Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Bibie FaizaFoxy nilitaka kuandika Mwalimu si mwanamama usikimbilie mambo madogo madogo ebo.

Kwako unaliona dogo? Umebadili historia nzima halafu unasema dogo?

Inabidi uombe wanajamvi msamaha. Mwalimu na "mwanamama" wapi na wapi?
 
Makinda wa maalim Mohamed mnatapatapa tu mzee wetu kashindwa kujibu hoja za mkuu Nguruvi3 hapo juu ya yye na mwapachu nani mrongo?
Wembeee,
Sijashindwa nimetoa majibu isipokuwa hakuridhika na majibu yangu.
Mimi siko hapa barzani kutafuta ushindi dhidi ya yeyote awae yule.

Mimi niko hapa kueleza yale ambayo wengi hamkuwa mnayajua.
Halikadhalika niko hapa na mimi nijifunze kutoka kwenu kile ambacho
mnakifahamu katika historia ya TANU.

Lakini bahati mbaya historia hii hamuijui kwa hiyo mnaniuliza maswali
na mimi najitahidi kuwajibu kadri ninavyoweza.
 
Sasa wewe hapa unatafuta ugomvi buree,Ustaadhi Mohamed Said hana uwezo wa kujibu hoja kazoea kulisha makinda wasokuwa na uwezo wa kuchagua au chakula wanachopewa ikifika mahali watu kahoji kwa hoja nzito juu ya maandishi yake yenye utata mwanzo mwisho utimua mbio na sababu kedekede mara nilidarasisha chuo kikuu cha Lagos, akigeuka kushoto atakwambia hata Msikiti wa Manyema wanatambua kipaji chake na Sheikh Chaurembo anamtambua haya sasa na sisi tunataka kutambua uwezo wako maswali kiduchu tena kwa maandishi aliyoyaleta mwenyewe anakimbilia kwa wajukuu wa wapigania uhuru ebo kumbe huyu Ustaadhi mwepesi sana halafu anataka kumshusha Baba wa Taifa Mwl Nyerere kumlinganisha na msimamizi wa soko.
Mzee wetu ni mwepesi sana kwenye hoja za msingi kama zile za mkuu Nguruvi3 ndio Mahana kaenda kuwaita makinda wake waokoe jahazi lkn me namuomba majibu ya hoja za Nguruvi3 ndipo twende mbele
 
Kolorama,
Waleikum Salaam Warahmatullah Wabarakatuh,

Kitabu kinapatikana Ibn Hazm Media Centre Bookshop
Msikiti wa Mtoro na Manyema, Soma Bookshop Mikocheni
na Novel Idea Slip Way Masaki.

Bei ya Ibn Hazmm ni 10,000 kwengineko ni 13,000.
Shukran jazirah nitapita weekend in shaa Allah
 
Mkuu Carlos ulikuwepo mnakasha mmoja mrefu sana miaka mitatu nyuma. Mkuu Nguruvi3 na hao wote anaolalamikia walikuwepo kiukweli ulikuwa ni mtanange wa nguvu mpaka Yericko alikiri kuwa si mtoto wa Nyerere. Sasa hawa nawaita waarabu wa pemba sisi tupate darsa ndo muhim
Kolorama, nakumbuka kipindi hicho nilikuwa nafuatilia sana ingawa sikuwa mchangiaji sana nakumbuka uzi ulikuwa unaitwa uchochezi wa Mohamed Said.
 
Wembeee,
Sijashindwa nimetoa majibu isipokuwa hakuridhika na majibu yangu.
Mimi siko hapa barzani kutafuta ushindi dhidi ya yeyote awae yule.

Mimi niko hapa kueleza yale ambayo wengi hamkuwa mnayajua.
Halikadhalika niko hapa na mimi nijifunze kutoka kwenu kile ambacho
mnakifahamu katika historia ya TANU.

Lakini bahati mbaya historia hii hamuijui kwa hiyo mnaniuliza maswali
na mimi najitahidi kuwajibu kadri ninavyoweza.
Je maalim ms umekubali kua wwe ni mzushi sababu umetoa maelezo tofauti na mwapachu kwenye issue moja ya Nyerere kutambulishwa kwa viongozi wa chama kwa mara ya kwanza?
 
Mzee wetu ni mwepesi sana kwenye hoja za msingi kama zile za mkuu Nguruvi3 ndio Mahana kaenda kuwaita makinda wake waokoe jahazi lkn me namuomba majibu ya hoja za Nguruvi3 ndipo twende mbele
Sasa wewe unawaita members wenzako makinda kisa unatofautiana nao mitazamo angalia lugha yako kuwa na stara watu wakikujibu kihuni utalalamika kweli? Nguruvi mkanye kijana wako.
 
Makinda wa maalim Mohamed mnatapatapa tu mzee wetu kashindwa kujibu hoja za mkuu Nguruvi3 hapo juu ya yye na mwapachu nani mrongo?
Mkuu wembeee heshima yako. Kuniita kinda wa maalim kwangu sikwaziki Bali naona ni sifa nzuri kwani nimepata ilmu kubwa sana kupitia kwako. Ila siwezi kuwa kinda kwako kwani sina nijifunzayo toka kwako. Labda uniambie wewe ni kinda la nani?
 
Shukran jazirah nitapita weekend in shaa Allah
Kolorama,
Ningependa usoma na kitabu cha Ali Muhsin Barwani:
Conflict and Harmony in Zanzibar kiko Ibn Hazm na
Tanzania Publishing House Samora Avenue.

Bei ni 10,000.00

Kitabu hiki ni kumbukumbu zake na kwa hakika kuna
mengi kuhusu mchango wa, Nyerere katika kuiangusha
serikali ya Sheikh Mohamed Shamte, Zanzibar 1964.

Ukivimaliza vitabu hivi viwili utajua kwa nini hali ya Zanzibar
na Tanzania Bara iko hivi iliko leo.
 
Mkuu wembeee heshima yako. Kuniita kinda wa maalim kwangu sikwaziki Bali naona ni sifa nzuri kwani nimepata ilmu kubwa sana kupitia kwako. Ila siwezi kuwa kinda kwako kwani sina nijifunzayo toka kwako. Labda uniambie wewe ni kinda la nani?
Mi sio kinda wa mtu yyte yule sababu natumia akili kuhoji sio kama nyie kila neno mnapanua mdomo na kumeza paspo kuchagua zipi pumba hupi mchele mwisho wa siku mnameza sumu paspo kuhoji
 
Mkuu wembeee heshima yako. Kuniita kinda wa maalim kwangu sikwaziki Bali naona ni sifa nzuri kwani nimepata ilmu kubwa sana kupitia kwako. Ila siwezi kuwa kinda kwako kwani sina nijifunzayo toka kwako. Labda uniambie wewe ni kinda la nani?
Nadhani umemjibu vyema.
 
Kolorama,
Ningependa usoma na kitabu cha Ali Muhsin Barwani:
Conflict and Harmony in Zanzibar kiko Ibn Hazm na
Tanzania Publishing House Samora Avenue.

Bei ni 10,000.00

Kitabu hiki ni kumbukumbu zake na kwa hakika kuna
mengi kuhusu mchango wa, Nyerere katika kuiangusha
serikali ya Sheikh Mohamed Shamte, Zanzibar 1964.

Ukivimaliza vitabu hivi viwili utajua kwa nini hali ya Zanzibar
na Tanzania Bara iko hivi iliko leo.
Nashukuru sana mwalim wangu nitavipitia in sha Allah ili nijue nijifunze
 
Mzee wetu ni mwepesi sana kwenye hoja za msingi kama zile za mkuu Nguruvi3 ndio Mahana kaenda kuwaita makinda wake waokoe jahazi lkn me namuomba majibu ya hoja za Nguruvi3 ndipo twende mbele
Wembeee,
Ikiwa umependzwa na maneno hayo yako sina la kukufanya.
 
Je maalim ms umekubali kua wwe ni mzushi sababu umetoa maelezo tofauti na mwapachu kwenye issue moja ya Nyerere kutambulishwa kwa viongozi wa chama kwa mara ya kwanza?
Wembeee,
Mbona nimekujibu hilo?
Nakuwekea tena jibu ambalo nimeliweka sasa katika blog yangu:

WATOTO WA WAPIGANIA UHURU BI. MAUNDA PLANTAN, JUMA MWAPACHU, HAPPY MTAMILA NA KLEIST SYKES WANAPOWAKUMBUKA WAZEE WAO
Nguruvi3,
Ama ingekuwa si kwa kuwa naburudika kufanya mjadala na wewe
mie muda mrefu ningelikwisha nyanyua mikono juu lakini nastarehe
kuongea na wewe.

Allah amekupa kipaji cha aina yake.

Majibu nimekupa kuhusu katiba ya TAA Political Subcommittee kuwa
nyaraka na microfilm zote hazionekani Maktaba ya CCM Ddodoma
na TNA.

Sikuishia hapo nimekueleza kuwa kabla yangu katiba hiyo ilitajwa na
Listowel mwaka wa 1965 na Pratt 1976.

Bado unataka nikuletee hiyo document.
Kama wewe hodari sana mbona huwaulizi CCM nyaraka hizo zilipo?

Lakini ninastarehe katika mnakasha huu kwa kuwa natoa darsa na
wengi wanasoma historia ambapo hawakupatapo kuisikia hata kwa
mbali.

Ndiyo maana narudi hapa tena na tena na tena.
Nakushukuru sana kwa hili.

Sasa nisikikize kwa makini na tuliza ubongo wako nikufunze mbinu
za ''critical analysis'' na kujifunza kusoma katikati ya mistari.

Sitakujibu hayo yote uliyoandika nitakujibu hayo tu ambayo umeweka
rangi nyekundu.

Hamza Mwapachu alimjulisha Nyerere kwa uongozi wa TAA 1949.

Akili yako mara moja imekwenda kuwa walikuja hadi New Street na
kuzungumza na Mwalimu Thomas Saudtz Plantan aliyekuwa rais na
Clement Mohamed Mtamila aliyekuwa katiibu wa TAA wakati ule.

Lakini ukweli ni kuwa Mwalimu Thomas Plantan na Clement Mtamila
walikuwa hawajapata kukutana na Nyerere hadi alipokuja kwa Abdul
Sykes
1952.

Inawezekana ujulisho huo ulikuwa wa salam za mdomo au wa barua.

Nakuwekea picha nikifanya mahojiano na Bi. Maunda Thoams Plantan
mtangazaji wa kwanza wa kike Tanganyika Sauti ya Dar es Salaam 1952
na mwalimu wa shule.

HF-E-j6n6D2pW-h8ANND7lxCGUZH73Fhpokdj2U2guz10UUuq33enwGopPRGbfU8HCP7ZcOmNxS-DYu2x5-G9w9vqeN1Qi-nUydPTJmLDHXRS5Py3_84OP_2iecQyjAYflQuA-tfQEQHjxuJ2g-u9pEPK4ambOrJMcYaSt3LVeEiUl_Vmzi9FR4Tc93Ia6bRAnRaPJaZduvvap83uIisUDG_MLkVDJflrFjbfG52G0QkumZ1Q8RLCfhByBEOZSMLvacusXptB2KzZUZsPAhrME9h_gdQ7j3rtG2ZsdVBVOrbgBhPzNax2ekRbIh04vu7ScoezknEk38PM7QP387nntcrgWcDyiEXt0YQPmsByTOz1rAvCc-6WY0lmImew7xIbgp98ByU2R77IA5nGTGz8u56qfwSP6b2qDXMgh6gTm5q6_htGMMiIpNWtqbNLOCELZGKVMJArxuwYYP0S9ZMKK-ZoOBxgFTNE8p2DBcjtpISFD4AdqyqQg2OxjxjVvoqSJPGzr0cyRCfG_8asDxe6xqXSCz2KmWUg2Ndylw8Pz1Fth1LBc2j5yNsnv-qClIy78x38wD3lCWFVEnKTs3aaibrjebomUxY=w480-h360-no

Mjukuu wa Affande Plantan na mtoto wa Mwalimu Thomas Saudtz
Plantan,
Bi. Maunda Plantan na Mwandishi

Katika mazungumzo yetu hakupatapo kunambia kuwa baba yake
alipata hata kwa siku moja kuonana na Nyerere.

Nimezungumza pia na Happy Mtamila hata mara moja hajanieleza
kama baba yake alipata kuonana na Nyerere kabla ya 1952.

20140808_140140-001.jpg

upload_2016-6-21_11-46-48.gif

Kulia Bi. Happy Mtamila na Mwandishi

Ningependa kukufahamisha tu kuwa uamuzi wa Nyerere kuacha kazi
ulifanyika nyumbani kwa Clement Mtamila Mtaa wa Kipata na Sikukuu.

Nyumba hii ilikuja kununuliwa na ukoo wa Baharoon ikavunjwa na
sasa ni ghorofa.
SKBStS8549EaS0LxcEjPslwMEGrAB07SVS4y1IX7IQnuFwFpUCQe_v4W3SeizHuDKf2QH3V0WlKT2EqL9kIQq6ednrg2U9uH6k3dlQmT8Mz7rNi1eqPmhE_EFy-NKlDVZ21yEeXyqFYXSn9KOClKilhcl_SRKRbOPBUWWLHdalTWPVz0WEbPArthXt8gVi3tWw2Bt21UquEHBsNTWOQY-NnX7QM5aT7wgpS00oAJGLZ8S02z_uMqJbKzQoFC1lnjt6NuvKlJ5uzUMEASF9-SovB663Ktqcylkzm9xxCARJHv6UgxrXqpU1O0ySM9kTZE3fTaI6aXWfF8jJBamFMv75OHkcKK_6YgSLp6jXkdIPVY0gjgjOF6UiCnxj1wJL3T6RMY2tJpgJFNaJJHxbKjfT6K_Y94ur8JrmjsBuDPrHefHLGHpt9Ys_Vp_gD8_JdI3Prg4jIltelpjXFSUapbD80qO1qU4zLrPk0cVcw3fl1tCD65m-3DiigAOFIUffL8YUwWMkCQhFlrHLX3VkiE9NGA6BrAfqp8ugUPHW1DzZYAtdD1pDyYduZPfJJvI4rsiw-4NqyadZXRvJVFziWXt48Oah53RcI=w986-h657-no

Kushoto: Kleist Abdulwahid Sykes, Ebby Abdulwahid Sykes, Saudtz
Thomas Plantan na Abdulwahid Ally Sykes
 
Attachments

  • upload_2016-6-21_11-46-47.gif
    upload_2016-6-21_11-46-47.gif
    43 bytes · Views: 37
Vp, akina Marialle, role yao TANU, na uhuru wa nchi hii!

Ndakilawe,
Iko siku mimi na Abbas Sykes tulikwenda nyumbani David Marealle.

David Marealle ni mdogo wa Chief Thomas Marealle na tukiishi jirani.

David Marealle
akanambia mimi kuwa yeye alipofika Dar es Salaam kwa
mara ya kwanza alifikia nyumbani kwa Abdul Sykes kwa maelekezo ya
kaka yake Chief Marealle.

Hii ilikuwa katika miaka ya 1950.

Nimesoma barua ambazo Chief Marealle akiandikiana na Ally Sykes.

Taarifa nilizopata katika barua zile sikuziweka katika kitabu kwa sababu
kadhaa.

Lakini nitakuwekea hapa mazungumzo niliyofanya na Mwalimu Sakina
biti Arab
akinihadithia uhusiano kati ya Chief Marealle na Abdul
Sykes
:

''Abdulwahid’s house was also a center of socialising for the young
intellectuals and their wives. Abdulwahid had very good relations
and was at ease with a good number of chiefs. Whenever they
were in Dar es Salaam to attend the Legislative Council, Abdulwahid
would seize the opportunity to invite them to his house for lunch or
dinner and sometimes he would throw a party for them. Among them
were Chief Haruna Msabila Lugusha of Sikonge, the first Tanganyikan
to qualify as an agriculturalist, and Chief Thomas Marealle of Marangu
(Abdulwahid used to address him as ‘King Tom’, the reason being that
the British wanted Africans to believe that it was only white people who
could have monarchies with lines of kings, queens, princes and princesses.
Africans could only have chiefs).''

Abdul hakufanikiwa kuwaleta machifu katika TANU kama vile alivyoshindwa
kumleta Chief David Kidaha Makwaia katika uongozi wa TAA na kisha waunde
TANU.
 
F.F...

Kinachostaajibisha zaid ni pale ambapo Al mujitahid Mohamed Said anapotia nanga humu JF kutoa ilm zake bila khiyana hawa hawa wanaosema kwamba hana lolote ndiyo huwa haraka haraka kukimbilia kuweka kitako na kumsikiliza...kinachostaabisha zaid badala ya kuuliza wapewe ilm zaid wao wameendelea na ule ule utaratibu wao wa kupiga mazumari yasiyo na maana...

Always sisi tunawaambia kuwa wao ni wa humu humu...

Watabakia kuwa wa humu humu...
Lugha za stara kama zile unazotumia wewe? Si ndiyo maana yake?

Naona juu huko ulianza kuomba poo na kuleta porojo eti za Alama Mohamed Said kuita watu!

Mimi nnakuitia hapa Mag3, Mzee Mwanakijiji, anaejiita Yericko Nyerere, Pasco and the likes, mkusanyane wote, mjadili hii historia na Alama Mohamed Said pekee, pia hamumuwezi hata chembe. Sana sana mtaanza lugha chafu tu.

Chambilecho, humu kwani tunapewa ilmu bila hiyana na nani mwengine zaidi ya Alama Mohamed Said?

Sisi tunafyonza ilmu tu, tofauti kubwa ni kuwa hao wanaotajwa ni wazee wetu tunaowajua amma wao amma watoto zao amma wajukuu zao.

Tunasoma na kupata ilmu na entertainment hususan pale unapokuja na maswali ya kebehi, huwa tunasubiri kwa hamu unavyofundwa bila khiyana na Alama Mohamed Said.
 
Back
Top Bottom