Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Haaa haaa Sheckh Mohamed Said Mapinduzi matukufu hayapaswi kuzodolewa kwa namna yoyote.Ukimwona mtu anayakosoa Mapinduzi matukufu basi lazima atakuwa na vimelea vya kikoloni.
 
Haaa haaa Sheckh Mohamed Said Mapinduzi matukufu hayapaswi kuzodolewa kwa namna yoyote.Ukimwona mtu anayakosoa Mapinduzi matukufu basi lazima atakuwa na vimelea vya kikoloni.
Wala siajabu ww kuandika haya kama prof LIPUMBA anafanya viroja itakuwa ww.
Huu ndio umaskini tulionao waafrika wengi tu bila kujali elimu zetu au kipato chetu.
 
Mohamed Said
Kuna mambo kadha wa kadha umeyaongelea, ningependa unisaidie kufahamu

1. Kwavile umesema Pasco hajui kitu kuhusu 'mapinduzi matukufu' leo unawaambia nini wazanzibar wanaosherehekea mapinduzi hayo kila January 12 ya kila mwaka?

2. Je, bado unasimama na kauli yako kuwa hujamdharau au kumdhalilisha Nyerere?

3. 'Umhumi wa nyerere haupo tena' sisi kama Taifa tunawezaje kuandika historia ya nchi hii bila kumtaja Mwalimu?

4.Ni nani aliyeandika katiba ya kwanza ya chama cha siasa Tanganyika?

5. Na kwavile umuhimu wa Nyerere haupo, umuhimu upo wapi na kwa nani sasa hivi?

Ningependa tujadiliane katika muktadha huu, na siyo nukuu za vitabu

Nitashukuru ukinisadia kama nukta zilivyo hapo juu na si kuchanganya mambo katika kapu moja

Ahsante
Nguruvi3,
Kuhusu kusherehekea mapinduzi Wazanzibar wenyewe wananasihana
kuwa kuna mauaji yalifanyika katika mapinduzi haifai kusherehekea
kwani ni kinyume na mafunzo ya Uislam.

Nasaha zangu kwao ni hizo kuwa wamuogope Allah kwani yaliyopitika
ni ya kujutia.

Hakika nasimama katika kauli yangu kuwa sijamdharau na kumdhalilisha
Mwalimu Nyerere.

Ningeweza kuishia hapo lakini nitaongeza maneno ili nifahamike.

Nilichotofautiana na wanahistoria wengi na huu ndiyo ulikuwa msimamo
wa CCM katika historia ya TANU ni kuwa Mwalimu Nyerere ndiye aliyeunda
TANU 1954 (Angalia: Historia ya TANU, Chuo Cha Kivukoni, 1981).

Hapa ndipo tulipokhitilafiana mimi nikenda nyuma ya Nyerere nikaanza na
mwamko wa Waafrika kuanzia miaka ya 1929 na kw akutumia Nyaraka za
Sykes nikaeleza vipi siasa zilianza hadi kufikia 1950 walipoingia vijana kutoka
Chuo Kikuu Cha Makerere khasa waliokuwa Dar es Salaam wakishirikiana na
Sykes brothers Abdul na Ally Sykes walivyoleta mabadiliko ndani ya TAA.

Historia hii sasa inafahamika sina haja ya kuirudia kwa kirefu.

Hili la umuhimu wa Nyerere nilisema hivyo kwa muktadha wa mimi kuendelea
kutafiti katika historia ya TANU na harakati za kudai uhuru.

Umuhimu wa Mwalimu Nyerere kwangu mimi katika historia ya TANU na ya
kudai uhuru...

Maana yangu ni kuwa kwangu mimi nimeshasahihisha kile kilichokosewa kwa
wanahistoria kudhani kuwa kabla ya Nyerere hapakuwa na kitu.

Inawezekana wengine waliandika hivyo kwa kutokujua na wengine labda kwa
kuelekezwa na wengine kwa kujipendekeza (Angalia: HAK Mwenegoha (1976),
John Illiffe, Edward Barongo, Saadan Abdu Kandoro, Kirilo na Seaton
na Chuo Cha Kivukoni).

Mtafiti yoyote yule akiwasoma waandishi hawa walioandika historia ya TANU
watapata mshtuko mkubwa sana watakapokuja kusoma kitabu cha Abdul
Sykes
.

Baada ya kuandika historia ya TANU kama nilivyoelezwa na wazee wangu na
kuona nyaraka za wakati ule kuyakinisha niliyoelezwa kile kitendawili cha kuwa
kaja Nyerere Dar es Salaam 1952 kawa na ofisi, kawa na fedha za kuendesha
chama, kama na watu wa kumuunga mkono yote akiyafanya peke yake, kikawa
nimekitegua.

Sasa umuhimu wa mimi kuendelea na utafiti wa Mwalimu Nyerere na historia
ya TANU ndiyo sasa haupo tena.

Kama vile isivyowezekana kuandika historia ya TANU bila ya kumtaja Abdul
Sykes
kwa kutaja jina moja tu kwani yako mengi ndivyo hivyo hivyo
isivyowezekana kuandika histora ya TANUbila ya kumtaja Mwalimu Nyerere.

Nina yakini nimeeleweka.

Katiba ya kwanza ikiwa unakusudia ile aliyopendekeza Gavana Edward Francis
Twining,
waliyoiandika ni TAA Political Subcommittee na wajumbe wake ni hawa:
Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Abdulwahid Sykes, Hamza Mwapachu,
Dr.Vedasto Kyaruzi, Said Chaurembo
na John Rupia.

Hii ilikuwa mwaka wa 1950.

Swali la mwisho sina la kusema kwa kuwa nitakuwa nawasemea watafiti wengine.

Umuhimu wa Mwalimu Nyerere katika historia ya TANU umekoma kwangu kwa
sababu nimekamilisha nililokusudia.

Watafiti wengine wanaendelea (Angalia: Morton 2014).

Mwisho ningependa kusema kuwa umenipa sharti kuwa ''nisichanganye mambo''
kwenye kapu moja na ''nisitumie vitabu.''

Sijui vipi unaweza kufanya mjadala wa kisomi nje ya vitabu.

Ikiwa utaona nimeweka rejea za vitabu niwie radhi hali kadhalika ikiwa utaona
pia nimeweka yote katika kapu moja.
 
Haaa haaa Sheckh Mohamed Said Mapinduzi matukufu hayapaswi kuzodolewa kwa namna yoyote.Ukimwona mtu anayakosoa Mapinduzi matukufu basi lazima atakuwa na vimelea vya kikoloni.
Ngongo,
Hakuna kazi ya mikono ya binadamu itakayokamilika.
Makosa yatakuwapo na ndiyo katika makosa haya leo tunajadili.

Hii ni mada ya kujitegemea ikiwa unataka tujadili fungua uzi na
In Shaallah nitakuitika tuyajadili mapinduzi.
 
Bigirita,
Katika uandishi unapotumia ''dots,'' sheria ni kuwa ziwe tatu tu ...

Mhariri wa kitabu cha Abdul Sykes Bi Mkubwa mmoja wa Kiingereza
alipomaliza kuhariri kitabu alinitumia, ''note,'' akasema ''Mohamed you
are a brilliant story teller I enjoyed your book...''

Unatunga na hadithi za watoto au za Nyerere tu?
 
Unatunga na hadithi za watoto au za Nyerere tu?
Mwana Mtoka...
Ikiwa unakusudia ile ''note,'' ya yule bibi wa Kiingereza prof. wa historia,
maana ya kusema ''story teller,'' si kuwa anamaananisha, ''mpiga hadith.''

Kwa lugha ya Kiingereza huo ni msemo kuwa naandika msomaji anasoma
anasisimkwa kama vile anasoma hadith na wala si kazi ya kisomi.

Kwa kawaida kazi za kisomi zinakuwa ''drab'' na wakati mwingine, ''boring.''
Bibi yule alikuwa anasifia, ''style,'' yangu ya uandishi.
 
Onyx,
Baada ya uhuru Nyerere alimtia Chief Kidaha kizuizini Tunduru
chini ya Dentition Act of 1962.

Chief Kidaha alipoachiwa akahamia Kenya.

Kwa habari zaidi ingia:
Mohamed Said: CHIEF DAVID KIDAHA MAKWAIA
Mohamed Said: Chief David Kidaha Makwaia 1922 - 2007
kwanini Nyerere aliamua kuwasurubu kama sio kuwa timu wenzie waliokuwa nae bega kwa bega katika harakati za uhuru,alafu kwa story nyingi nazozipata hata kutoka kwa watu wafamilia waliokuwepo wakati huo nikuwa wakati huo wenzie walimpendekeza mwali japo wengi walikuwa na ushawishi mkubwa kwa wanachama na jamii mfano Sykes na hata chief Kidaha..!!Sana huwa na umizwa na story ya Kambona na Nyerere
 
Naamini waweza nisaidie kupata historia yake, nilishawahi pata dondoo kuwa vile vile Bi mkubwa huyu ndiye mama wa Mwl. Sakina na Mwl. Fatna Mohamed Arab na ni Dada wa Marehemu Mzee Mrisho Khamis mmiliki wa ile nyumba ilipokuwa Saigon Club zamani Narung"ombe/Sikukuu.
Kamba...
Sina taarifa za huyu bibi katika siasa.
 
kwanini Nyerere aliamua kuwasurubu kama sio kuwa timu wenzie waliokuwa nae bega kwa bega katika harakati za uhuru,alafu kwa story nyingi nazozipata hata kutoka kwa watu wafamilia waliokuwepo wakati huo nikuwa wakati huo wenzie walimpendekeza mwali japo wengi walikuwa na ushawishi mkubwa kwa wanachama na jamii mfano Sykes na hata chief Kidaha..!!Sana huwa na umizwa na story ya Kambona na Nyerere
Ingema,
Historia hii si ya kusulubu wala kutimuana ikiwa kulikuwapo.
Mimi nimeandika historia ya TANU.
 
Ingema,
Historia hii si ya kusulubu wala kutimuana ikiwa kulikuwapo.
Mimi nimeandika historia ya TANU.
niliulizwa swali ambalo linaendana na hiyo historia ya chama mama TANU,na kwanini hatupendi kueleza mapungufu yetu tulipo kosea kama wnzetu wanavyofanya?anyway niko nje ya mada
 
CtOKRwRzrB5mBzQ5Cb9hS_jD8pN0sOFV1B9UckVYU8i70_Q_XEgdcQvlLqtXwNIGW3VWYaLF4a3otlgbC7K9Em0h3Ei39ed7tspSVQ5gtgrZL5rX2su_TqGlyreZorkWRdRYWBJm9Hn-QodC4i5vw06b46UkgySmTNjczP8cj6bmXb4RA6T3qSC_BRU6IEc8Uk75bpciUYbt_YdFaT-dh7hXKdN7cAdD9DHdB4xKJnFGYL4kk1Re5KOjQb6dQbt6-W2QvuYpX7q_3wE2ayyasqEFYWkowgSSkAVFoSq7jL6StW7uicmeAbddSAD_lW0f1GKpvu4xqI9a4PI-bYpm_24kxvl6H8PB1jGH53J9kAbmKXXFPW9YH4qAATIs8DSUScqrg8cJFiy35i4w8jl_JY9uTugl2Aw44difR64FY7bDSEaxEnvJoAwt7M-fxGIG15Umq6XOPqn2rzgSW-lp0fZFNQw9Psx1PGIaIrPRkMAm9PszJcCMiwBkZ9tPSxmQbYeMWxj0yL1lzzPXdNCcTFcoGpAmatJ1uOku2ZCcVz5Si6WIiO58WJjxk8cC3pX-kibj3Y1fBK5co9QGLfLHjSh0zHTOmAOH=w579-h657-no

Chief Michael Lukumbuzya wa Ukerewe​

Nilikuwa naitafuta picha ya hayati Chief Michael Lukumbuzya kwa miaka mingi bila mafanikio. Sababu ya kuitafuta picha ya Chief Lukumbuzya ni kisa alichonihadithia Bi. Mwamvua biti Masha mke wa marehemu Abdulwahid Sykes maarufu akijuikana kwa jina la mwanae wa kwanza Daisy hivyo tukimuita Mama Daisy.

Nilikuwa kila nikipata fursa ya kuwa na mama yangu Bi. Mwamvua, yaani Mama Daisy nikipenda kumdodosa mambo yalivyokuwa wakati wa ukoloni walipokuwa wanapambana na Muingereza, kwanza kichinichini katika miaka ya mwanzo ya 1950 wakati wa TAA kisha wakipambana na mkoloni dhahiri baada ya kuunda TANU mwaka wa 1954.

Bi. Mwamvua
alikuwa wakati mwingine bila kutegemea akiniangushia habari muhimu kupita kiasi. Mfano siku aliponiambia kuwa nafasi ya president wa TANU nafasi ile ilikuwa ya Chief Kidaha Makwaia lakini alikataa ndipo bahati ikamuangukia Julius Nyerere.

IMG-20160406-WA0111%2B%25281%2529.jpg

Chief David Kidaha Makwaia​

Iko siku akanieleza taharuki iliyotokea nyumbani kwa Abdul Sykes baada ya Nyerere kula chakuka kilichomfanya tumbo limkate na ikadhaniwa kuwa amelishwa sumu.

Mkasa huu ulitokea wakati mama yake Nyerere, Bi. Mugaya Nyangombe yuko na Mama Maria Nyerere vilevile wamekaa uani na akina mama wengine na Abdul Sykes, Nyerere na viongozi wengine wako nyumba kubwa wanapanga mipango ya kupeleka harakati mbele.

Mama yake Nyerere alianza kulia akiamini kabisa kuwa mwanae katiliwa sumu katika chakula. Mama Daisy alikuwa na habari nyingi sana za nyakati zile. Historia ya TANU kama zilivyo nyaraka na picha zake nyingi zimo mikononi mwa watu.

Mfano mwingine ni wa mkutano wa kwanza wa Wanawake wa TANU uliokuwa ukifanyika Arnautoglo Hall na yeye alikuwa yuko nyumbani anafanya shughuli zake. Anasema, ‘’Aliporudi nyumbani Bwana Abdul kanikuta nimekaa, akaniuliza wewe hukwenda mkutanoni? Wenzako wote wako Arnautoglo…’’ Bi. Mwamvua anasema hapo hapo akachukua baibui lake na kuelekea mkutanoni.

Wasemaji wakuu walikuwa Bi. Titi Mohamed na Bi. Tatu biti Mzee. Huu ndiyo mkutano wa kwanza wa wanawake wa TANU.

toW0HLKw0_eZRKHUURD38LIxZWcW5RXD7goNoYJWFVWEj8kMEyL1bPXqHWB5CmfrXmD1mA=w329-h566-no

Kushoto Mama Daisy na mbele yake ni Bi. Titi Mohamed
na Bi. Zainab mke wa Tewa Said Tewa

Katika mazungumzo kama haya ndipo siku moja akanihadithia habari za Chief Luumbuzya. Anasema walitoka Dar es Salaam yeye mumewe kwenda Nansio, Ukerewe kumtembelea Hamza Mwapachu.

Anasema walipanda meli Mwanza pamoja na Chief Lukumbuzya kuelekea Nansio. Lukumbuzya alikuwa anatokea Makerere Uganda alipokuwa anasoma anarudi nyumbani likizo. Abdul Sykes na Michael Lukumbuzya hawakuwa wanajuana.

Hamza Mwapachu alikuwa amekusanya wananchi na kikundi cha ngoma kuja kumpokea bandarini Nansio President wa TAA Abdulwahid Sykes. Lukumbuzya alishangazwa kukuta sherehe bandarini akifanyiwa mtu ambae yeye hakuwa anamjua na akiuliza anaambiwa ni mgeni kutoka Dar es Salaam.

Lukumbuzya alipigwa na butwaa kuona mapokezi ya watu wake wa Ukerewe wakiwa katika nderemo wakati yeye chief hakuna hata mtu alikuwa anajua kuwa yumo katika meli ile ile. Baadae Hamza Mwapachu alimfahamisha yule mgeni waliokuja kumpokea pale alikuwa nani katika siasa za Tanganyika.

proxy

Hamza Kibwana Mwapachu​

Simulizi kama hizi zilinifikirisha sana katika kutaka kuwajua wazalendo wa wakati ule. Hamza Mwapachu alikuwa anafanya haya ya kukusanya wananchi kumpokea kiongozi wa Waafrika chini ya pua za Waingereza bila kujali nini kitampata licha ya kuwa yeye kupewa uhamisho kupelekwa kisiwani Ukerewe peke yake ilikuwa ni adhabu, kwa hakika ni kifungo khasa cha kumtia kuzuizini asiweze kuenedeleza mipango yake ya kuunda chama cha siasa.

Uhuru ulipopatikana Chief Michael Lukumbuzya alipelekwa nje ambako alikuwa balozi na mwisho akawa balozi Canada ambako huko ndiko umauti ulikomfika.

6La5FUdYcnEadMYf6JSIrrWhkpElkSUYiAFTlRs_Bz4mDSXPmSD4EMzk4gTvEnMGuvf8pxy__jBGacnsvJHLYxP_wyS0OA25OYba8__txYHDI2z5TOfGkl7O_IoMO3NAleFvmru20T-YQF39hdK_UD7K79l2x2k40bDIMbiMoIB_ArerygwQ5oIGK11itARq1AoviA_D4OZrLGJZ-mOTiDWEC0pNQPmQPCS-cXzyWVr9raFuGLLKTwCz1GYMrJwsoBIeqCiy_AoHfwRMiTgHgBNRPHowAkwTnbtPxlJ_q9CTx_Ny6xhgBxkIMIBwc9Y79KJA7DXbYcODNB5X-lEL7SxzUEASzHc9r77_ByOVTHcN0j-HCDs2tr7oGw85M3YPXBv0OHG_2pnc_yZefK7n9_UyaxLXX1pmIeP1p01hc6LGf1QcrRusRSirpgfDZrxPMGTwr3EcKUjvY8vh1Kj2_zL9VnkUc-uHdQCSgUi6JBUaZrDi_2LVFAy1ImbD9BwIspcf8aHvXSBLQFSWfC2m3EGmjIMKOU2CDUXZv8NTjsn7UCfaBiWfrRT4ab3OSNhVpvB2GqLU1Rgk5_YjnfJgAxeKukdqeFoc=w476-h657-no

Abdulwahid Sykes​
Sydney Ahsante sana kwa vitu adimu kama hivi -Ahsante
 
Ahsante Mwalimu Mohammed Said kwa historia mujarabu! Nmejifunza mengi ya kihistoria kutoka kwenye simulizi zako na ningependa kujifunza zaidi... Kama mwalimu wa somo la Historia nimeona kuna mapungufu mengi hasa katika topic ya NATIONALISM f.4, kuna mengi yalistahili kuwepo hayapo! ... Ila ningependa kujua yafuatayo! Ukipata wasaa utuelimishe.
Role ya African chiefs ktk harakati za uhuru? Pia ningependa kujua kuhusu
Kassanga Tumbo
Kasela Bantu
Chief Abdallah Fundikira
Zubeir Mtemvu
 
Pukudu,
Kuna kitabu kipo kwa Kiingereza na Kiswahili nilichoandika
kuhusu maisha ya cha Abdul Sykes.

Kinauzwa: Msikiti wa Mtoro na Manyema Ibn Hazm Bookshop,
Slip Way Novel Idea, Soma Bookshop Mikocheni na Elite B/Shop
Mbezi Samaki.

Bei ni kati ya 10,000 ukinunua Ibn Hazm na kwengineko ni 13,000.
Pata kitabu hiki yote uliyouliza yapo humo.

YhA73nxTrRSSxcsKu8BYcrnD_y0y137b_JeukBx724bZ2gAZPa88NwpSJwV20NWzOD7NviuHYNori5gSSfxyhueutiz531IW16JiIfPvDihGEU-xh7qMYqbwGws3sbcYmXAIORwK3fOyIatNJPipbTxQbv-JzCe-zU30-irQfEqZ4Fpttxh7qoY_eT7KhzfGzbYJuzvMIj8DSBJjQMhbAot4J5XMFA2FMgWoZirzR1mdEySxs3VdXR2rWlEJp3vRzUpWAnjyXlIu8WeG6DvB6dbrv-4GTkUKlAv3YnQ27Nf-eS4ASGCv7mYerapZje5Ok6a6UjPdsevYazknB1pH5aZ-nq01BM8m46eCVUttXkX9JBN4Fy2fXtr1x6T8dJN4tyTjXOFdHPshGwSB7weaGE14WOVJOpAvJa38im29-bTNdxQAld_Akgg1FUo9AQA6jhmFrNbMoPD8__w6-a3EhhJ1NBW2Cunx9mj4Uz36LeCvzyF3_x334c8MvcDRvtcq3iL-nvZWTGsKez-7yioJq8BgZ4b1VcTcbSmgQ-1L1ZBGNA3N-nGJ7isxEzuDOrvbWUuc=w940-h690-no
 
Nguruvi3,
Kuhusu kusherehekea mapinduzi Wazanzibar wenyewe wananasihana
kuwa kuna mauaji yalifanyika katika mapinduzi haifai kusherehekea
kwani ni kinyume na mafunzo ya Uislam.

Nasaha zangu kwao ni hizo kuwa wamuogope Allah kwani yaliyopitika
ni ya kujutia.

Hakika nasimama katika kauli yangu kuwa sijamdharau na kumdhalilisha
Mwalimu Nyerere.

Ningeweza kuishia hapo lakini nitaongeza maneno ili nifahamike.

Nilichotofautiana na wanahistoria wengi na huu ndiyo ulikuwa msimamo
wa CCM katika historia ya TANU ni kuwa Mwalimu Nyerere ndiye aliyeunda
TANU 1954 (Angalia: Historia ya TANU, Chuo Cha Kivukoni, 1981).

Hapa ndipo tulipokhitilafiana mimi nikenda nyuma ya Nyerere nikaanza na
mwamko wa Waafrika kuanzia miaka ya 1929 na kw akutumia Nyaraka za
Sykes nikaeleza vipi siasa zilianza hadi kufikia 1950 walipoingia vijana kutoka
Chuo Kikuu Cha Makerere khasa waliokuwa Dar es Salaam wakishirikiana na
Sykes brothers Abdul na Ally Sykes walivyoleta mabadiliko ndani ya TAA.

Historia hii sasa inafahamika sina haja ya kuirudia kwa kirefu.

Hili la umuhimu wa Nyerere nilisema hivyo kwa muktadha wa mimi kuendelea
kutafiti katika historia ya TANU na harakati za kudai uhuru.

Umuhimu wa Mwalimu Nyerere kwangu mimi katika historia ya TANU na ya
kudai uhuru...

Maana yangu ni kuwa kwangu mimi nimeshasahihisha kile kilichokosewa kwa
wanahistoria kudhani kuwa kabla ya Nyerere hapakuwa na kitu.

Inawezekana wengine waliandika hivyo kwa kutokujua na wengine labda kwa
kuelekezwa na wengine kwa kujipendekeza (Angalia: HAK Mwenegoha (1976),
John Illiffe, Edward Barongo, Saadan Abdu Kandoro, Kirilo na Seaton
na Chuo Cha Kivukoni).

Mtafiti yoyote yule akiwasoma waandishi hawa walioandika historia ya TANU
watapata mshtuko mkubwa sana watakapokuja kusoma kitabu cha Abdul
Sykes
.

Baada ya kuandika historia ya TANU kama nilivyoelezwa na wazee wangu na
kuona nyaraka za wakati ule kuyakinisha niliyoelezwa kile kitendawili cha kuwa
kaja Nyerere Dar es Salaam 1952 kawa na ofisi, kawa na fedha za kuendesha
chama, kama na watu wa kumuunga mkono yote akiyafanya peke yake, kikawa
nimekitegua.

Sasa umuhimu wa mimi kuendelea na utafiti wa Mwalimu Nyerere na historia
ya TANU ndiyo sasa haupo tena.

Kama vile isivyowezekana kuandika historia ya TANU bila ya kumtaja Abdul
Sykes
kwa kutaja jina moja tu kwani yako mengi ndivyo hivyo hivyo
isivyowezekana kuandika histora ya TANUbila ya kumtaja Mwalimu Nyerere.

Nina yakini nimeeleweka.

Katiba ya kwanza ikiwa unakusudia ile aliyopendekeza Gavana Edward Francis
Twining,
waliyoiandika ni TAA Political Subcommittee na wajumbe wake ni hawa:
Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Abdulwahid Sykes, Hamza Mwapachu,
Dr.Vedasto Kyaruzi, Said Chaurembo
na John Rupia.

Hii ilikuwa mwaka wa 1950.

Swali la mwisho sina la kusema kwa kuwa nitakuwa nawasemea watafiti wengine.

Umuhimu wa Mwalimu Nyerere katika historia ya TANU umekoma kwangu kwa
sababu nimekamilisha nililokusudia.

Watafiti wengine wanaendelea (Angalia: Morton 2014).

Mwisho ningependa kusema kuwa umenipa sharti kuwa ''nisichanganye mambo''
kwenye kapu moja na ''nisitumie vitabu.''

Sijui vipi unaweza kufanya mjadala wa kisomi nje ya vitabu.

Ikiwa utaona nimeweka rejea za vitabu niwie radhi hali kadhalika ikiwa utaona
pia nimeweka yote katika kapu moja.
Ahaa sawa kabisa.

Na hapa nirejee kauli zako ili kuweka rekodi sawa sawa.

1. Mohamed Said anawaambia wazanzibar ''mapinduzi ya January 1964 hayana maana kwao kwasababu kulikuwa na mauaji na ni kinyume cha Uislam.
Hivyo, wanaosema mapinduzi daima, wanatenda kinyume''

2. Mohamed anasema, kwa mujibu wake baada ya utafiti umuhimu wa Nyerere haupo tena. Hapa anamaanisha umuhimu kwake haupo, na wala hajamaanisha umuhimu wa Nyerere kwa Taifa, Afrika na Dunia.

Hivyo neno umuhimu kama amelitumia ni kwake si wa watu wote, na umuhimu anaozungumzia ni wake si watu wote na wala haujaondoa umuhimu wa Nyerere kwa ujumla wake bali kwake. Mohamed kaliweka sawa

Kwa maneno mengine, dharau na kejeli za kushusha pazia ni kwa mujibu wake na kama mtu/mwandishi Mohamed ana haki ya kupinga au kukubaliana na lolote

Nitakuwa sina adabu, mpuuzi na mjinga nikisema umuhimu wa Abdul au Kyaruzi n.k hauna maana kwasababu tu sikubaliani na hoja kwa interest zangu.

Nitakuwa mshenzi niliyebobea kama nitasema Abdul Sykes hakuwahi kutawala hata siku moja nchi hii na hakuwahi kuwa mjumbe wa baraza lolote la utawala wa nchi hii.
Na kwamba umuhimu wake uliishia Karikoo.

Siwezi kufika huko nikiamini mchango wa kila mmoja unahitaji kuthaminiwa

Hata kama sikubaliani na mtu kwasababu nyingine, siwezi kuibadili historia

Tatu,Mohamed kasema kuna katiba iliyoandikwa na wazee ingawa hakuna kumbu kumbu popote pale ya katiba hiyo.

Anatueleza alichosimuliwa ,na hakika hadithi za mapokeo zipo hata katika vitabu vya dini.

Muhimu ni kuwa hakuna kumbu kumbu zozote za katiba hiyo ya wazee wetu

Nne,nilichosema ni kuwa hoja zinazotoka katika vitabu vyako unaweza kuzieleza kwa ufupi bila kujinukuu.Inachosha unapojibu hoja rahisi sana kwa kumpa mtu kitabu kizima. Ingalikuwa hivyo tusingekuwa na presentation
 
Ahaa sawa kabisa.

Na hapa nirejee kauli zako ili kuweka rekodi sawa sawa.

1. Mohamed Said anawaambia wazanzibar ''mapinduzi ya January 1964 hayana maana kwao kwasababu kulikuwa na mauaji na ni kinyume cha Uislam.
Hivyo, wanaosema mapinduzi daima, wanatenda kinyume''

2. Mohamed anasema, kwa mujibu wake baada ya utafiti umuhimu wa Nyerere haupo tena. Hapa anamaanisha umuhimu kwake haupo, na wala hajamaanisha umuhimu wa Nyerere kwa Taifa, Afrika na Dunia.

Hivyo neno umuhimu kama amelitumia ni kwake si wa watu wote, na umuhimu anaozungumzia ni wake si watu wote na wala haujaondoa umuhimu wa Nyerere kwa ujumla wake bali kwake. Mohamed kaliweka sawa

Kwa maneno mengine, dharau na kejeli za kushusha pazia ni kwa mujibu wake na kama mtu/mwandishi Mohamed ana haki ya kupinga au kukubaliana na lolote

Nitakuwa sina adabu, mpuuzi na mjinga nikisema umuhimu wa Abdul au Kyaruzi n.k hauna maana kwasababu tu sikubaliani na hoja kwa interest zangu.

Nitakuwa mshenzi niliyebobea kama nitasema Abdul Sykes hakuwahi kuwa kutawala hata siku moja nchi hii. Na kwamba umuhimu wake uliishia Karikoo.

Siwezi kufika huko nikiamini mchango wa kila mmoja unahitaji kuthaminiwa
Hata kama sikubaliani na mtu kwasababu nyingine, siwezi kuibadili historia

Tatu,Mohamed kasema kuna katiba iliyoandikwa na wazee wake ingawa hakuna kumbu kumbu popote pale ya katiba hiyo. Anatueleza alichosimuliwa kwa mujibu wake, na hakika hadithi za mapokeo zipo hata katika vitabu vya dini.

Muhimu ni kuwa hakuna kumbu kumbu zozote za katiba hiyo ya wazee wetu

Nne,nilichosema ni kuwa hoja zinazotoka katika vitabu vyako unaweza kuzieleza kwa ufupi bila kujinukuu.Inachosha unapojibu hoja rahisi sana kwa kumpa mtu kitabu kizima. Ingalikuwa hivyo tusingekuwa na presentation
Nguruvi3,
Ukipunguza hamaki na ghadhabu utaweza kufikiri vizuri sana na kuja
na hoja nzuri.

Mimi nakushinda kwa kitu kimoja.

Nimesomeshwa na Maalim wangu Sheikh Haruna adab za majadiliano.

Ndiyo maana ninapoandika hutoona tusi katika maandishi yangu wala
hamaki.

Ungeweza kusema yote uyapendayo bila ya kutumia maneneno, ''ushenzi,''
''ujinga,'' ''upuuzi,'' nk.

Naingia katika mnakasha.

Ningeweza kukuomba uonyeshe mahali nilipoandika kuwa ''mapinduzi hayana
maana,'' lakini nitakutaabisha bure na mimi sipendi mjadala wa nipe nikupe.

Hapa tupo barzani na barza ni moja ya mila zetu Waislam.

Mko barzani mnabishana lakini hambughudhiani na ukipiga duru ya kahawa na
kashata na anaekupinga na yeye pia anakunywa kwa starehe hakuna kinyongo.

Huu ndiyo utamaduni wa barza.
Kustahiana na kuheshimiana.

Nilichosema katika mapinduzi ni mauaji sikusema hayana maana.
Ikiwa kulisema hilo naweza labda kwenye muktadha mwingine si huu ulio jamvini.

Jibu na mbili ulivyosema ndiyo hivyo hivyo ila kwa hilo la ''dharau,'' na ''kejeli.''
Hilo hapana.

Hakuna mtu yoyote duniani awezae kumkejeli au kumdharau Mwalimu Nyerere.
Heshima yake inatambulikana dunia nzima.

Kuwa Abdul Sykes hakuwahi kutawala nchi hii hilo wala halihitaji kusemwa kila
mtu analijua ila umelileta kwa kuwa kifua chako kina joto chembelecho Maalim
Faiza
na ndiyo maana ukasema ''umuhimu wake uliishia Kariakoo.''

Hilo si kweli.

Umuhimu wa Abdul ulianza Burma akiwa katika 6th Battalion ya KAR wakati wa
Vita Kuu ya Pili.

Hapo ndipo alipowaeleza askari wenzake umuhimu wa kuunda chama cha siasa
kuwaondoa Waingereza Tanganyika.

Wakati huo Abdul alikuwa na umri wa kiasi cha miaka 23 hivi.
Angalia hiyo picha yake hapo chini akiwa Burma:

CIMG2281.JPG

Ukipitia Tanganyika Intelligence Gazette kuanzia 1950 hizi ni taarifa
za kikachero za Waingereza zikiandikwa na Special Branch utaona
habari za Abdul akiwa Dar es Salaam na mikoani alikokuwa akipita
kuongea na viongozi wa TAA kuhusu hali ya baadae ya Tanganyika.

Moja ya taarifa hizi ambazo mimi ninayo ni ni safari ya Abdul Sykes
ya Kanda ya Ziwa aliyofanya mwaka wa 1952 akiwa Katibu na Kaimu
Rais wa TAA kukutana na Paul Bomani na kisha kuelekea Uganda.

Lakini kabla ya hapa mwaka wa 1950 Abdul Sykes alifanya mkutano
na Jomo Kenyatta na kundi lake la kina Paul Ngei, Kungu Karumba,
Bildad Kaggia
na wengine Nairobi agenda kuu ikiwa kuunganisha nguvu
za Waafrika wa Tanganyika na Kenya kupambana na Waingereza.

Huu ulikuwa wakati wa Mau Mau.
Nimeeleza habari hizi kwa kirefu kwenye kitabu chake.

Mimi sikulaumu kuwa wewe hujui historia hii.

Utaijuaje ikiwa haikupatapo kuandikwa hadi nilipoiadika na kitabu kuchapwa
Uingereza mwaka wa 1998?

Tatizo lako ndugu yangu Nguruvi3 ni kuwa unataka kuleta ubishi katika jambo
ambalo wewe huna ujuzi nalo.

Katiba iliyoandikwa na wazee wangu mwaka wa 1950 ipo.

Abdul Sykes kaieleza katika taarifa yake kwa wanachama wa TAA (Angalia:
Annual Report of the Secretary of Tanganyika African Association, 7 January,
1951 Sykes' Papers).

Cranford Pratt katika kitabu chake ''Critical Phase in Tanzania,'' kaieleza na
kaisifia (Angalia: Cranford Pratt, The Critical Phase in Tanzania 1945-1968,
Cambridge University Press, London, 1976, uk. 29-31.)

''Document'' hii hutoweza kuiona popote pale kwa sababu hata Tanzania National
Archives (TNA) imenyofolewa jalada liko tupu.

Hata kwenye maktaba yake ya ''microfilm,'' pia imeondoshwa.
Halikadhalika katika Maktaba ya CCM Dodoma jalada pia liko tupu.

Nimepata kuandika kuhusu, ''Lost Documents,'' naitafuta hii paper nikiipata nitaileta
barzani In Shaallah.

Leo sishangai kwako wewe kunitaka mimi nikupe ushahidi wa katiba iliyoandikwa
na wazee wangu mwaka wa 1950.

Wakati tunahariri mswada wa kitabu kulikuwa na ubishani mkubwa kati yangu na
wachapaji kwa kuwa neno nililoandika ni kuwa nyaraka hii ya katiba ''imeibiwa.''

Mhariri hakupenda neno hili na akasema niseme, ''imepotea,'' au ''haikonekani.''
Isiwe ''imeibiwa.''

Nguruvi3,
Nimekupa ushahidi wa katiba ya iliyoandikwa na wazee wangu waliokuwa katika
TAA Political Subcommittee.

Document hii ilijadiliwa katika mkutano mkuu wa TAA 1954 mkutano uliounda
TANU na mwaka wa 1955 Nyerere alisoma yaliyokuwa katika ''document,'' hii
UNO mbele ya Kamati ya Udhamini.

Ikiwa hujaridhika na haya niliyokueleza mimi nipo hapa In Shaallah nasubiri.
Bahati mbaya unachoshwa na kusoma vitabu.

Mimi vitabu ndiyo maisha yangu toka nina umri wa miaka 6.
 
Umemaliza hiyo simulizi ya kale vizuri sana, hata bibi yangu baada ya uhuru alisahurika pamoja na kwamba alikuwa mwana harakati
 
Nguruvi3,
Ndiyo maana ninapoandika hutoona tusi katika maandishi yangu wala
hamaki.

Ungeweza kusema yote uyapendayo bila ya kutumia maneneno, ''ushenzi,''
''ujinga,'' ''upuuzi,'' nk.

Ningeweza kukuomba uonyeshe mahali nilipoandika kuwa ''mapinduzi hayana
maana,'' lakini nitakutaabisha bure na mimi sipendi mjadala wa nipe nikupe.

Nilichosema katika mapinduzi ni mauaji sikusema hayana maana.
Ikiwa kulisema hilo naweza labda kwenye muktadha mwingine si huu ulio jamvini.

Hakuna mtu yoyote duniani awezae kumkejeli au kumdharau Mwalimu Nyerere. .Heshima yake inatambulikana dunia nzima.

Umuhimu wa Abdul ulianza Burma akiwa katika 6th Battalion ya KAR wakati wa
Vita Kuu ya Pili.

Moja ya taarifa hizi ambazo mimi ninayo ni ni safari ya Abdul Sykes
ya Kanda ya Ziwa aliyofanya mwaka wa 1952 akiwa Katibu na Kaimu
Rais wa TAA kukutana na Paul Bomani na kisha kuelekea Uganda.
Mimi sikulaumu kuwa wewe hujui historia hii.

Tatizo lako ndugu yangu Nguruvi3 ni kuwa unataka kuleta ubishi katika jambo
ambalo wewe huna ujuzi nalo.

Katiba iliyoandikwa na wazee wangu mwaka wa 1950 ipo.

''Document'' hii hutoweza kuiona popote pale kwa sababu hata Tanzania National
Archives (TNA) imenyofolewa jalada liko tupu.

Hata kwenye maktaba yake ya ''microfilm,'' pia imeondoshwa.
Halikadhalika katika Maktaba ya CCM Dodoma jalada pia liko tupu.

Nimepata kuandika kuhusu, ''Lost Documents,'' naitafuta hii paper nikiipata nitaileta

Wakati tunahariri mswada wa kitabu kulikuwa na ubishani mkubwa kati yangu na
wachapaji kwa kuwa neno nililoandika ni kuwa nyaraka hii ya katiba ''imeibiwa.''

Mhariri hakupenda neno hili na akasema niseme, ''imepotea,'' au ''haikonekani.''
Isiwe ''imeibiwa.''
Mohamed , Pasco alisema jitihada zako ni kuhakikisha unamdhalilisha Nyerere.

Ukaomba ushahidi, nikauweka mara tatu kwa maneno yako ''Nyerere si muhimu tena katika historia...pazia limefungwa''

Ingawa umesema ni kwa mujibu wako tunajua nia yako dhidi ya Nyerere.

Una chuki dhidi ya Nyerere , unaandika na kuficha ukweli.

Unamtukana kwa lugha laini, kwa muumini, unafiki kauzungumzia mwenyezi mungu

Utasema Nyerere alimfukuza Sheikh Amir, huelezi sheikh alifanya nini dhidi ya Nyerere.

Hutasema Mwinyi alimwendea sawa Kassim Juma, utatumia neno serikali.

Hata siku moja hujaandika Kikwete kamfunga Ponda, unatumia serikali.

Ikifika kwa Nyerere, si serikali ni mtu.

Mohamed, Nyerere ni figure ambayo huwezi kuiwekea katika mizani na yoyote katika nchi hii, Afrika na Dunia. Nyerere anabaki kuwa Nyerere. Period!

Amebadili harakati zikazaa matunda. Ameandika katiba ya chama na nyaraka

Hadi zitakapopatikana nyingine, ukweli, alibadili siasa kwa elimu na utaalamu.

Nyerere amewakuta, akawaongoza na kuongoza Taifa miaka zaidi ya 20.

Huwezi kudharu mchango wake na huwezi kufuta historia hiyo! Nitty gritty

Kuhusu majadiliano,kufunzwa adabu ni suala moja, kutumia mafunzo ni suala jingine na kuelewa mafunzo ni jingine pia.

ungekukwa umefunzwa adabu usingemtukana Nyerere kwa ''semantics''.
Si kwa uongozi wake, bali kwa umri wa Nyerere wewe huwezi kumtusi ukatuambia una adabu. Unaweza kumkosoa si kumtukana!

Ndiyo maana mimi situmii ''semantics' nakueleza ukweli. Hatutaki unafiki tunasema wazi

Siwezi kuwa mshenzi wa kudharau mchango wa mzee yoyote yule aliyepigania uhuru wa nchi hii popote alipo, mwenyezi awarehemu waliotangulia.

Siwezi kuvaa vazi la chuki na upumbavu kudhalilisha mzee au mtu yoyote wa nchi hii popote alipo kwa lugha yoyote kutokana na harakati za kulikomboa Taifa

Pazia la Nyerere haliwezi kushushwa, anazungumzwa Duniani kila siku

Unaweza kuwa na chuki na Nyerere ni haki yako, lakini chuki si sehemu ya historia
Ni chuki zako moyoni na zitafutie dawa, historia si mojawapo ya tiba

Narudia tena, Kyaruzi, Kidaha, Chaurembo, Sykes, Mkwawa, Mirambo, Selengie n.k. wana nafasi zao katika nchi hii, tunawashukuru.

Nyerere ana nafasi yake, haifutwi kwa pazia la Abdul hata siku moja. Ishi na uchungu huo

Abdul hakuwahi kuingia baraza lolote la utawala wa nchi hii.Ni ukweli.

Hakuwahi kutawala nchi hii hata kwa dakika moja, ni ukweli.

Unaposema Abdul anafunga pazia la show ya Nyerere ni matusi kwa wote wawili
 
Back
Top Bottom