Haniulizi kwa lolote

Haniulizi kwa lolote

Aisee huwa nataman kukutana na wanawake wa dzain hii,awe na kwake na mimi kwangu,na asiwe na wivu wa kifala kama wa wanawake wengne.........nashindwa hata kukushauri maana naona wewe ni mswahili umezoea wanawake wa kiswahili,huyo humuwez
 
Kumbe ile kununa nuna kwa wanawake kunawapendeza watu wengine.

Yuko poa huyo,oa utulie.
 
Usikute hata kitandani haupo vizuri, kuwa mwanaume
 
Sio kwamba ana akili nyiingiiii. Manzi Jamaa siyo size yake. Ni sawa na nikk minaj awe related na baraka da prince. Baraka ataburuzwa tu na nikk atakuwa tayari kwa lolote kutoka kwa baraka [emoji23][emoji23][emoji23]
Hayo Mapenzi yapo tu inategemea wewe una act vipi kama Mwanaume, mfano Aunt Ezekiel,Diamond,na wapenzi wao,,pia kuna Dogo mmoja tunaishi nae hapa Katoro Geita,,alitongozwa akakubali,,Akaelekezwa nini cha kufanya kafuata vyote huko kwenye migodi Leo Wamezaa watoto na ndoa yao Imeimalika na tunavyo ongea Leo Jamaa Anasauti na Anauwezo wa kujisimamia na kuhoji,,na mke alikuwa kama anajaribu but Leo Kazama ,,Yule Dogo aliweza kusoma akili za mke wake Leo amerudisha heshima take,,Huwa ni kumsoma MTU unayeishi naye tu kaka,,Kuwa na uwezo wa kuwaza zaidi yake japo yeye mwanzo ataona kama anakukontro but hufikia siku anakubali na kukukubali zaidi ya mwanzo,, so usipomfahamu yeye direct atakuwa amekuzidi akili ya Maisha
 
Mtoa mada...vp kwenye yale mambo yetu...analalamika hata kidogo au kimya kimya tu...vp at a anajitingisha hata kidogo??? .....ila nimempenda sana huyo Dada iwish ningekua hivyo hizi mbulukenge zingenitambua
 
Habari
Naomba nianzie mbali kidogo, mimi ni mwanaume wa miaka 43. Sijaoa ila niko mbioni kuoa. Wakati nilipomaliza kidato cha nne, nilijikuta katika mahusiano yaliyoniletea mtoto wa ujanani mapema sana. Mama wa mtoto huyu tuliachana nilipoingia chuo kikuu, hivyo nikawa kwenye mahusiano ya hapa na pale ambayo hayakudumu kwa kweli kiasi cha kufikia kuoana.

Mtoto wangu alipofikisha miaka 10 nilimchukua toka kwa mama yake na kuanza kuishi naye wakati huo nikiwa naishi kwa wazazi na hata nilipoanza kujitegemea niliondoka naye na niko naye hadi sasa na ni binti mkubwa tu. Kuna wakati tulikwaruzana sana na binti yangu. nadhani katika zile hatua za ukuaji. Akawa mtukutu sana na mwenye maendeleo mabaya shuleni.

Sasa katika kutafuta mahusiano nikajikuta katika mahusiano na mwanamke mmoja ambaye nimemzidi miaka 10. Mwanadada huyu tulikutana katika halfa fulani. Tukafahamiana na taratibu tukawa marafiki. Kiukweli nilivutiwa naye sana sio tu kwa mvuto alionao, bali pia namna alivyokuwa amejiweka. Msomi, mjasiriamali, muelewa na msikivu.

Nikawa nasita kidogo kumtokea nikihofia tofauti ya umri lakini siku moja akaamua mwenyewe kunieleza hisia zake. Nilishangaa sana mwanamke kunitokea.

Hivyo ndivyo tukajikuta katika mahusiano, Nakiri kwanza kuwa amenisaida mno kumnyoosha binti yangu kitabia na kitaaluma. Hivi ninavyoandika binti yangu anafanya vizuri darasani na ana nidhamu kwangu.

Ni miaka miwili tangu niwe na huyu dada inaelekea watatu lakini kinachonifanya niombe ushauri ni mambo madogo madogo ambayo nayaona kwa huyu dada na yananipa msongo kwa kiasi fulani, sielewi tatizo ni mimi au huyu dada.

Kwasasa tunaishi pamoja, ingawa ana kwake pia ila muda mwingi yuko nyumbani kwangu. Huyu dada hajui kubembelezana na mtu. yaani hana zile hulka za kike kike za mkikosana abembeleze au anune nune hivi. Huyu hana kabisa. Akikosea ataomba radhi hapo hapo na amemaliza. Ukimkaushia imekula kwako kwa kuwa akikutafuta mara mbili tatu ukamchunia ni mpaka utakapoamua wewe kumtafuta na utamkuta poa tu wala hakuulizi kwanini ulimkaushia.

Pili, Ukimkosea hana zile analia au kusema mpenzi wangu umeniumiza na vitu kama hivyo, yeye atakwambia abcd zake na amemaliza. Uombe radhi au upotezee hana habari. Hili jambo ndio huwa linaniacha hoi kabisa. Kuna wakati nilikuwa karibu na mwanamke fulani kazini. Akafuma meseji zenye utata kidogo. Alichofanya aliuliza na mimi nikajitetea kizembe sana ikawa basi, akaingia jikoni kupika na alipotoka uko akawa kama hakuona chochote.

Ni kama vile hana wivu ingawa pia akiona kitu tata anahoji kwa ukali kwelikweli na alishaniambia akichoka vituko atasepa kimoja, na mimi sitaki hilo litokee

Kuna wakati niliamua tu kumjaribu nikamkalia kimya, aliponitafuta nikamwambia nahitaji muda wa kuwa peke yangu. Nilijua labda atanibembeleza nimueleze tatizo. Aliitikia na kukubaliana nami. Huwezi amini alikaa wiki mbili kimya kabisa mpaka nilipoamua kumtafuta. Nikamuuliza kisa cha ukimya, akajibu ulisema unahitaji muda wa kuwa mwenyewe. Nilishangaa mno! Nikamwambia nimerudi. Akajibu karibu hakuuliza tatizo langu wala nini, Nilipomhoji kwanini haulizi hata kwanini nilikuwa kimya. Akanijibu we ni mtu mzima ukiamua utasema. Akaishia hapo.

Niliwahi kumkutanisha na dada yangu, masaa tu aliyokaa naye, aliniuliza huyu dada tutamuweza? Mbona hana bashasha za kiwifi wifi akimaanisha hazoeleki haraka. Marafiki zake ninaowajua ni watatu na sijawazoea kivile maana hata wao hawaelekei kunizoea.

Nikahisi labda anafanya hivi kwa kutafuta ndoa na angenionyesha makucha yake baadaye, nikamwambia mikakati ya ndoa tusitishe kwa sasa. Akajibu sawa wewe ndio muoaji, hakushtuka wala kukasirika. Baadae nikamwambia basi tuharakishe kufunga ndoa, akaniambia naonekana sijui nataka nini hivyo nitulize akili nijiulize kama kweli nataka kuoa na nataka kumuoa nani.

Nimekuwa nikichunguza kama ana mahusiano mengine ya nje, kwa miezi mitatu nilimfuatilia sana na sikugundua kitu chochote zaidi ya kuwa ana ukaribu na watu wenye pesa zao na hadhi kubwa kubwa. nahisi kama ananicontrol bila kujua najikuta namfanyia visa na vituko vya kitoto kila mara mradi tu anipe attention yake hata kama ni kunionyesha hasira ila wapi.

Anaweza akaamua kutokupika, na ukimuuliza anakujibu straight mimi sio wife hapa kwako ni mpenzi tu, nina uhuru wa kuamua kupika au lah. Majibu kama hayo nachoka kabisa ukizingatia nimemzidi miaka 10!

Ana mtoto mmoja ambaye, anaishi kwake pamoja na mdogo wake. Mtoto wa huyu baba yake ni mtu wa nje na hawana hata mawasiliano kwa kuwa hilo nimechunguza pia. Kama ni kunipenda alinitamkia mwenyewe japo mimi pia nilishampenda lakini sielewi kwanini yuko hivi alivyo.

Nifanye nini anionee wivu hata kidogo tu, au awe na hulka za kike, au kama wanawake wengine wanaonyenyekea waume zao aache uandava alionao… nikisema nitumie pesa kumhandle hata yeye anazo kiasi chake na huwa haombi chochote kile na hajawahi kuomba hata senti na nilitegemea na umri wake huo angenipapatikia kidogo ili nimuoe matokeo ni tofauti. Ila nampenda sana huyu dada maana kwenye sekta zingine kama mwanamke sio mtu wa mchezo.
Nioe mimi nikunyooshe,period![emoji21]
Muoe ivo ivo... Yan we una 43 afu bado unaringa ringa. Ukifa bila mke tutakuziba na gunzi kwenye mk**
 
Ni tabia za masingle maza weng hasa waliotelekezwa halafu wakatafta maisha so wanaweza kuish wenyew
 
Mkuu huyo fanya kwel, hutapata tena mtu km huyo. Wanawake wa cku iz shida tupu. Ukishindwana naye nipe mim nimuoe maana ntaishi kwa furaha
 
Nipe mm nimwoe mara moja natafuta wanawake kama hawa ambao wanajitambua sio ambao wapo wapo tu kutwa kupelekwa puta na wanaume wasiojitambua km ww..nipasie best nimalize maana unachezea dhahabu chooni
 
Hashakum na kumRadhi natanguliza.."huu ndiyo UGONJWA mkubwa kwa wTZ, wanapenda kulialia, kulaumu, kununa nuna, kutunga Usanii, kufura/kuvimba nk ilimradi apewe attension na aachiwe bure alilofanya !! huu utamaduni umepitwa na wakati....

bigmomkipipa kuwa GENTLEMAN bhana...
Yani mbaba wa miaka yake kadhaa eti ananuna ili aulizwe like seriously? Unajua kuna umri unafika unaact kuendana na umri sasa anataka abembelezwe aulizwe ulizwe yani aiseee mambo mengine sio kabisa.Bidada kamuona kwa huo umri wake hastaili kufanyiwa drama za secondary ila baba wa watu ndio anataka kuanza kuonewa wivu na kununiwa[emoji1]
 
Mkuu.....
Kwa hayo yote ulio yataja kuhusu huyo mwanamke wako... naomba siku ukimchoka unistue, maana mimi nina tafuta mwanamke wa aina hiyo.
 
Back
Top Bottom