Mkuu Maalim
Mohamed Said, kwanza nakiri sina nijuacho, na sio zaizi yako, na hata hayo Mapinduzi Matukufu nimeyajua kwa kusoma tuu na kuhadithiwa!.
Sipambani na wewe bali tunatofautiana tuu kwa mmoja wetu kuwalisha watu urongo humu, na baadhi yetu kukataa kuumeza urongo huo !.
Dini zumetufunzwa kuwa na shukani katika madogo ili tuweze kupewa makubwa!, ni Nyerere ndiye aliyetupatia uhuru, kwa hili pekee hana budi kuenziwa na kushukuiwa daima!. Wengine hatuna uvumilivu wa kuona licha ya kutangulia mbele ya haki, kila uchao, unakuja humu na posti zako za udini ulikubuhu mtu kisha kumbeza!.
Kama mtu amehukumiwa kifo kwa upanga, na sheria ya upanga ule ni kupigwa kwa pigo moja tuu!, inapotokea yule mkata upanga akakuepushia kifo na badala ya kukata shingo, upanga ukashukia kwenye mkono na kukata mkono hivyo kuepuka kifo, mtu aliyesalimika kifo, atamshukuru mchinjaji kwa kumuepushia kifo badala ya kumlaani kwa kumkata mkono!.
Hao walionusuishwa kifo na Nyerere huko walipo wanamshukuru Nyerere, who are you kumbeza kila uchao?!.
Mimi japo sii mwanazuoni na sii mwandishi kuyaandika yote niliyoyasikia, lakini nimezungumza na Sheikh Mkuu Hemed Bin Jumaa Bin Hemed, Sheikh Kassim Bin Juma, Sheikh Nurdin, Sheikh Yahya Hussein, Sheikh Comorean, Sheikh Jabir, Omar Matata na wengine wengi, misimamo yao naijua na shukrani zao kwa Nyerere nazijua huku waliko wanakusoma na kukushangaa jinsi unavyombeza humu!.
Maadam wewe wasema ''Mimi si saizi yako, ukinivaa utapwaya", kiukweli nimekuvaa na nimepwaya and here I rest my case!, endelea kulisha watu urongo, wa kumeza watameza, wa kutema watatema hadi watakapotokea saizi yako ndio labda watatunusuru na urongo wenye kupandikiza mbegu za chuki za udini kwa kisingizio cha kuhifadhi historia!
Asante.
Pasco