Tetesi: Handeni, walioiba silaha Ofisi za TAKUKURU ni TAKUKURU wenyewe

Tetesi: Handeni, walioiba silaha Ofisi za TAKUKURU ni TAKUKURU wenyewe

Habari za mapumziko,

Inasemekana walioiba Silaha kwenye ofisi za TAKUKURU huko Handeni ni maafisa TAKUKURU wenyewe.

Chanzo chetu kutoka Handeni kinasema maafisa hao wakishirikiana na watu wa ishu/Majambazi walisuka njama za kuziiba silaha hizo huku wakiahidiwa kupewa donge nono.

Inasemekana siku ya tukio washukiwa walikuwa wote kwenye baa moja maarufu wilayani hapo wakikamilisha mpango huo.

Mnyetishaji wetu anasema hakukuwa na uvunjifu wowote na kutupwa kwa funguo ni geresha iliyopangwa na maafisa hao ili kuonesha kwamba walikuwa ni majambazi.

silaha hizo zilisafirishwa usiku na kupelekwa mkoa mmoja huko kaskazini mwa nchi ambako kuna ujambazi mwingi.

Tunazishauri mamlaka zinazohusika ziwabane MAAFISA TAKUKURU Ili wakaoneshe silaha zilipo kwani wao ndiyo wahusika kwenye mpango huu.

Nawasilisha

Iwe wamehusika au hapana.hili ni suala linalohitaji majibu yasiyo mepesi.sababu hii ni taasisi nyeti sana.kutokea kwa tukio hili lenye utata namna hii linatia dosari sana kwa credibility ya Takukuru
 
Hiyo ni mikoa ya kanda ya ziwa,

Mikoa ya kaskazini ni arusha, manyara, kilimanjaro na tanga

Kanda ya kati kuna singida dodoma nazani na tabora

Kanda ya mashariki kuna pwani dsm na morogoro

Kanda ya kusini kuna lindi mtwara na ruvuma

Kanda yanyanda za juu kusini kuna iringa njombe mbeya na songwe

Kanda ya magharibi au ziwa tanganyika ni kigoma na rukwa na katavi

KAnda ya ziwa ni shinyanga simiyu mara geita mwanza na kagera
Kagera na mwanza ipo kusini ?wewe shule ulikwenda kusoma UJINGA

USSR
 
Kagera na mwanza ipo kusini ?wewe shule ulikwenda kusoma UJINGA

USSR
Mueleweshe kwa urahisi.
-Kanda hutumika kueleza uelekeo ilipo mikoa au sehemu mchanganyiko kwa uhalisia au kukaribishia(approximations) tu.
-uelekeo(positions,locations)ndiyo uhalisia wa eneo tajwa ulipo kimahesabu ya sayansi kijiografia.Aelewe kutofautisha na kukariri.
 
Back
Top Bottom