'Hangover' ya propaganda za utawala wa Magufuli zitadumu kwa baadhi ya watu milele

Tatizo sio Magufuli na wala sio propaganda, tatizo ni sisi wananchi na umaskini kwa ujumla.

Umaskini ndio tatizo kubwa linalotukabili na tunalo pigana nalo, huo umaskini umeleta pia uvivu na uzito katika kupigana nao, kiasi cha kutegemea aje mtu fulani atusaidie kupigana na umaskini.

Ndipo anapokuja mwanasiasa kwa engo ile ile ya kupigana umaskini unaotukabili.
Huyo mwanasiasa nae kwa sababu ya umaskini amekua akiutumia umaskini kuwaaminisha wananchi kwamba yeye ndie pekee anaeweza kuwaondoa kwenye umaskini, badala yake anafanya wengi wawe maskini ili aungwe mkono na watu wengi.

Tokea uongozi wa mwalimu Nyerere mapaka huu wa samia ni mapambano tu dhidi ya umaskini, badala ya hata huo umaskini kupungu ndio unazidi kuongezeka na kuwa mbaya zaidi maana umeenda mpaka umaskini wa fikra na akili.

Umaskini huo huo ndio unamuona Samia ni bora kuliko Magufuli, na ndio huo huo ulimuona Magufuli ni bora kuliko Kikwete, na huo ulimuona Kikwete ni bora kuliko mwinyi na kwa mwalimu Nyerere pia dhidi ya mwinyi.

Na huo huo umaskini ndio utakao kuja kufanya samia aonekane hakufanya kitu dhidi ya mwandamizi wake.

Yote ya yote katika mapambano dhidi ya umaskini kwa nyakati zetu hizi magu6 alikua na heri kwa kiasi chake.

Kwa vile yeye aliku mwanadamu, na mwanadamu hana ukamilifu wowote isipokua Mungu na ndio maana yanakutwa makosa kwake, ajaliwe pumziko la amani milele.
 
Utakuwa unaliwa na kibamia wewe
 
Ni FISADI tu huyu hana lolote
 
Mpaka leo Zanzibar wanahangaika na jina tu la Shamte. Waziri Mkuu kwa chini ya miezi 2.
 
Well said.
 
Mtoto wa dada yake, aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya fedha Dotto James alifanya kazi kubwa sana kusafirisha fedha za mjomba wake nje.
Umejaa uongo na propaganda wewe chawa wa awamu ya 6.

Kama mnadhani kumchafua Jpm kutawapaisha kisiasa na kuwafanya raia wasahau ugumu wa maisha wanayopitia mnajidanganya.
 
We ajuza hutakaa uolewe na umbea wako
 
Haha kipindi hicho nilikua hainipiti hotuba zake hata kidogo lakini Sasa hata dakika Moja siwezi kumsikiliza huyo mama

Alinijaza uzalendo wa kweli lakin Sasa .mmh

Ni ujinga tu...
 

Ambwene Mwasongwe song: Alikuta ibada.#'
 
Usisahau Elimu bora yenye kufikirisha na vitendo.
 
Propaganda zipi unazoziongelea!!? Watanzania waliambiwa tunajenga bwawa la nyerere,sgr mabarabara,madaraja (busisi nk.) viwanja vya ndege na kila aina ya miundombinu tanzania nzima kila mkoa kulikuwa na ujenzi unaondelea na wananchi waliona kwa macho,

leo hii mpumbavu mmoja anatoka mbele na kusema kuwa ule ulikuwa ni uwongo na propaganda za mwendazake ,mkitaka kupambana na marehemu fanyeni mara mbili ya yale aliyoyaanzisha na sio ku mbwela mbwela kama makalio yaliyokata seal.
 
Kama zilivyodumu za Mwalimu. Si ajabu kusikia vijana wakisifia enzi za Mwalimu kumbe hata walikuwa hawajazaliwa wakati anang'atuka.
Hiyo ndiyo nguvu ya propaganda.
Nimecheka nikikumbuka zile enzi ukiona watu wameweka mawe kwenye foleni na wewe unaweka la kwako hata hujui ni kitu gani unapangia foleni. Alimradi cho chote kitakachouzwa kwenye duka la RTC basi unakihitajia. Siku nyingine unauziwa mpaka jembe la kulimia kwa lazima.
 
Alimuua nani huko kwenu? Ndo maana tunasema mna maneno mengi ila mna mambo yenu binafsi tu wala sio sababu za kijamii
Magufuli kaua hilo halina ubishi. Siyo kwa sababu wewe uko hai na kwenu hakuna aliyeuliwa ndiyo useme hakuna! Jiulize tu kwa nini hatumuandiki Kikwette au Mwinyi na Mkapa kwa habari hizi? Kwa nini yeye tu!!
 
Alianzisha miradi hiyo kibwege kwa kukurupuka bila utaalamu wa project management matokeo yake mpaka anakufa hakuna hata mmoja uliofika 40% mpaka anakufa. Ni ubwege pia kumsifia kwa kuanzisha mradi halafu haujamalizika

Angekuwa na akili nzuri angejikita na mradi mmoja kwanza say SGR pengine leo ingekuwa imemalizika na inaingiza fedha
 
Umejutahidi kupambana na marehemu unasahau kupambana na maharamia wanao ishi.

Unapoteza mda. Umejitahidi kuandika tuhuma pasi na ushahidi.
1. Taja real estates za Magufuli na document zake

2. Bank gani ya nje ya nchi alificha pesa? Ni kiasi gani hicho?

Mtu alijitahidi kutatua shida za wananchi wewe unaita propaganda? JPM alipowabinya wezi wa Twiga na wauwaji tembo ndipo unaona shida?

Katika bandiko lako unazani hakuna hata jema kwa JPM?

Nakushauri, pambana na walioko madarakani tuone kama una Nia njema na maisha yetu. Vinginevyo tutakuona choko tu
 
Magufuli kaua hilo halina ubishi. Siyo kwa sababu wewe uko hai na kwenu hakuna aliyeuliwa ndiyo useme hakuna! Jiulize tu kwa nini hatumuandiki Kikwette au Mwinyi na Mkapa kwa habari hizi? Kwa nini yeye tu!!
Sababu kubwa aliwanyima tonge. Sasa hivi mnalamba Asali mtasema Nini kingine ili mnenepe zaidi?
 
Magufuli kaua hilo halina ubishi.
Siyo kwa sababu wewe uko hai na kwenu hakuna aliyeuliwa
ndiyo useme hakuna! Jiulize tu
kwa nini hatumuandiki Kikwette
au Mwinyi na Mkapa kwa
habari hizi? Kwa nini yeye tu!!
Jibu liko wazi kwa sababu mnamchukia, we fikiria hivyo vifo vya kuokota maiti za kwenye viroba ni kipi kilichofanya hadi hivyo vifo vihusishwe na Magufuli? Utagundua ni chuki tu ndio hufanya mumpa hiyo tuhuma.

Kuna wengine wanakwambia alikufa kwa corona ila hana sababu yeyote ya msingi ya kushawishi kuwa kweli alikufa kwa corona na ajabu unakuta mtu anaamini hivyo na humwambii kitu, unagundua hii ni athari ya chuki yani mtu anaona kusema Magufuli kufa na corona ni jambo la kumdharirisha ni kama adhabu.
 
Propaganda ipi unayoizungumzia wewe

1) kutumbua watumishi mafisadi?
2) Kufanikiwa kudhibiti ujambazi na ajali barabarani?

3) Kujenga Reli ya mwendokasi?
4) Kununua Ndege?
5) Kujenga bwawa la Umeme?
6) Kujenga mwendo kasi mbagala to Kkoo?
7) Kutoa elimu bure?
8) Kupeleka makao makuu ya serilali Dodoma?
9) kuondoa shida ya wananchi kuchukua mizigo yao bandarini kwa kuwambia bandari washughulikie documents kabla mzigo haujafika ili meli ikifika tu watu wachukue mizigo yao?

Sent from my TECNO Camon CX using JamiiForums mobile app
 
JMP ameondoa shida gani kwa Wananchi? Magufuli ameondoka watu hawana fedha, deni la ndani limekuwa zaidi kwa kuchukua fedha za watu na kuwekeza katika miradi mikubwa ambayo haina faida ya moja kwa moja kwa watu.

Ndani ya miaka mitano amekopa over 10 trillion, wewe huogopi? Ndege, SGR, Mwendokasi na miradi yote mikubwa amekopa nje bila approval ya Bunge. Kupeleka mji Mkuu Dodoma ni mpango wake wa kutoa zabuni kwa makampuni ya ujenzi ya Kichina ili apate 10%, acheni upuuzi huyu jamaa was filthy thief.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…