In a nutshell: Magufuli anaonekana na watanzania kama mtu hodari na mchapakazi, kiuhalisia mimi naona kinyume chake.
Binafsi si msafiishaji wala sina uhusiano wowote na sekta hiyo , lakini ninasafiri sana kwa barabara nchi karibu zote za SADC, Suala la mizani na sheria zake zinazidi Kuwa tight hapa kwetu pengine kuliko nchi nyingine za sadc, na pengine ndo tunaongoza kwa rate ya uharibifu wa barabara kuliko wenzetu kwa sababu ya ubabe wa mtu mmoja tu, MAGUFULI !!!
Uharibifu wa barabara kwa kiasi kikubwa unatokana na sheria mbovu zilizowekwa na kusimamiwa na viongozi husika, kulalamkikia wasafirishaji ni sawa na kuficha ukweli wa tatizo, si kweli kuwa tunabeba mizigo mizito sana. Bali tuna utaratibu mbaya wa kubeba mizigo ndo maana barabara zetu hazidumu.
Kuna mawili huwa nafikiri dhidi ya wizara hii na watendaji wake: Either wananufaika na rushwa kutoka kwa wasafirishaji hivyo wanaopt njia ambazo hazitatui tatizo bali kuiongezea mzigo serikali na mtu wa kawaida au hawajui na hawako serious kuboresha pengne kuondoa kabisa sheria kandamizi zinazopelekea watu kutocomply.
Mfano: Botswana idadi ya juu ya axle ni 9 urefu mwanzo hadi mwisho ni mita 22, hapa kwetu ni axle 7 na urefu hautakiwi kuzidi mita 17!!! Put it simple: napokuwa na axle nyingi ndio unavyozidi kutetea barabara na the opposite is also true,
Ningekuwa mimi ndo Magufuli ningejiuliza swali moja -kwanini South Africa wanabeba mizigo mizito yet road network zao zina lifespan kubwa kuliko zetu na pia hawana idadi kubwa ya mizani kama sisi. Na bado wakifika Tunduma wanaona ni afadhali ku-offload mizigo na kupakia kwenye malori yetu??
Hivi kuna hasara gani TANROADS ikiruhusu axle 9 na urefu ukawa 22 metre! !! Kwanini Trailers za Interlink ambazo zinatuika karibu Africa nzima hapa kwetu ni marufuku? Remember: Australia wanabeba mpaka tani 80 kwa kuongeza idadi ya axle na kuto limit urefu! Na bado barabara zao zinadumu.