitabu chake hicho Ali Muhsin alimueleza Nyerere kwa namna
ambayo haikuwahi kufanywa kabla.

Kitabu hiki kilipigwa marufuku kimya kimya kuingia Zanzibar lakini photo
copy ya kitabu iliweza kupenyezwa na kuwafikia baadhi ya watu.

Kila aliyekisoma alipata mshtuko wa aina yake na mmoja wa wasomaji
wa kitabu hiki alikuwa Prof. Haroub Othman.

Mara tu baada ya kutoka kitabu cha Ali Muhsin ndipo kikatoka kitabu
cha Abdul Sykes mwaka wa 1998.

Kama ilivyokuwa kwa kitabu cha Ali Muhsin, kitabu hiki nacho kilikuja
na mengine ambayo yalionekana kuwataabisha baadhi ya watu na
mmoja katika hao waliotaabika alikuwa Prof. Haroub Othman.

Hakuweza kustahamili ndipo alipofunga safari hadi nyumbani kwa
Mwalimu Nyerere na kumuomba akijibu kitabu cha Ali Muhsin
Barwani
na kitabu cha Mohamed Said kwani vikiachiwa bila majibu
vitaharibu ''legacy'' yake.

Mwalimu Nyerere alikuwa kasoma vitabu vyote viwili na jibu alilompa
Prof. Haroub ni kuwa yeye Haroub atengeneze kamati na yeye atakuja
kueleza yote ili wao waandike historia yake.

Kamati ilitengenezwa lakini hakuna kilichofanyika hadi Mwalimu Nyerere
alipofariki dunia mwaka 1999.

Kitabu cha Ali Muhsin Barwani kinapatikana Tanzania Publishing House,
Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Mtoro na Manyema na Elite Bookshop
Mbezi Samaki na Soma Bookshop Mikocheni kwa bei ya shs: 10,000 hadi
shs 13,000.
 
Uncle...
Kusema kuwa ati historia inayojulikana ni ya walioshika madaraka
hiyo si kweli na hakuna ushahidi wa kisomi wa hiyo dhana yako.

Historia haijali haiba ya mtu labda iwe ''official history.''
Historia itaeleza yale yaliyotokea na waliohusika.

Kwa historia hii tunayoijadili hapa hiyo iliyoandikwa na watafiti wetu
historia hii ni ''official history,'' watafiti walielekezwa kipi cha kuandika
na kipi cha kuacha.

Fanya utafiti kidogo tu uangalie ni watu gani walifutwa katika historia
ya uhuru wa Tangnayika na jiulize ni kwa sababu gani?

Nimeeeleza haya kwa urefu na mapana katika kitabu cha Abdul Sykes.
Iweje mtu avishwe kilemba na joho si lake na asione vibaya?

Hebu ingia hapa:
Mohamed Said: UPINZANI DHIDI YA HISTORIA YA KWELI YA TANU NA UHURU WA TANGANYIKA 4



Dr. Khamisi Mkanachi na mimi Dodoma
 
Ahsante mzee wangu mohammed said siku zote huwa sichok kusoma maandish yko maana najifunza mungu akupe afya njema na akulipe kla la kheir inshaallah
 

Reading between lines, dhamira yako ya kumdharaulisha Nyerere bado inaendelea.
Nyerere "alimtiaje" ndani chief David Kidaha?
Je ni sahihi kuandika historia ya sasa kuhusu Sheik Ponda kuwa alipigwa risasi na Kikwete, kwa vile tu tukio lilitokea wakati utawala wa Kikwete?
 
Ahsante kwa historia nzuri ya Taifa letu Ndugu Mohamed Said.u
Ningelipenda kujua ktkt harakati za uhuru upande kina mama kama una habari yeyote ya Chiku bint Said Kisusa wa New Street enzi hizo ambaye alikuwa mke wa Sharif Said Al attas (ulishawahi mtaja kwenye simulizi zako) .
 
Kambaresharubu,
Bahati mbaya sina taarifa za bi. mkubwa huyu.
 
Nanren,
Thomas Molon
ameandika kitabu: ''Nyerere The Early Years.''

Ameeleza sintofahamu iliyokuwapo kati ya Chief Kidaha na
Nyerere iliyodumu kwa miaka mingi.

Naamini Molon hakuwa na nia ya kumdhalilisha Nyerere kwa
kueleza ugomvi ule.
 
Onyx,
Mwaka wa 1974 Ali Muhsin Barwani alifunguliwa kutoka jela za Bara ambako
Nyerere alimfunga kwa miaka 10 baada ya serikali ya Zanzibar kupinduliwa
mwaka wa 1964.
Mkuu Maalim
Mohamed Saidasante kwa taarifa, kutujulisha kumbe enzi zile ni Nyerere ndio alikuwa anatia watu jela na kuwafunga tuu!, ila haikusemwa watu hao waliofungwa na Nyerere, walikuwa wanafunguliwa na nani kutoka vifungo hivyo vya Nyerere?!. Mimi nilidhani ungesema ni serikali ya Nyerere!, kumbe ni Nyerere!, asante!.

Kwa msio jua kilichotokea Zanzibar baada ya mapinduzi yale matukufu ya 1964, wapinzani wa Karume walikuwa wana vanish into thin air, hata unywele haukuonekana (taarrifa zisizothibitishwa zilisema walininginizwa majiwe shingoni, kutiwa ndani ya magunia na kutoswa baharini). Kufuatia Mwalimu Nyerere kuwa ni mcha Mungu, hakuridhishwa na kinachoendelea kule, hivyo ili kuwanusuru waliotofautiana na Karume, aliwachukua na kuwafunga huku bara ambayo hiyo ndio salama yao!, hivyo ndivyo Nyerere alivyowanusu wengi akiwemo Col. Mafudha, Abrahman Mohamed Babu na baadhi ya Makomredi, vinginevyo saa hizi, tungekuwa tunazungumza mengine!.

Kiukweli shukrani ya punda ni mateke!, asingekuwa Nyerere na Muungano, baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, sijui ingelikuwaje kwa race fulani kule Zanzibar, halocust ingekuwa ni afadhali maana angalau ulipatikana japo mfupa au hata majivu!, Zanzibar hata unyayo tuu ulipokanya mara ya mwisho,usingeonekana, sii unywele wala ukucha!. Badala ya kushukuru ndio kwanza watu humu wanabeza!.

Kwa amsiomjua Nyerere, japo nchi yetu ina adhabu ya kifo, katika utawala wake wa miaka 23, alisaini hati moja tuu ya kunyongwa kwa Mwamwindi!. Aliyefuatia ni swala tano!, uliza alisaini hati ngapi na watu wakanyongwa!.

Vitu vingine bora tuacheni tuu!, harakati za kumtangaza Nyerere ni Mwenye Heri, zinaendelea!.

Pasco
 
Ahsante MZEE Mohamed
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…